Posho wanazojilipa Wakurugenzi na Mameneja huwa ni wizi mtupu! Bila kuzifuta posho hatutoboi

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Ukizunguka wizarani na kwenye mashirika kuna hawa watu wanaitwa wakurugenzi na mameneja (senior staff)

Hawa watu wameajiliwa kwa mishahara mikubwa sana average 2m ~8m kwa mwezi kama malipo ya mshahara katika majukumu yao!

Lakini cha ajabu kila jukumu la kazi huwa lina posho!
Mfano!
  1. Kuandaa report (lazima walipane posho na menu)
  2. Kupitia report (posho na menu)
  3. Kujadili mpango kazi (posho na menu)
  4. Kuchambua tenda (posho na menu) n.k
Tena wakati mwingine hata hawahudhulii vikao hivyo lakini maelekezo huwapa wasaidizi kwamba kila kikao lazima jina la MD au mkurugenzi lianze kwanza, posho kubwa hadi za 1m kwa kikao kimoja!

Sasa unajiuliza hizo posho za nini wakati wameajilia kwa kazi hiyo?

Haijulikani mshahara huwa wanalipwa wa nini kama kila jukumu la kikazi wanapeana posho!

Ukiachana na hayo bado wanapewa usafili na hela ya mafuta lakini hiyo haitoishi na madili wanapiga!

Value for money iko wapi hapo?

Nashauri Posho ziondolewe watu watumikie mishahara yao! Mbona watumishi wa chini wanaweza wao inakuwaje wanapeana posho za nini?

Pia iwepo na sheria ya kunyonga watu haraka, ipewe tenda kampuni ya uwakili ili kusaini unyongaji wa watumishi wabovu kwa niaba ya Rais ili iwe fundisho.

Haiwezekani Tukatoboa kwa style hii ya kujaza pipa halafu wengine wanatoboa chini maji yatoke!

HAKUNA NIDHAMU YA FEDHA HATA KITOGO
 
Naona umeandika ukiwa na hasira sana. Ni kweli haya mambo yanaleta hasira sana mpaka unafikiria hao watu walioyapanga haya walikuwa wanafikiriaje?

Kuna watumishi mishahara yao ni laki 5 - 6 na hawana posho wala per diem na ndio engine za maendeleo, watoa amri tu ofisini mishahara 2M - 15M bado posho kibao na marupurupu kibao.

Unakaa unafikiriiii weeeee unaona kabisa hii Nchi haijapata kuwa na kiongozi mwenye akili nzuri wote wanyonyajii tuuu.
 
Hizo wanaziita honoraria, kimsingi nchi hii wataalamu na wasomi wanalipwa mishahara kiduchu sana ukilinganisha na elimu zao. Kwa hiyo zikitokea hizo fursa za viposho ndo wanaponea hapo angalau kuishi maisha ya hadhi yao, vinginevyo wataishia kubanana uswahilini na kwenye daladala.
 
Mkuu hayo yapo siku nyingi sana na ndiyo inafilisi Serikali mpaka tunashindwa kunulia watoto wetu madawati. Hayo mahekalu watu wanajenga tena watumishi wa Serikali ni kwa njia hiyo. Nikifanya kazi serikalini miaka 30 iliyopita bosi wangu ambaye sasa ni marehemu alikuwa anawaandikia baadhi ya wafanyakazi imprest za safari bubu na mwisho wa siku wanampa yeye na kuwagawia kidogo. Hapo ni baada ya yeye kuchukua masurufu bubu ya mwezi mzima ya kwake.

Kwa jinsi hiyo pesa nyingi zinaliwa na wakubwa. Hii imekuwa laana kwa taifa na baada ya kutembelea baadhi ya nchi za kiafrika hayo ndiyo ninayoyaona. Wenzetu Ulaya kwa muda nimekaa kule hakuna upuzi kama huo na uwezi kupata pesa kiraisi hivyo na wana nidhamu ya pesa ya serikali ndiyo maana wamepiga hatua. Nimekuwa South Afrika na nikaona jinsi wazungu walivyoweka miundo mbinu nzuri lakini baada ya sisi kukabidhiwa nchi yanayoendelea mnayajua.

Zimbabwe baada ya sisi kuchukua nchi watu wamekuwa ombaomba. Ulevi, wizi, ushirikina, uvivu, kutaka utajiri wa haraka haraka bila kuufanyia kazi, uasherati/uzinzi na kutupelekea kuzaa watoto ovyo ovyo bila mpango na kuwa na vijana wasio na wazazi ambao mwisho wa siku wanakuwa majambazi au makahaba, kutokuwa na upendo katikati yetu na serikali yetu ni baadhi ya mambo ambayo yanaathiri sana maendeleo yetu.

Ukiwa mzalendo unataka kulinda mali za uma wanakumaliza. Hii ni laana au ni nini kwa hizi nchi zetu. Labda kizazi kitakachokuja kifanye big revolution ya kuondoa haya maovu yaliyo katika jamii yetu otherwise hatuendi popote na hatuwezi kutoboa bali tutaishia kulana sisi kwa sisi. Wewe unayeibia seriakli usifikiri kwamba upo salama sana maada damu yako siku moja itadaiwa kwenye geti lako. Siku moja majambazi watakuulia kwenye geti lako ukiwa kwenye gari lako la kifahari.

Hao ni wale watoto wangetakiwa waende shule au wapate waalimu wa kuwafundisha, serikali ikawa haina pesa kwa ajili ya wewe kutokuwa mwaminifu. Turidhike na mishara yetu au na kile kidogo tunachopata na kulinda pesa ya umma na Mungu atakubariki. Nimeishi kwa jinsi hiyo na sikupungukiwa na kitu chochote. Ninakumbuka tu kunyanyaswa na bosi wangu miaka hiyo baada ya kumkatalia kumpitishia imprest bubu. Ninawatakia Jumapili njema.
 
Naona umeandika ukiwa na hasira sana. Ni kweli haya mambo yanaleta hasira sana mpaka unafikiria hao watu walioyapanga haya walikuwa wanafikiriaje ??

Kuna watumishi mishahara yao ni laki 5 - 6 na hawana posho wala per diem na ndio engine za maendeleo, watoa amri tu ofisini mishahara 2M - 15M bado posho kibao na marupurupu kibao.

Unakaa unafikiriiii weeeee unaona kabisa hii Nchi haijapata kuwa na kiongozi mwenye akili nzuri wote wanyonyajii tuuu.
Duuuuuu
 
Ni kweli kabisa waliochini yao wanaumia sana kwa kazi
 
Hizo wanaziita honoraria, kimsingi nchi hii wataalamu na wasomi wanalipwa mishahara kiduchu sana ukilinganisha na elimu zao. Kwa hiyo zikitokea hizo fursa za viposho ndo wanaponea hapo angalau kuishi maisha ya hadhi yao, vinginevyo wataishia kubanana uswahilini na kwenye daladala..
Mkuu, umeandika jambo moja la maana sana hususan hapo uliposema "angalau kuishi maisha ya hadhi yao".

Mkuu, watu hatufanani umuhimu wetu katika taifa. Katika nchi yoyote ni lazima kuwe na kundi la "elites" watakaokuwa wanawaongoza wenzao ndio maana wengi wao wanakaa Oysterbay na Masaki. Hao jamaa (Wakurugenzi na Mameneja) ni assets sana kwa taifa.

Watu hatufanani hata siku moja.
 
Bongo watu hawa value kabisa taaluma za watu......si ajabu impact ya wataalamu wetu haionekani kwa hizi dharau, eti mil. 2 ndo mtu anaona mtaalamu kalipwa pesa ndefu....
 
Back
Top Bottom