Precision Air, hii ndio Customer Care mliyofunzwa?

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,323
18,793
Nimebook flight ya wageni wangu kutoka Arusha kwenda Zanzibar na kurudi Arusha.....mmewapeleka vizuri........siku ya kurudi nimere-confirm na mkanihakikishia hiyo flight ipo.......wageni wangu wamecheck in saa 1215......kumbe mmecancel hiyo flight lakini hamkuwaambia........kwa nini wakati wana check in hamkuwaeleza wakarudi kufanya shuguli zingine.....?....hilo mnalijua wenyewe......

Watu wamekaa airport kuanzia saa tano mpaka saa kumi na mbili jioni kusubiri flight ya kutoka Zanzibar-Dar-Jro.....na route ilikuwa ni Znz-Dar-Ars.....nyie ni kina nani mpaka muharibu mipango ya watu.....?......kwa shingo upande walikubali huo upuuzi wenu kwa sababu hawakuwa na la kufanya......

Wamefika Dar wakaconnect vizuri mpaka JRO.....wamefika saa nne usiku.....hapo mliwahakikishia kuwa shuttle yenu itawasubiri kuwapeleka mjini kwa sababu kwanza mmewapotezea muda na mmewachosha......kufika JRO mnawaambia kuwa shuttle imeshaondoka kwa hiyo wakodi tax....really.....!!......bahati mbaya mlikuta wapo ngarangari.....likawashuka.....mkawakodia tax....ok wapeni basi mizigo yao waende.....khaaa....mmeiacha Dar.......what the f**k was that....!!....saa sita usiku.........kweli mmefuzu taaluma ya u-customer care.........kesho yake mkawaletea mizigo yao but hamkuwaomba hata radhi ya usumbufu.......man***na.......

Sasa basi.....wageni hao hao baada ya week na nusu wanarudi kwao.......wanakwenda Nairobi kuconnect international flight....mmewahakikishia shuttle yenu itaondoka saa tisa na nusu usiku kuwapeleka JRO.......tisa kamili wawe wamefika kituoni kwenu......usiku kama huo mtu hajalala.......ameamka kwenda kuwahi flight......kumbe hiyo shuttle haipo....mmecancell bila kusema.....mnapigiwa simu hampokei.....kweli......?......mlitegemea mtu afanye nini wakati huo ili hali taarifa hamkumpa.......?

Siwaharibii biashara lakini siku nikisikia mtu anasema anataka kufly na nyie......nitamkataza hata kwa kuvua nguo.......

ASANTENI SANA KWA HUDUMA YENU NZURI.......
Naamini kupitia JF ujumbe wangu umewafikia..........

 
Pole preta unajua mentality ya customer care bado sana.

kwa sababu wanajua hapa kwetu hakuna wa kumlalamikia.......sasa wasubiri hao walioenda kwao sijui watarudi na maoni gani........
 
Hawa jamaa kuna siku kutoka zanzibar kwenda dar asubuhi tumeshacheck in, baadae tunaambiwa ndege hamna. Tukakusanyika abiria wa ndege tatu, wakaleta ndege moja tu, pia tukatangaziwa wale wa international flights tu ndo wapande sisi tusubiri!,ndege inagombaniwa kama daladala ya mbagala. Tukakodishiwa kandege kadoogo, ilikuwa ndege ya polisi ile inabeba abiria wanne tu! zanzibar kwenda dar nusu saa! huwa nikikumbuka kwakweli nabaki kucheka tu. Pole sana preta. Wazoee!!!
 
Hawa ni wahuni tu! Dawa yao inachemka maana wamekuwa zaidi ya kiburi.
 
manina me ningeenda hadi kwa yule managing director wao kushitaki usipende kuvumilia sana upuuzi kama huu
 
manina me ningeenda hadi kwa yule managing director wao kushitaki usipende kuvumilia sana upuuzi kama huu

MD wao ndio huyo anaitwa Shirima........?.......kama kuna mwenye namba yake ya simu atusaidie hapa........ili next time tujue cha kufanya........
 
Nilishawahi kuwapigia customer care, nikaanza kwa kujitambulisha jina, akanijibu "kwahiyo?"....seriously!!!?
 
MD wao ndio huyo anaitwa Shirima........?.......kama kuna mwenye namba yake ya simu atusaidie hapa........ili next time tujue cha kufanya........

Pole mkuu lakini hawa watuwashalalanikiwa sana ku cancel flights ni kipaji chao ndo maana unaambiwa bora u book fastjet tu maana wako on time kama jro zanzibar fresh tu
 
Wageni hawa ni wamisionari nini mbona wapole sana..

hebu niambie unafanyaje hapo......upo mbali na kwenu......usafiri unaoutegemea ni huo......umetoka holiday umezitafuna haswa........unafanyaje.....?
 
Hawa jamaa kuna siku kutoka zanzibar kwenda dar asubuhi tumeshacheck in, baadae tunaambiwa ndege hamna. Tukakusanyika abiria wa ndege tatu, wakaleta ndege moja tu, pia tukatangaziwa wale wa international flights tu ndo wapande sisi tusubiri!,ndege inagombaniwa kama daladala ya mbagala. Tukakodishiwa kandege kadoogo, ilikuwa ndege ya polisi ile inabeba abiria wanne tu! zanzibar kwenda dar nusu saa! huwa nikikumbuka kwakweli nabaki kucheka tu. Pole sana preta. Wazoee!!!

lol hadi nimecheka....kweli thr is no hurry in Africa....foleni hadi kwenye ndege......majanga
 
Mwakyembe na spidi zake zisizoeleweka kuhusu ATC zinafanya tuzidi kuamini pamemshinda.

Mikwara yote ile ATC bado inazidiwa hata na UDA.Hili linchi limeoza rushwa ndio maana hawa wahuni Precision Air wanakuwa na tabia kama za manesi wa government hospital.
 
siku hizi kikosea lazma uione kazzi yako ngumu. Wafanyakazi wa Precision wanahali mbaya basi tu wanavumilia jamani, mda mwingine wanaambuliamatusi hadi huruma. ukija kuangalia shirika sio lao, kazi wanitaka maskini af mabosi ndio wanakaa kimya bila kutatua mataizo ya wateja... lawama zote kwao. Tuwahurumie basi jamani...
ILA PUMB*VU ZAO, WALIKUWA WANARINGA SANA KIPINDI WANAOPERATE VIZURI HAWA, TENA WA KUWACHAPA MAKOFI KABISA
 
tatizo wako wenyewe tu, kwa hiyo hata mlalamike vipi hawajali, nawafananisha na KQ, kenya Airways, hawa nao balaa nadhani hawa katika joint venture yao ndio waliowaambukiza PW, ila PW ni majanga kwa kweli
 
Back
Top Bottom