Nashauri Mawaziri kuchuja maneno na kauli kabla ya kuzungumza mbele ya Umma ili kutoleta taharuki

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,280
9,719
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hekima na unyenyekevu mkubwa sana,kwa upendo na heshima kubwa sana na uzalendo wa hali ya juu sana ningependa kutoa rai na ushauri wangu kwa viongozi wangu hasa Mawaziri kuchunga sana ndimi zao,vinywa vyao kabla ya kutoa maneno ,matamshi na kauli kwa umma au hadharani. Hii ni kwa kuwa Waziri ni kiongozi wa juu sana katika ngazi ya uongozi wa Taifa letu,ni mjumbe wa baraza la mawaziri chombo cha juu kabisa kiuongozi,ni sehemu ya chombo kinachomshauri Mheshimiwa Rais katika masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Hivyo wajumbe wake au mjumbe wake anatarajiwa kuwa mwenye hekima, busara, unyenyekevu, uzalendo, utulivu, uvumilivu, utii kwa Taifa lake na makini katika mambo yake.kwa sababu maneno ya waziri yana athari kubwa sana katika jamii tofauti yakitolewa na mtu wa chini yake ndani ya wizara kwa kuwa yanaweza kuleta taharuki, sintofahamu na Mjadala unaoweza chochea hata chuki kwa serikali yote na wakati mwingine mashambulizi yakaelekezwa kwa Rais mwenyewe ambaye ndiye mteuaji. Ndio maana ni muhimu sana waziri kama hana neno au taarifa za kutosha na rasmi juu ya jambo fulani ni bora aka kaa kimya kujipa muda kabla ya kutoa au kufanya maamuzi au kutoa maelekezo au kauli au maagizo.

Mfano nimeisikia kauli ya Mheshimiwa waziri mmoja akisema kuwa haitaruhusiwa kwa mtanzania kuingia na jezi ya timu pinzani uwanjani wakati timu mgeni ikija kucheza na club zetu za hapa nyumbani ,kwa kuwa utakuwa siyo uzalendo. Kwanza ningependa kusema kuwa uzalendo haupo na haukai katika jezi au rangi ya nguo au tisheti aliyovaa mtu.uzalendo upo katika moyo wa mtu ambao utajionesha nje kupitia matendo.hii ndio maana kuna watu wana kaa maofisini tena ofisi kubwa na za hadhi kubwa lakini wanafanya ufisadi,wanapokea rushwa na kuiba mali za umma ikiwepo pesa au kusaini vitu kwa maslahi binafsi huku ukutani mwa ofisi zao kukiwa na Picha ya Rais ikiwatizama.

Wapo wengine wanapokea rushwa kutoka kwa maskini bila hofu ya aina yoyote ile huku katika viuno vyao wakiwa wamevaa mkanda wenye rangi ya bendera ya Taifa. Kwa hiyo ni lazima tujifunze kupanda mbegu za uzalendo katika mioyo ya watu wetu na siyo kuupima uzalendo wa mtu kwa kuangalia mavazi aliyo yavaa.maana kama nimavazi ndio yangekuwa ni kipimo na tafsiri ya uzalendo basi tungekuwa tunaamua tu vazi fulani wavae viongozi wetu ili wafanye mambo yao kwa uzalendo.

Maana katika suala la jezi wapo watu mitaani utakuta anajezi ama tisheti ameinunua kama sehemu tu ya mavazi yake na wala siyo kwa kuwa ni mshabiki wa timu hiyo.mwingine anaweza ipenda mwonekano tu au rangi yake tu.ndio maana unaweza mkuta mtu amejivalia zake leo jezi ya man u au man city au Liverpool kutoka uingereza ,au Madrid au Barcelona kutoka Spain au Chelsea kutoka Uingereza au psg kutoka Ufaransa au Dortmund kutoka Ujerumani au ajax kutoka uholanzi au Maccab Tel Aviv au Maccab Haifa kutoka Israel au Porto kutoka ureno au juve au Roma au Intermilan kutoka italy. Mtu anavaa tu japo siyo Raia wa nchi mojawapo ya ulaya na wala hajawahi kufika ulaya.

Mimi mwenyewe japo ni mshabiki wa Dar Yanga Afrika lakini kuna wakati nimevaa sana jezi ya man u japo sikuwa mshabiki wa man u lakini nilinunua na niliivaa tu kama sehemu ya nguo yangu kama zilivyo zingine.kwa hiyo kumzuia mtu kwasababu amevaa jezi ya club nyingine mtu aliyelipia tiketi kutizama mchezo huo inakuwa siyo sawa na ni kumuonea sana na kujenga chuki na hasira kwa watu zisizo na sababu ya aina yoyote ile..kwa sababu hakuna mahali sheria inapokataza mtu kufanya hivyo. Lakini pia inakuwa ni kupoteza na kuondoa Radha ya mpira ambao siku zote ni burudani, furaha na utani na siyo amri amri tu. Utani na kuzodoana kwa simba na yanga ndiko kumefanya club zetu hizi kupata mafanikio yanaonekana leo hii ,maana kila mchezaji akiingia uwanjani anataka kupambana sana ili timu yake ipate ushindi na kuwapa raha mashabiki wake wanaokuwa wamefurika uwanjani dhidi ya wale wanaokuwa wapinzani wao bila kujali ni watanzania waliovaa jezi za timu pinzani kutoka nje au ni wa kutoka nje moja kwa moja.

Uzalendo ni lazima tuusisitize kwenye timu za Taifa maana huko tunaunganishwa na Utaifa wetu na utanzania wetu lakini siyo huku kwenye club.huku tuombeanage tu zote zisongage mbele ili sifa zijage sana Tanzania na kuipa nchi nafasi ya kujitangaza na hata serikali kuchukua nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii .kama ambavyo simba kwenye jezi zao waliandika kuwa Visit Tanzania.uzalendo tuusisitize lakini si katika namna hii ya kupangiana hadi aina ya nguo za kuvaa kwa ngazi za mashindano ya Club .sisi wenyewe huwa tukienda nje ya nchi wakati mwingine tunapata washabiki huko huko wa ugenini wanaokuwa nao wanataka wapinzani wao watoke.

Kikubwa ambacho kingesisitiizwa ni kuwa hawa watakao vaa jezi za timu pinzani basi wakae eneo lao na siyo kwenda kukaa kwenye mashabiki wa club nyingine ili kuepusha vurugu zinazoweza kutokea hasa kutoka kwa wale waliofungwa.na hivyo kufanya au kuchochea au kupelekea uharibifu wa miundombinu ya uwanjani kama vile kung'oa viti, kurushiana chupa za maji , kupigana ngumi na wakati mwingine kuharibu hata utulivu wa mchezo wenyewe na hata kupelekea vifo. Mpira ni uwekezaji kwa hiyo tuendelee kusisitiza na kujikita katika uwekezaji na kuvutia wawekezaji katika Secta ya michezo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Nchi hii baadhi ya watu wana mihemko ya kipuuzi, Waziri hakuna alicho kosea yuko sahihi.
Huna haja ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayo tokea nje ya nchi ukiwa uwanjani.

Unaweza kushangilia iyo timu pinzani bila kuvaa jezi, Jezi yako kavae mtaani au kwako ui burudishe nafsi yako.

Nenda uwanjani kashangilie timu uipendayo(pinzani) hakuna atakaye kusumbua.

Waziri katika nafasiyake angalau ameonyesha kutokubaliana na mambo ya kipumbavu na ame kemea na wapo Watanzania wengi wame muunga mkono kwa jambo ilo.
 
LEO umeandika madini sana, mimi nashangaa wazirii anasisitiza uzalendo kwenye club hizi za Dar ambazo wachezaji wengi wanatokea nje ya nchi. Nafikiri serikali ijitoe huku maana kwenye huu mchezo tukienda kwa amri tutaondoa ladha ya mchezo burudani
 
Mimi nilivyomuelewa waziri, watanzania wasivae hiyo jezi kwa siku ya mchezo huo kama mashabiki wa upande huo. Badala yake watanzania wapenda michezo wawe wazalendo na timu zao.
 
Nchi hii baadhi ya watu wana mihemko ya kipuuzi, Waziri hakuna alicho kosea yuko sahihi.
Huna haja ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayo tokea nje ya nchi ukiwa uwanjani.

Unaweza kushangilia iyo timu pinzani bila kuvaa jezi, Jezi yako kavae mtaani au kwako ui burudishe nafsi yako.

Nenda uwanjani kashangilie timu uipendayo(pinzani) hakuna atakaye kusumbua.

Waziri katika nafasiyake angalau ameonyesha kutokubaliana na mambo ya kipumbavu na ame kemea na wapo Watanzania wengi wame muunga mkono kwa jambo ilo.
Wewe na wazir wote ni wapumbavu mnafanana akili.
Kwani mamelodi ni timu ya taifa? Kwani tunavyoshabikia Man U au Liverpool mbona akatazi?
Yaani Jezi ninunue kwa pesa yangu, nikate tiketi kwa pesa yangu Halafu uniletee upumbavu!
Naval Jezi ya Al ahly au mamelodi huwezi kunilazimisha nivae simba na yanga.
Kwa sheria gani ya mpira? Kwa sheria gani ya nchi nimevunja?
Acha CCM waendelee kutawala sababu si viongozi wala raia kama wewe wamejaa makamasi kichwani
 
Nchi hii baadhi ya watu wana mihemko ya kipuuzi, Waziri hakuna alicho kosea yuko sahihi.
Huna haja ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayo tokea nje ya nchi ukiwa uwanjani.

Unaweza kushangilia iyo timu pinzani bila kuvaa jezi, Jezi yako kavae mtaani au kwako ui burudishe nafsi yako.

Nenda uwanjani kashangilie timu uipendayo(pinzani) hakuna atakaye kusumbua.

Waziri katika nafasiyake angalau ameonyesha kutokubaliana na mambo ya kipumbavu na ame kemea na wapo Watanzania wengi wame muunga mkono kwa jambo ilo.
Ww ndo mpumbavu ndani ya nchi hii kila mtu yuko huru kufuata mtazamo wake anao uona ni sawa lamsingi uwe hauvunji sheria za nchi.

Huwezi nirazimisha nipende kitu nisicho kipenda.
Alafu timu haishindi kwa sababu ya mashabiki wazalendo bali ina shinda kwa uwekezaji ndani na nje ya uwanja.
 
Safi
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hekima na unyenyekevu mkubwa sana,kwa upendo na heshima kubwa sana na uzalendo wa hali ya juu sana ningependa kutoa rai na ushauri wangu kwa viongozi wangu hasa Mawaziri kuchunga sana ndimi zao,vinywa vyao kabla ya kutoa maneno ,matamshi na kauli kwa umma au hadharani. Hii ni kwa kuwa Waziri ni kiongozi wa juu sana katika ngazi ya uongozi wa Taifa letu,ni mjumbe wa baraza la mawaziri chombo cha juu kabisa kiuongozi,ni sehemu ya chombo kinachomshauri Mheshimiwa Rais katika masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Hivyo wajumbe wake au mjumbe wake anatarajiwa kuwa mwenye hekima,busara, unyenyekevu,uzalendo,utulivu, uvumilivu,utii kwa Taifa lake na makini katika mambo yake.kwa sababu maneno ya waziri yana athari kubwa sana katika jamii tofauti yakitolewa na mtu wa chini yake ndani ya wizara.. Kwa kuwa yanaweza kuleta taharuki, sintofahamu na Mjadala unaoweza chochea hata chuki kwa serikali yote na wakati mwingine mashambulizi yakaelekezwa kwa Rais mwenyewe ambaye ndiye mteuaji. Ndio maana ni muhimu sana waziri kama hana neno au taarifa za kutosha na rasmi juu ya jambo fulani ni bora aka kaa kimya kujipa muda kabla ya kutoa au kufanya maamuzi au kutoa maelekezo au kauli au maagizo.

Mfano nimeisikia kauli ya Mheshimiwa waziri mmoja akisema kuwa haitaruhusiwa kwa mtanzania kuingia na jezi ya timu pinzani uwanjani wakati timu mgeni ikija kucheza na club zetu za hapa nyumbani ,kwa kuwa utakuwa siyo uzalendo. Kwanza ningependa kusema kuwa uzalendo haupo na haukai katika jezi au rangi ya nguo au tisheti aliyovaa mtu.uzalendo upo katika moyo wa mtu ambao utajionesha nje kupitia matendo.hii ndio maana kuna watu wana kaa maofisini tena ofisi kubwa na za hadhi kubwa lakini wanafanya ufisadi,wanapokea rushwa na kuiba mali za umma ikiwepo pesa au kusaini vitu kwa maslahi binafsi huku ukutani mwa ofisi zao kukiwa na Picha ya Rais ikiwatizama.

Wapo wengine wanapokea rushwa kutoka kwa maskini bila hofu ya aina yoyote ile huku katika viuno vyao wakiwa wamevaa mkanda wenye rangi ya bendera ya Taifa. Kwa hiyo ni lazima tujifunze kupanda mbegu za uzalendo katika mioyo ya watu wetu na siyo kuupima uzalendo wa mtu kwa kuangalia mavazi aliyo yavaa.maana kama nimavazi ndio yangekuwa ni kipimo na tafsiri ya uzalendo basi tungekuwa tunaamua tu vazi fulani wavae viongozi wetu ili wafanye mambo yao kwa uzalendo.

Maana katika suala la jezi wapo watu mitaani utakuta anajezi ama tisheti ameinunua kama sehemu tu ya mavazi yake na wala siyo kwa kuwa ni mshabiki wa timu hiyo.mwingine anaweza ipenda mwonekano tu au rangi yake tu.ndio maana unaweza mkuta mtu amejivalia zake leo jezi ya man u au man city au Liverpool kutoka uingereza ,au Madrid au Barcelona kutoka Spain au Chelsea kutoka Uingereza au psg kutoka Ufaransa au Dortmund kutoka Ujerumani au ajax kutoka uholanzi au Maccab Tel Aviv au Maccab Haifa kutoka Israel au Porto kutoka ureno au juve au Roma au Intermilan kutoka italy. Mtu anavaa tu japo siyo Raia wa nchi mojawapo ya ulaya na wala hajawahi kufika ulaya.

Mimi mwenyewe japo ni mshabiki wa Dar Yanga Afrika lakini kuna wakati nimevaa sana jezi ya man u japo sikuwa mshabiki wa man u lakini nilinunua na niliivaa tu kama sehemu ya nguo yangu kama zilivyo zingine.kwa hiyo kumzuia mtu kwasababu amevaa jezi ya club nyingine mtu aliyelipia tiketi kutizama mchezo huo inakuwa siyo sawa na ni kumuonea sana na kujenga chuki na hasira kwa watu zisizo na sababu ya aina yoyote ile..kwa sababu hakuna mahali sheria inapokataza mtu kufanya hivyo. Lakini pia inakuwa ni kupoteza na kuondoa Radha ya mpira ambao siku zote ni burudani ,furaha na utani na siyo amri amri tu .utani na kuzodoana kwa simba na yanga ndiko kumefanya club zetu hizi kupata mafanikio yanaonekana leo hii ,maana kila mchezaji akiingia uwanjani anataka kupambana sana ili timu yake ipate ushindi na kuwapa raha mashabiki wake wanaokuwa wamefurika uwanjani dhidi ya wale wanaokuwa wapinzani wao bila kujali ni watanzania waliovaa jezi za timu pinzani kutoka nje au ni wa kutoka nje moja kwa moja.

Uzalendo ni lazima tuusisitize kwenye timu za Taifa maana huko tunaunganishwa na Utaifa wetu na utanzania wetu lakini siyo huku kwenye club.huku tuombeanage tu zote zisongage mbele ili sifa zijage sana Tanzania na kuipa nchi nafasi ya kujitangaza na hata serikali kuchukua nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii .kama ambavyo simba kwenye jezi zao waliandika kuwa Visit Tanzania.uzalendo tuusisitize lakini si katika namna hii ya kupangiana hadi aina ya nguo za kuvaa kwa ngazi za mashindano ya Club .sisi wenyewe huwa tukienda nje ya nchi wakati mwingine tunapata washabiki huko huko wa ugenini wanaokuwa nao wanataka wapinzani wao watoke.

Kikubwa ambacho kingesisitiizwa ni kuwa hawa watakao vaa jezi za timu pinzani basi wakae eneo lao na siyo kwenda kukaa kwenye mashabiki wa club nyingine ili kuepusha vurugu zinazoweza kutokea hasa kutoka kwa wale waliofungwa.na hivyo kufanya au kuchochea au kupelekea uharibifu wa miundombinu ya uwanjani kama vile kung'oa viti, kurushiana chupa za maji , kupigana ngumi na wakati mwingine kuharibu hata utulivu wa mchezo wenyewe na hata kupelekea vifo. Mpira ni uwekezaji kwa hiyo tuendelee kusisitiza na kujikita katika uwekezaji na kuvutia wawekezaji katika Secta ya michezo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Leo umezungumza kama mzalendo wa kweli, sio kila siku mapambio kuna wakti lazima tudadavue masuala ya ki-nchi kama hivi

Nje ya mada, Ila sasa mbona siku hizi mawasiliano yako huweki?😂

Pengine kuna ambao wanataka kutuma pongezi
 
Back
Top Bottom