Kero ya wauza maziwa Arusha kuweka maji na unga wa ngano

Habari Leo

New Member
Jun 18, 2023
2
1
Kama kichwa kinavyo jieleza. Hili ni janga la muda mrefu na hali hii inazidi kukomaa hali inayopelekea maziwa kutokuaminika kabisa.

Wauzaji kuanzia wafugaji wanao kamua maziwa hadi wenye maduka wanaouza rejareja, wengi wao wanaweka maji ili maziwa yawe mengi na kisha kuweka unga wa ngano ili kuyafanya yaendelee kuonekana mazito.

Hali hii si nzuri kwa afya hasa kwa watoto wadogo ambao huyatumia kwa takriban kila siku ili yawawezeshe kukua vizuri, badala yake wanadhurika.

Mamlaka husuka hakikisheni mnalifanyia kazi hili si kwa Arusha tu, hata na mikoa mingine wanao fanya hivyo(Arusha imekithiri), vile vile toeni onyo na adhabu kali kwa wauzaji wanaofanya hivyo.

Nawasilisha.
 
Si bora hao wanaoweka maji, wengine wananunua yale ya unga, wanatia maji ya kutosha wanachanganya na maziwa kiduchu.
Unakuta chuma nyeupe pee unaingia mkenge.
 
Back
Top Bottom