Ufugaji wa Punda kwa ajili ya Maziwa

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,915
Watu wengi hasa hapa Bongo tunajua kazi ya punda ni kubeba mizigo au hata kwenda Kulima, na sasa pia ile ya kuchinjwa na wachina.

Ila jambo tusilo lijua ni kwamba Punda pia anatoa maziwa au anaweza fugwa kwa ajili ya Maziwa kama ilivyo mifugo mingine.

Maziwa ya Punda yanaaminika kwamba ndiyo maziwa yanayo karibiana au yako sawa na ya binadamua kwa kiwango kikubwa sana kuliko aina nyingine yeyote ya maziwa. Na kwa jamii hasa huko Asia na Ulaya Mashariki ambako wanafuga punda pia waliwa wanatumia maziwa ya punda kulishia watoto yatima walio fiwa na mama zao wakiwa bado wachanga.

Inaaminika pia sina hakika asilimia 100 kwamba Cleopatra mwanamke mrembo kuwahi kuumbwa sina hakika pia, alikuwa akioga maziwa ya punda, yaani Malikia Cleopatra alikuwa haogei maji bali maziwa tena ya punda.

Ukiachana na maziwa ya punda kuwa karibu kabisa na ya binadamu ila pia ni moja ya tiba nzuri sana ya ngozi, na Duniani hukko kuna products za ngozi zinazo tokana na maziwa ya punda.

Ila pia the most expensive Ghee Duniani ni ya maziwa ya punda, unaweza google.

Hivyo tunaweza wekeza pia kwenye maziwa ya punda hata kama sio kunywa basi kwa ajili ya product za ngozi,jasa sabuni, ila pia kwenye kunywa, maziwa yake ni tiba.

Swala la anakamuliwa vipi nazani ni mafunzo tu kuanzia awali, punda akifundishwa vyema hana shida kabisa.
FB_IMG_1700675635364.jpg
FB_IMG_1700675686595.jpg
 
Anzisha biashara ya maziwa ya binadamu. Sababu maziwa ya punda ni Kwa ajili ya mtoto wa punda. Huoni aibu mtu mzima kumdhulumu mtoto chakula.
 
Back
Top Bottom