Posho na Mishahara ya wabunge...

 
Tuwe wakweli Mh Mbowe hajawa mpole baada ya kusema kuwa wamekopa posho ila amefafanunua vizuri kuwa posho hizo zinapatika pindi yu mtu anapo ingia kwenye kikao,kwahiyo ameshangaa ni kwa jinsi gani mtu atakopa hiyo sitting allowance.
Kuhusu posho zipo ambazo huwa siyo fixed amount inategemea kwahiyo haiwezekani kupewa mkopo wowote kwa allowance ambazo hazionyeshwi kwenye kwenye karatasi yako ya mshara,ikiwemo ile ya safari nayinginezo za namna hiyo.
Bado ukweli nikwamba hawa jamaa wanacho fanya siyo sahihi maana posho zao za siku karibia zinalingana na mshahara wa mfanyakazi wa serikari kwa mwezi mzima.Mh Lukuvi anachosema kuwa nao wameisha liona hilo,ila kilicho nifurahisha Mh Mbowe amamwambia kuwa mipango yenu hmmeshindwa kiweka kivitendo likiwemo la kutumia magari ya kifahari.
 
Endelea ku-download akili yako mpaka ikiwa full nadhani ndio utafahamu, usipayuke tu wewe kila kitu kinachoisema Chadema unaleta Controversy, ungeangalia kipindi nadhani usinge kurupuka eti hakuna bank inayotoa mikopo, Kamanda wako wa Kihindi Mbowe kabanananishwa na Lukuvi kaambiwa wewe umeishakopo benk milioni 200 umedhaminiwa na katibu wa bunge, Mbowe hana kenua meno tu, anasema tuongelee posho za serikali tuachane na za bunge, unataka kumjibia mchagga mwenzako umechemka
 
There are currently 150 users browsing this thread. (43 members and 107 guests)
 

mbowe hawezi kubananishwa na mtu wa uwezo wa lukuvi wewe.. hivi wewe unachoshabikia ni nini?
 
Mimi kinachonishangaza ni kuwa kila linapotokea jambo tata ambalo upinzani unalishikia kidedea lazima January Makamba aibuke na kujidai aidha analijua sana au ana solution mkononi! Hili suala la posho yeye anataka kutuaminisha kuwa ilikuwa ni agenda ya CCm na tayari ilishakuwemo kwenye mpango wa maendeleo wa miaka 5!
January acha kuwa msemaji wa CCM indirect, ulitoka Ikulu muda mrefu sahau ya Ikulu.
 
Mimi ninavyofahamu mtu uwezi kukopa posho bali unakopa mshahara.

Je huko Tanzania kuna sheria mpya iliyotungwa kuhusu watu kuweza kukopa posho.

Naomba tujuzane sheria hiyo na ya mwaka gani?
 
Inaonyesha watu wa magamba elimu zao zina matege,Lukuvi anajibu mambo mazito kwa kutumia akili au?Na mnaoshabikia huu upupu wa
lukuvi nina wasiwasi na nyie kama kweli ni Gt,ni benki gani inayomkopesha mtu kwa perdiem?????????tuambiane ili na sisi tukakope basi
 
Kweli akili yako imejaa masizi, utaki kukubali kama wabunge wachadema waishakopa benki akiwemo Mbowe na Zitto, wengine wamechukuwa milioni 200 wengine milioni 150. Mdhamini wao ni katibu wa bunge watakuwa wanakatwa Sitting allowance ndio inapelekwa benki. Sasa wewe unakataa Mwenyekiti wako kakubali na kaishachukuwa na huo mkopo wewe Chadema-kata unapinga
 
mbowe hawezi kubananishwa na mtu wa uwezo wa lukuvi wewe.. hivi wewe unachoshabikia ni nini?
Wabunge wa Chadema wanafiki wanapinga posho kumbe wameishaichukulia mikopo bungeni, kuna wengine wamechukuwa milioni 200 wengine milioni 150, hiyo tofauti na milioni 90 mkopo wa gari
 
Wakuu,posho ya mafuta nadhani ikpo constant au guaranteed kiaina fulani for five years,
Kama jamaa amesema ofisi ya katibu wa bunge imemdhamini mkopo kwa makubaliano ya posho kwa kupitia benki au akaunti yoyoite ya bunge,msikatae.
Bali tuwaulize wabunge hapa jamvini kama hii tuhuma ni kweli......tusiwajibie.
Tuache uchama,kama tunataka hii kitu iondoke itabidi tuwe honest kwa watu wa vijijini wanaosota,tuwakabe hawa wabunge hapa bila ushabiki,tuombe wajibu tuhuma.
 
Posho za vikao vya bodi za wakurugenzi kwenye taasisi na mashirika ya UMMA ni balaa. Sio chini laki tano kwa kikao kimoja hata kama watakutana kwa nusu saa. Mbaya zaidi bodi hiz hazina manufaa wala tija yoyote kwenye taasisi hizi

Hivi Michango yetu ya NSSF na PPF, Hakuna Jinsi tunaweza kui manage wenyewe kama ka Saccos fulani?
 
Kamanda wako wa Kihindi Mbowe mbona kashindwa kukanusha kaambiwa na Lukuvi wewe si umechukuwa mkopo tayari. Anang'aa sharubu tu
 
Kama vyombo vya habari vilimnukuu vizuri Mh Spika, posho ipo kisheria. Kama ipo kisheria ni haki yao wabunge kuipata hadi hapo sheria hii ya kijinga itakapofutwa. Kuikopa posho pia inawezekana kwa ninavyowafahamu wanasiasa wetu. Siasa kwao sio ajira tu, ni uwekezaji wa nguvu.
 
kwanza wamejua leo bajeti ya chadema inasomwa wamekata umeme makusudi hilo linajulikana mbona juzi awajakata jana pia kwa nini leo? Ila siku zao za hesabika
 
Wabunge wa Chadema wanafiki wanapinga posho kumbe wameishaichukulia mikopo bungeni, kuna wengine wamechukuwa milioni 200 wengine milioni 150, hiyo tofauti na milioni 90 mkopo wa gari
Tuseme mbunge kaugua kikao chote cha bunge huo mkopo analipaje?
Tuwe tunafikiria wakati mwingine bana sio ushabiki tu!
 
Kama Opposition imetoa hoja nzuri na CCM ikaona ni jambo jema sana.. na wao kama Majority wakaona waanze kulitekeleza kwa nini tusiwape credit hata kwa hili dogo? Wangeamua kuwa kichwa ngumu i bet wangeshambuliwa zaidi.!! Tukubali tu kuwa hizi posho ni kutumia vibaya hea za walipa kodi.
Vyama vya siasa vita-play politics hapa lakini ukweli utabaki pale pale.. hizi posho ni ufujaji! Ziondolewe tu.. maybe watu watajiuliza mara mbili kabla ya kuacha "uprofesa" Vyuoni na kukimbilia bungeni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…