Mkuu hawa baadhi ya member humu jamii forum ndo wanaizamisha Chadema kabisa maana wana baadhi sifa zifuatazo,
i) Kejeli, kitu chochote ambacho kinafanya na waislam basi hata kama kina manufaa wao wanakejeli
i) Dharau, kwa mtazamo wao wanadhani kwamba wao ndio binadamu wenye akili kwa maana kwamba kingine chochote konachofanywa na mtu mwingine hususani muislam basi cha kwanza wao ni kudharau
iii) Matusi, nadhani hapa sihitaji kuelezea sana maana ukitaka ushahidi fungua thread yoyote inayohusu mtu yeyote mwenye itikadi ya kiislam utashuhudia
iv) Wanajua sana, wao ndio kila kitu hakuna mwingine
Sasa mimi nilikuwa nina ushauri ufuatao
Tanzania ni nchi kubwa sana ambayo population yake kubwz iko vijijini na ndio hao wapiga kura wengi sasa kama kila kukicha kazi kuwaponda waislam na kuwadharau kwa kila jambo wanalolifanya unategemea uingie ikulu kweli?
Hata kama mtakuja munitukane na mimi hapa lakini nasema kwa style hii Chadema hatochukua hii inchi kwa kutegemea wafuasi wenye sifa tajwa hapo juu.
Na wakumbuke wengi wao wanaofanya hayo matukio tajwa hapo juu huwa hawapigi kura mfano mwaka 2010 nilikuwa msimamizi katika moja ya kotuo cha uchaguzi, kati ya wapiga kura 400 waliofika ni 150 tu na wengi wao wakiwa vyama vingine tofauti na Chadema na wakati huo huo wafuasi wake walikuwa wanakelele sana mtaani.
Ni hayo tuu, kwa sasa!
kituo cha uchaguzi