Tuna namna moja tu ya kudhibiti utendaji mbovu wa watumishi wa mahospitalini na kwenye taasis zingine

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,638
5,145
Nitolee mfano Morogoro referral hospital, utendaji wa madaktari na wauguzi ni mbovu sana. Rushwa, neglegence, wizi wa dawa, impolite languages za wauguzi na baadhi ya madaktari, yaani vurugu tupu kwenye hospital iliyo katikati ya jiji morogoro.

Kwavile mfumo wa opras wa kutathimini utendaji wa wafanyakazi wa serikali ulishindwa napendekeza wapewa huduma (mgonjwa aliyetibiwa) ndio watoe tathimini ya utendaji wa mtoa huduma za afya kwenye hospital husika.

Yaani iwe hivi. Kwa upande wa hospitals, Baada ya matibabu , HR wa hospitals wawe na form inayo ruhusu kujazwa jina na performance score ya mhudumu husika na kama huduma aliyotoa inaridhisha au la. Mhuduma au daktari mwenye poor performance rating kutoka kwa majority ya wateja ashushwe cheo au asipate promotion. Muuguzi au daktari mwenye record nzuri toka kwa wateja awe promoted na awe awarded kama mfanyakazi bora. Yaani assessment ya wapokea huduma ibebe points nyingi kwenye vigezo vya promotion. Utaratibu huu utumike hivo hivo kwenye taasis zingine za umma kama polis, uhamiaji, tra, bandarini, posts, nk.

Tayari utaratibu huu upo kwenye baadhi ya level za utumishi na taasis na kwenye siasa. Ni namna tu ya kuupeleka na Maeneo mengine.

Mfano, kwenye siasa. Mantiki ya uchaguzi wa rais na wabunge kila Baada ya 5 years nikwamba hao watumishi waanatathiminiwa na wananchi Baada ya miaka mitano kuisha. utendaji ukiwa mbovu wataondolewa na raia anaowatumikia.

Utendaji wa mawaziri na nakaribia wakuu, wakuu wa wilaya na mikoa, wakurugenzi, unatathiminiwa na raisi aliye wateua.

Pia huu mfumo upo vyuo vikuu. Moja ya points for promotion ya waalimu universities zinatoka kwa wanafunzi. Ukipata poor rating toka kwa wanafunzi imekula kwako.

So napendekeza siye wapewa huduma tupewe rungu laku judge peromance ya mtumishi wa umma. Mwajiri wake ampromote au demote kutokana na performance rating zetu. Hii itaboresha utendaji kazi kwenye taasis za umma hasa kwenye hospitals za umma zilizo jaa uozo
 
On point
pia uwepo mfumo mzuri wa kuwashughulikia wabadhirifu na wezi wa mali za imma.

Maana siku hizi mtu Ili aonekane mjanja awe mpigaji kwenye kitengo alichokabidhiwa wale waadilifu wanaonekana majuha na mataahira Kwa kushindwa kupiga madeal mbalimbali.
 
Tatizo nipo sehemu nauguza. Ningeweza kuandika hapa namna nzima huu mfumo unaweza kutekelezwa kwenye taasis mbalimbali
 
Shida ni usimamizi wa OPRAS, mfumo ni mzuri sana ukitekelezwa vile inatakiwa.

Wakuu wa vitengo hawaufahamu mfumo huu ipasavyo malengo wanayoweka hayapimiki na wakuu wanaowasamia wenzao hawako reaponsible hivyo wanajaza zile fomu kama fomality tu hazina tija.

Ukiona mtu amejaziwa vibaya huyo alitofautiana na kiongozi wake na si kwamba hajatimiza malengo.

Lakini pia hata maHR wa Serikali hawajui namna ya kusaidia masupervisor kusimamia performance au utendaji.

Ww HR wa taasisi unapokea fomu kutoka kwa idara mbali mbali fomu hazina malengo yanayopimika, malengo sio halisi na huchukui hatua hata ya kusadisi why iko hivyo ili uweze kuona je wafundishwe upya au nini kifanyike.

Kwa ujumla huu mfumo ni mzuri sana kwenye makaratasi ila utekelezaji ni zero.

Huwa nafikiria hata kuchukua makatibu wakuu vyuoni nayo si sawa hawa wamezoea kuhubiri sio kutenda. Sijui km katibu Mkuu utumishi amewahi kureview kwa kutumia wataalam kuona km Perfomance Management System inafanya kazi au nini kiboreshwe yupo tu.

Si hilo tu kuna taasisi za serikali ziko overstaffed na nyingine understaffed before kuajiri ilitakiwa tubalance wafanyakazi waliopo ili tuwe na matumizi sahihi ya rasilimali zetu. Katibu Mkuu utumishi yupo tu sijui tutamkumbuka kwa lipi anyway labda kusaini barua though hii hata ofisi attendant anaweza.

Taasisi zinapoomba ajira ni nani anashughulika na ikama. Ni kitengo gani kiko responsible kujua taasisi ya malengo haya inahitaji watumishi kadhaa kwenye kitengo hiki na kadhaa kwenye kitengo kile kulingana na duties zilizopo, sijui hii pia nani anafanya taasisi zinaomba tu wafanyakazi without justification ya gaps zilizopo na katibu mkuu yupo tu.
 
Well said mkuu. Mambo ni mengi. Mfumo opras una changamoto nyingi including ulizozitaja. Sehemu yangu ya kazi watu kadhaa hawajawahi kuzielewa opras . Walikua wanaomba msaada kujaziwa. Kama inaweza ukawa hivyo sehemu zingine kwenye utumishi wa umma unaweza ona jinsi gani huo ni usanii? Acha assessment zifanywe na wanaopokea huduma
 
Back
Top Bottom