Post election situation - prediction | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Post election situation - prediction

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by TIMING, Oct 30, 2010.

 1. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wakuu... Kesho tunapiga kura kuchagua rais, wabunge na madiwa... regardless of results, nchi itaendelea kuwepo na nadhani tukisie kidogo baadi ya matukio muhimu

  Mimi ntaanza na hali ya fedha, kwa sasa naona wahisani wamepiga pini fulani kwenye GBS na hivyo serikali imelazimika kujipapasa kwueza kulipa mishahara (and a few overheads); kwa hili hongera serikali

  Tukimaliza kura kuna mawili
  la kwanza lililo obvious in anxiety ya watanzania kwani haijawahi kutokea campaigns kama hizi na mwamko wa hali ya juu toka kwa wapinzani, pia tupongeze kikwete kwa kutoa uhuru huu ingawa kwa kiasi fulani kuna mambumbumbu wa modern life kama TBC waliendelea kujibana (of course vyeo vyao ni vya kupewa, competence ndogo).... hii anxiety, makisio yangu ni kwamba haitatufikisha wkenye vurugu hata majibu yaweje, vurugu zitatokea sehemu chache za mijini

  la pili na la maana sana ni kusubiri serikali mpya.... kwangu binafsi hapa ndipo nina wasiwasi
  sitegemei chama chochote kwana serikali iliyo strong kwenye kila idara, laki kusema ukweli kama ni chadema ntaomba muwe na serikali ya kitaifa, kama ni kafu pia na kama ni ccm hivyohivyo au kama mtaona haifai, basi toeni mawaziri wote waliolalamikiwa

  Pia naombeni mrudishe hadhi ya makatibu wakuu wa wizara na kuwaacha mawaziri wawe kama enzi za mkapa

  Je wenzangu mnapredict nini??
  Amani? Vurugu? uchumi kukua? whisani kufunguka??

  Amen
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Acid

  la kwanza ni prediction lakini la pili hapo kaa ni maombi yako binafsi hivi.
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  1. Nishawishi niamini kuwa Serikali yetu inategemea fedha za misaada kulipa mishahara ya watumishi

  2. Hili la vyombo vya habari serikali inahitaji kupongezwa ingawaje inawezekana ikawa ni shinikizo la hao wanaotoa pesa za mishahara kama ulivyoteta.

  3. Hapa kama Waingereza wanabana matumizi, yeyote atakayeshinda hana budi kuunda serikali ndogo yenye tija ili kupunguza matumizi ya kawaida na kuongeza matumizi ya maendeleo. Uanzishwaji wa mikoa na wilaya mpya nadhani ndani ya miaka mitano ijayo kuna haja ya kusitishwa.

  4. Kuwa na mawaziri wanaofyata mbele ya bosi wao huo siyo uongozi. Raisi ajaye anatakiwa kuchagua mawaziri wenye kuthubutu kama Mh. Magufuli au Lyatonga Mrema ili nchi isonge mbele kimaendeleo.

  5. Mapungufu nayotabiri ni kuwa bunge lijalo litakuwa halina uwezo wa kusimamia Serikali ipasavyo kwani Spika ajaye ataweka mbele maslahi ya chama na hivyo kuminya uhuru wa wabunge kuikosoa serikali yao.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  @augustino... Rejea gbs records na percentage funding... ntashare docs kadhaa na wewe later, kwa sasa fungu gumu ila tupongeze ujasiri
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mimi nachokumbuka bajeti ya matumizi ya kawaida kwa 100% inatoka katika mapato yetu ya ndani. Ile ya maendeleo ndiyo inategemea wafadhili, na hoja ya wapinzani kama utakumbukua ilikuwa nchi haiwezi kuendelea kama bajeti ya maendeleo kwa zaidi ya 50% inategemea wafadhili ambao nao wanachangamoto zao kama inavyotokea Ufaransa na Uingereza
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Vincent, nimefanya homework yangu na ukweli ni kwamba salaries zote zinatoka serikalini, ila impact ya donors support kwenye GBS ni pale walioacha kutoa pesa kwa sasa na inafanya gv=overnment kuwa na mzigo kwani hata uchaguzi wenyewe una gharama kubwa sana kwenye posho, ulinzi nk...

  Kwahiyo basi sasa, ingawa salary hawalipi, kitendo cha donors kubana, kunaitesa serikali kimtindo
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Unachosema ni kweli. Lakini tatizo linakuja kwenye 'liquidity' (nimesahau kidogo kiswahili chake!). Kuchelewa kupata pesa kutoka kwa donors kunaweza kuleta matatizo makubwa ya mzunguko wa fedha hasa ukizingatia pesa nyingi zimetumika kwenye shughuli zinazoambatana na uchaguzi.
   
Loading...