Katika gazeti la Guardian ya leo, PPF wametoa tangazo la kumfukuza kazi Bi. Gisella Mhoro. Dada huyu alinin'gang'ania sana mwaka jana tumkatie mafao yetu ili aweze kutoa cheque zetu. Nawapongeza sana PPF kwa kumnasa dada huyu. Mafao ni jasho la mtu, haliliwi hovyo. Natoa mwito kwa PPF wasiishie hapo bali waendelee kuwachunguza wengine.
hivi jamani, fao la kujitoa limeanza kutolewa niamkie ubungo kesho???? naombeni kujuzwa plzzzzzz
Makubwa Kafukuzwa na Ijumaa kakamatwa na polisi.adi jana alikuwa anasota rumande jamani omba Mungu asikupe uroho na tamaa ya pesa.Maana huyoo mama alikuwa na kila kitu na mme wake ni mwanajeshi.ila safari hii PPF wamemkamata utamu.28Mls zimuponza.Watatajana vizuri pana chezea pesa za mafao ya watu.
Ipo kweli na lidandasi limepita 50 out.ila yeye kaondolewa kabla ya lindandasi.mijihelaa ilimnogea jamani na barua ya kufukuzwa kazi alipelekewa home akagoma kupokea.wakamlazimisha na kusaini kupokea.ween unakataa kupokea barua yako mbona pesa za manuva unapokea.Kazi ipo hapo kaitaka mwenyewe! Nilimwambia mafao ya uzeeni ni ya mtu husika...Ukila yatakuponza!
Ipo kweli na lidandasi limepita 50 out.ila yeye kaondolewa kabla ya lindandasi.mijihelaa ilimnogea jamani na barua ya kufukuzwa kazi alipelekewa home akagoma kupokea.wakamlazimisha na kusaini kupokea.ween unakataa kupokea barua yako mbona pesa za manuva unapokea.
Yule mama alikua mroho kweli...Nakumbuka jamaa yangu ambaye nae alikua akifuatilia mafao alisema yule danda angelikua mzuri halafu apende hela kihivyo angemumwambia wakutane Magomeni amtere kwanza halafu ammegee mafao....Lakini muonekano wa yule dada ulimtisha.....Nadhani waliobaki watakuwa na nidhamu. Kwa vile muda wa mafao yangu umekaribia tena, nitakuja nicheck kama kuna kimbelembele aliebaki..
Wamesahau kwamba huyo Gisella ni sehemu ya mtandao mrefu wa wizi. Kwa kufanya hivyo haitakuwa mwisho. suala hapa ni kuukata mtandao mzima kuanzia chini kwenda juu. Ni sawa sawa na Rais wa nchi anayesema atapambana na mafisadi wakati yeye ni zao ama "product" ya mtandao wa mafisadi na yupo kwa ajili ya kuwatetea na kuwalinda.....Kwa hiyo suala hapo ni kusafisha tuu. Sio longo longo la kutuchezea cheusi chekundu wavuja jasho wa nchi hii..