Unafahamu suala linalogusa masilahi binafsi ni gumu kulitekeleza kichama, lakini ni gumu kuacha kulitekeleza kama kutofanya hivyo unakizana na dhana ya kisiasa unayoihubiri. Wachache watamwangalia na kumchambua Zito wengine wataangalia dhana hii na msimamo wa chama. Hata mimi ningependa na nataka uwe ni uamuzi wa kitaasisi kwa maana ya CDM lakini kama chama hakina kauli moja sitazuia uamuzi wa mtu mmoja moja kukataa sitting allowance.
Ndugu wana Jamii forum hivi unapokuwa kwenye nchi yako ya Tanzania ambayo bajeti yake ni kubwa kuliko mapato yake kwa asilimia zaidi ya 50, na mapato yake ni asilimia 75 ya mahitaji ya matumizi yake ya kawaida kwa mwaka, halafu kunakuwa na hela ambazo zinamlipa mtu kwa kukaa kwa muda mrefu, unategemea nini? Serikali yeti ni ya uwema wa kulipa watu kwa kukaa? Chonde sana sana wabunge walipwe DSAs na si sitting allowance. Hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma na Mbunge anayesimamia kidete kupinga sitting allowance yupo na wapiga kura wake. Kama tutapambana kuokoa kiasi hiki cha hela tutakua tumeokoa watanzania wangapi. Nataka kuona Rais anatofautiana na Wabunge wa Chama chake, nataka kuona waziri mkuu anakaa upande wa umma, nataka kuona tunaanza kupunguza utegemezi wa bajeti kwa kuanza na Wabunge na viongozi wa Serikali Billioni mia saba kwa kulipa watanzania wenzetu kwa kukaa ni dhambi isiyosameheka
Wenye uchungu na nchi hii tumekataa vitu hivi huko nyuma, tunakataa leo na tutaendelea kukataa, hoja si nani anaisimamia, au wangapi wanaikataa hoja hii bungeni hoja hapa ni kwa masilahi ya nani na kwa mantiki ipi?
Nakubaliana na mwenyekiti alivyosema jana kuwa hii ni hoja ya chama basi na iwe hivyo tunapenda kuona akiwaongoza wabunge wake waitekeleze mara moja.
Hiyo ni ndowano ya Chadema kwa CCM itumieni, lazima watakuja upande wenu tu hawana jinsi, wanalazimika kuingia wazimawazima kwenye chambo hicho, hiyo ndiyo tiba na usalama wao wakiikwepa wataingia kwenye chambo isiyo na huruma ambayo imeshikiliwa na isikariot na wataadhibiwa ipasavyo.