Pongezi kwa wauza maziwa wa Chato stendi

kyarluta

Member
Oct 28, 2019
24
12
Nawapongeza akina mama na vijana wajasiriamali wa stendi ya Chato. Napongeza hasa wale wanaouza maziwa.

Ni hivi majuzi 19/4/2020, nilipita na basi Fikosh nikitokea Mwanza kuelekea Bukoba, muda wa saa 6 mchana. Nilishawishika kununua maziwa ya mgando baada ya kuwa na hamu nayo. Yalikuwa yako kwenye chupa kubwa ya maji ya lita moja na nusu. Maziwa hayo nilikuja kuyanywa saa nne usiku.

Ama kwa hakika maziwa hayo yalikuwa matamu, hayakuwa yamekatika kwa maana ya kujitenga na maji, hayakuwa machachu na harufu yake ilikuwa original. Hayakuniumiza tumbo. PONGEZI SANA.

Nawashauri wauza maziwa wa Bukoba stendi, Karagwe Kihanga ( kwa Wachina) Kyaka na wale wa Muhoro (njia ya Lindi) kuwaiga wajasiriamali hawa wa Chato stendi.

Kwa wana Chato, kamwe msije mkashawishika kuongeza maji, wala kugandisha maziwa kwa kulazimisha na chachu ili yagande haraka. Mtaharibu soko la maziwa yenu.
 
Wangefungasha vizuri wangeuza sana.. Hiyo ni fursa nzuri maana wengi wetu tunapenda mtindi kwa Kunywa au kama mboga
 
Wasukuma wanasifiana wenyewe kwa
Wenyewe, hyo michupa inakojolewa
Na chokoraa alaf unawekewa maziwa
Unakunywa?

Ndo maana mnakua wa mwisho
Mwisho tu

stidy
 
Iyo chupa ndo zile wanazo okota na kuzi suuza tu na maji kwenye ka ndoo
 
Nina wasiwasi wewe ni Uncle.. Mbona ukiwa Dar hatuoni chapua kutokea, Chato?
 
Back
Top Bottom