POSHO: Bunge lamjibu Zitto Kabwe; atoa msimamo wake

Wazo la Zitto ni zuri lakini CCM wameligeuza propaganda. Lakini hata hivyo, Zito amefanikiwa kuibua mjadala wa jinsi serikali inavyopoteza hela nyingi kwenye posho za vikao. Kwa mfano tunaambiwa ukiondoa posho kwa wafanyakazi wote wa serikali unapata bilioni 900. Hizi sio pesa kidogo. Tunaweza kuijenga ile reli ya kwenda Arusha tukasafiri kwa masaa 5!
 
kwa kweli mie sijaona mantiki ya mbunge kukataa posho, ingekuwa anachallenge kiwango cha hizo poso, ningeelewa. mfano mimi kazi zangu ni za kusafiri sana na mshahara wangu huwezi hata gharama za siku mbili hotelini, sasa usiponipa posho nitawezaje kutekeleza majukumu yangu kikamilifu? najua wakati mwingine posho ni kubwa hasa ukulinganisha na tija inayopatikana, lakini siyo uiondoe bali ikibidi uangalie uwezekano wa kupunguza!
Nakushauri uwe unazisoma threads kwa makini kabla hujajibu.
 
Spika ni CCM, anajua kabisa jambo analotaka kulifanya Zitto litakuwa ni mkuki kwa CCM. Sasa wewe unategemea angefanyaje? Sijawahi kumwona spika Boga kama huyu!
ni


ni!
 
Zitto alifanya move mzuri. Tatizo tu ni ubinafsi. Suala hili liko kwenye mpangowa chama. Wamelihubiri kwenye mikutano yao mingi, na kama mnakumbuka vizuri alilianza Dk. Slaa akiwa mbunge. Pia limo kwenye bajeti yao mbadala ya fedha. Alikuwa na haraka gani kuandika barua peke yake, hata kabla hiyo bajeti hajaisoma (mwenyewe) wiki ijayo? Na atueleza hiyo taasisi ya KDI ni ya nani kama si yake mwwnyewe?

..hivi anaelipwa posho ni chadema au mh. mbunge? ubinafsi uko wapi? kuna tatizo gn Mh. Zitto akiandika barua ya kukataa posho aliyopewa yeye? hata kama suala liliongelewa na chama, at the end posho anapewa mbunge, utasema nini kama wabunge baadhi wa chadema wamechukua posho? acha lawama zisizokuwa na msingi bwn!
Hata kama KDI ni yake bt km imesajiliwa na ina uongozi kulingana na sheria za nchi, tatizo nini hapo?
 
Naanza kuona mafanikio katika siasa za Tanzania na hapo ndipo tutaanza kujua nani yupo kwa manufaa ya watanzania na nani yupo kwa ajili ya tumbo lake, tumewasikia waropokaji Hamad Rashid, mkulo na Ndungai, hawa tumewajua kwamba ni wanasiasa masilahi, Zito sio kama kakurupuka ila wamemfanya kama chambo kwani mshkaji ana comf katika kufanya maamuzi magumu, rejea suala la Buzwagi so tuendako tutegemee wanasiasa wa ukweli ambao watakuwa hawafuati hizo sitting allowance. Viva Tanzania Politics
 
If I have to say the way I think may be I can't finish all today. Swala Watanzania ni 'Posho za wabunge na wafanyakazi wa taasisi wengine wa serikali' Hii ndio mifano dhahiri ya kikwete na ccm. Tunapoona wahuni wa ccm wanatetea hili swala la posho na ujinga mwingine wa policies za ccm ni vizuri tushikane mikono kwa pamoja. Kinachowafanya hawa wahuni wakubali au kuendelea kupokea hizi posho ni nini? Whats's your responsibilities then kama unalipwa unapokaa kwenye vikao au mnapokutana? Why are these ccm criminals allowed to receive mishahara too? Hebu tuangalie kitu gani tunazungumzia hapa
Habari kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM, zinasema kuwa pamoja na mambo mengine, wabunge wa chama hicho tawala wameungana kupinga kufutwa posho zao.
Kwa sasa wabunge wote wanalipwa per diem ya sh 80,000 na posho za vikao (seating allowance) ya sh 70,000, hivyo kuweka kibindoni sh 150,000 kila siku wawapo vikaoni.
Bunge njia panda

Lets compare na salaries za larget economy in the world:
peaker of the
House
= $223,500
House and Senate Majority and Minority Leaders = $193,400
House/Senate Member & Delegates = $174,000
Read more: Answers.com - How much do members of Congress get paid

Tukiangalia hapo juu tunaona gharama kiasi gani wanazitetea (kwa siku sh. 150,000). Hapa hatujazungumzia mishahara yao na gharama zingine kama hizi hapa:
1. Gharama za wafanyakazi wa bunge
2. Gharama za vyakula wakiwa kwenye vikao
3. Gharama za kukaa mahotelini
4. Gharama za usafiri
5. Gharama za ulinzi

Huu uzembe na ignorance ya ccm this is what we refer to a 'source of poverty in Tanzania and Africa in general' sisi kama watanzania we again seem very naive to remove these people from ruing our country. Tunajua wazi kwamba budget za ccm is not about policies and fiscal responsibilities but it's about posho, corruptions and stealing from people. I am confident saying this sisi watanzania na chadema we need to focus on removing ccm period and nothing less. Vitu muhimu tunaacha kuzungumzia na kubaki kumwangalia Mkullo, Ndulu na kikwete wakiandika vitabu vya uongo. Where are following policies kwenye budget:
1. Ongezeko la ajira kwa Watanzania hasa vijana?
2. Mipango to increase the value of Tanzania currency? (i.e. trade, interest rate)
3. Mipango to improve education and heatthcare systems
4. Mipango to reduce national debt?
5. Mipango to increase and improve local investments?
6. Where's constitution of Tanzania?

By the way, Zitto najua una-account JF, what you did is terrible as aparty leader. I don't know what were you thinking, anyway I will contact you other way.... just a shame again. This is a reason why I think Zitto politically you are killing yourself. Sisi kama watanzania tuzingatie hapa hizi barua na exchange za Zitto despite ni mbaya hivi but the big picture tutapoteza muda mwingi kusoma hizo notes na kumwacha mwizi Mkullo na ccm wanapitisha hu utumbo machoni mwetu.
 
Hivi kwanini Rostam anapewa posho?...au mbunge wa dodoma mjini?......duh,hii naimind sana!
 
Mimi naona Mh. Zitto is very right, yeye alikuwa anaomba pesa zipelekwe kule jimboni kwake, Mh. Mbowe tayari katangaza ni msimamo wa chama, Zitto amesema katu hatopokeaq pesa hiyo ni bora wabaki nayo wao, mimi na subiri kuona pia sheria inayosemwa na katibu wa bunge kuwa ni lazima mbunge apewe fedha yeye mwenyewe itakavyofanya kazi,
Si sote tunajua sheria ukienda against nayo lazima ichukue mkondo wake ? najua hiyo sheria haipo, hapo ni kucheza ngoma ya mdumange , Nape, Mkullo hiyo ngoma mtaicheza sana
 
Acha kuwa mbayuwayu wewe, lete data za mafao ya wabunge wa tanzania ukilinganisha na nchi za zingine za east africa, acheni kutumiwa kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa

Tanzania haiwezi kufanya move fulani eti kwa kuwa nchi nyingine za EAC zimefanya hivi na sisi tuige wao. Kwa maana hiyo basi cabinet ya bongo unataka iwe na mawaziri 90 kama ile ya Museveni kwa kuwa Uganda wana cabinet ministers 90?
Where is your genius brain?
 

Kwa mtazamo wangu hili la Zitto kukataa kabisa siliungi mkono, nilipenda approach yake ya kukataa na kupeleka KDI kwa sababu impact yake ingekuwa direct yaani ni kama mtu unapofanya saving kisha ukaipeleka sehemu fulani.
Paamoja na hayo lakini nakupongeza sana kwa msimamo wako ambao unatakiwa kuigwa na wabunge wote wa CDM.
Mkuu hapo Zitto kafanya sawa tu kwani ni siasa na anataka kuwaona watafanya nini sasa. Hamna sababu ya bunge kukataa kuweka hizo hela kwenye account ya maendeleo ya jimbo lake labda kama posho zote lazima wapewe cash mkononi.
 
Zitto hawa ccm huwa hawana aibu,nakumbuka walipewa 400bilioni toka global fund Bill clinton foundation kwa ajili ya aids na malaria,lakini walipeleka MSD bilioni 40 tuu mwaka mzima.Zingite ziliishia kutengeneza vipeperushi,fulana,semina na warsha bagamoyo kupitia TACAIDS.huku wakiwaacha wagonjwa bila lishe bali kusisitiza dawa za kurefusha maisha na vyandarua.Hapo wameshaanza kupiga mahesabu jinsi ya kuila hiyo posho yako!!!
 
What does this mean? Au alifikiri watu wanabeep walipokuwa wanataka posho ziondolewe?

Posho-Za-Vikao-Majibu-Ya-Bunge.jpg

Posho-Za-Vikao-Mhe-Zitto-Kabwe-II.jpg

Kabwe sikuelewi,dizain unazitaka hizo hela ila unazichungulia hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa;;lets c the batle'
 
VIP MBOWE NA WACHAGA WENGINE CHAMANI WANAZITAKA HIZO POSHO AU??SIJASIKIA MSIMAMO WA TYCOON NDESA PESA NA MABINTI ZAKE

waambieni wafunguke basi tujue moja
 
VIP MBOWE NA WACHAGA WENGINE CHAMANI WANAZITAKA HIZO POSHO AU??SIJASIKIA MSIMAMO WA TYCOON NDESA PESA NA MABINTI ZAKE

waambieni wafunguke basi tujue moja
 
VIP MBOWE NA WACHAGA WENGINE CHAMANI WANAZITAKA HIZO POSHO AU??SIJASIKIA MSIMAMO WA TYCOON NDESA PESA NA MABINTI ZAKE

waambieni wafunguke basi tujue moja
Mtu anayetawaliwa na ukabila na kutumia kabila la mtu huwa nampuuza kabisa, Hivi hakuna namna nyingine ya kujua msimamo wa Ndesamburo na Lucy Owenya au Mbowe bila kutaja kabila? Nchi hii bwana!
 
VIP MBOWE NA WACHAGA WENGINE CHAMANI WANAZITAKA HIZO POSHO AU??SIJASIKIA MSIMAMO WA TYCOON NDESA PESA NA MABINTI ZAKE

waambieni wafunguke basi tujue moja

umejoin JF just 3 days ago then unaleta pumba hizi? Ndio vijana wa Nape mliotumwa kuja jamivini
 
By the way, Zitto najua una-account JF, what you did is terrible as aparty leader. I don't know what were you thinking, anyway I will contact you other way.... just a shame again. This is a reason why I think Zitto politically you are killing yourself. Sisi kama watanzania tuzingatie hapa hizi barua na exchange za Zitto despite ni mbaya hivi but the big picture tutapoteza muda mwingi kusoma hizo notes na kumwacha mwizi Mkullo na ccm wanapitisha hu utumbo machoni mwetu.

I beg to differ with your assesment of HON ZiTTO. Ukisikia ufisadi serikalini ndiyo huo KULIPANA STAHILI AMBAZO HAZINA TIJA KWA KUWA TU MNAWEZA KUJITUNGIA NA KUAMUA TARATIBU ZA KUFANYA HIVYO.

Kwa nini ni ufisadi ni kwa sababu tatu

1. Mshahara wanaolipwa kwa mwezi umezingatia stahili na uzito wa kazi kwa hiyo malipo ya ziada yanatakiwa yawe ambayo kweli yanaongeza output ya kwenye malengo ya kazi ya kawaida ya mtumishi na kweli hiyo ziada ipimike na ilipwe kwa uziada wake.

2. Kwa sababu wakubwa wameamua walipwe mara mbili kwa kazi ile ile haihalilishi kuwa huo sio wizi au ufisadi.

3. Hiyo kwa undani ni kukiri kuwa mshahara hautoshi. Ni kweli hautoshi kwa sababu hakuna tija. Tumeua dhana na utamaduni wa malipo kwa kazi inayopimika. Sababu ni kuwa hakuna mtumishi ambaye kazi yake inalipwa kwa kazi inayopimika kwa sababu kazi kwa sasa hivi si output bali ni fursa ya kulipwa tu, uwe mshahara au posho ili mradi mtu yuko kwenye payroll. Kwenye kampuni binafsi hasa za kimataifa huna output huna malipo. Na ndiyo maana wana maendeleo.

Ndiyo maana serikali hii hata siku moja haitasema mpango wetu wa kazi ambao tumepangia bajeti hii utapimwa na vigezo hivi na hivi. Mana yake hawana uhalali wa kusema tumeendelea kwa sababu hatukuanza kukubaliana vigezo na viashiria vya maendeleo tunayoyataka.

Zito na CDM wana moral reason kuwa posho ni malipo ya mara ya pili (wizi) kwa kazi ambayo inalipwa kwa mshahara. Morally ni kukataa malipo hayo kabisa kwa sababu ya kushitakiwa na dhamiri kuwa si malipo halali. Lakini kwa ubadhilifu wa serikali ya CCM ndiyo kazi kubwa wanayofanya kulipana kijanja janja tu bila output. Lakini hiyo pesa ni nyingi sana inaweza kupunguza au kuondoa kabisa malimbikizo ya malipo halali ya watu kama walimu.

Huu mkakati wa CDM unahitaji wao kujitoa mhanga kwa sababu hakuna isiyehitaji hela. Hela haitoshi ila lengo hapa ni kuwabana wabadhilifu siyo tu kwenye suala la hizo posho bali utaratibu mzima wa kuhalalisha wizi kwa sababu wana uwezo na fursa ya kuamua hivyo. Sisi wakulima hatuna fursa ya kusema tulipwe kiasi fulani kwa mazao yetu. Hatuna chombo hicho cha maamuzi. Kwa hiyo kwa wawakilishi wetu kitendo hicho ni dalili ya nje ya nia yao njema kukataa ufisadi ambao unaohalalishwa kwa maamuzi na taratibu za kisheria.

Naomba wenzangu mnaosoma hapa mjue kuwa siyo mabilion kama ya EPA yanayofisadiwa tu, kuna matrilioni yanayoliwa kidogo kidogo na ukiyajumlisha unaweza kuzimia. Nayo ni kama hizo posho na mengine tanaweza kutaja hapa. Mfano ni kama wafanyakazi wanaotokana na nyadhifa za kisiasa kukaa mahoteni. Huo ndio ufisadi unaohalalishwa kisheria kwa maamuzi ya kipuuzi ya CCM na serikali yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom