PreGE2025 Polisi yazuia Mkutano wa John Heche na Waandishi wa Habari uliokuwa ufanyike leo Juni 17, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Jeshi la Polisi limezuia kufanyika Mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche na waandishi wa habari ulokuwa ufanyike leo Juni 17, 2025 katika hotel ya Seashells Millennium Hotel, iliyopo Makumbusho Dar es salaam, kwa maelezo kwamba chama hicho kimezuiwa na Mahakama kufanya shughuli za Siasa.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Brenda Rupia amesema wa wakati wakiandaa kwa mkutano huo, walifika watu waliojitambulisha kuwa ni maofisa wa polisi na kuzuia ufifanyike.

"Walikuja maofisa wa polisi wakasema CHADEMA imezuiwa kufanya kazi hivyo tusifanye mkutano. Lakini huu mkutano nimeuitisha mimi kama Brenda, sio wa chama," amesema.

Alipoulizwa kuhusu zuio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amehoji, "wanalalamika nini? Basi tunafuatilia wasichokijua na ambacho wanakilalamikia."

1750153188526.png

Taarifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleoa (CHADEMA)

Jeshi la Polisi limezingira hotel ya Seashells Millennium Hotel na kuwaamuru waandishi wa habari kuondoka, Makamu Mwenyekiti - Tanganyika John Heche alitarajia kufanya Mkutano na Waandishi wa Habari hotelini hapo leo tarehe 17 Juni 2025. Jeshi hilo limedai kuwa Chadema wamezuiliwa kujishughulisha na shughuli yoyote ya kisiasa.

Screenshot 2025-06-17 124219.png

POSTPONED (PP): John Heche anazungumza na Watanzania kupitia Waandishi wa Habari, Dar es Salaam, Julai 17, 2025

Polisi alivamia press na kuamuru Waandishi wa Habari wazime Kamera zote.

Screenshot 2025-06-17 120247.png
 
Jeshi la Polisi limezuia kufanyika Mkutano wa CHADEMA na waandishi wa habari ulokuwa ufanyike leo Juni 17,2025 katika hotel ya Seashells Millennium Hotel, iliyopo Makumbusho Dar es salaam, kwa maelezo kwamba chama hicho kimezuiwa na Mahakama kufanya shughuli za Siasa.
Vip kuhusu freedom of speech and expression, hiyo haiwezikani kuzuiliwa na mahakama, yoyote duniani hata mfungwa anasruhusiwa kuongea opinion zake......police wa Tanzania hawajui sheria.
 
eeeh
 
PoliCCM wana akili za kijinga sana aisee!
 
Vip kuhusu freedom of speech and expression, hiyo haiwezikani kuzuiliwa na mahakama, yoyote duniani hata mfungwa anasruhusiwa kuongea opinion zake......police wa Tanzania hawajui sheria.
Wao CHADEMA wamesajilliwa kupitia msajili wa vyama vya siasa

Jina la CHADEMA limeingiaje hapo? Wakati CHADEMA imefungiwa shughuli zake

Wakirudia tena msajili afute CHADEMA
 
Jeshi la Polisi limezuia kufanyika Mkutano wa CHADEMA na waandishi wa habari ulokuwa ufanyike leo Juni 17,2025 katika hotel ya Seashells Millennium Hotel, iliyopo Makumbusho Dar es salaam, kwa maelezo kwamba chama hicho kimezuiwa na Mahakama kufanya shughuli za Siasa.
Hiki chama kinapenda Kiki sana. Kinajua kama kimepogwa marufuku na mahakama kufanya shughuli za siasa lakini kinaitosha mkutano na waandishi wa habari. Hii ni dharau na kiburi kwa mahakama. Msajili wa vyama vya siasa yuko kimya inashangaza sana.
 
Afute usajili wa CHADEMA it is not a big deal kama hawatii mahakama
 
Wao CHADEMA wamesajilliwa kupitia msajili wa vyama vya siasa

Jina la CHADEMA limeingiaje hapo? Wakati CHADEMA imefungiwa shughuli zake

Wakirudia tena msajili afute CHADEMA
Hawajazuiliwa kuongea na kufikishwa expression yao kuhusu hilo zuio, freedom of speech ni fundamental human right huwezi kuikataza labda uwe mpumbavu, hata condemned anae enda kunyongwa anapewa na fasi kuangea na watu wake kasbla ya kunyongwa, tatizo hapa Tz shule ndogo sana kwa viongozi weti
 
e3bcd1ba-d7a5-423f-bb13-b83bb5130903.jpg
Jeshi la Polisi limezuia kufanyika Mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche na waandishi wa habari ulokuwa ufanyike leo Juni 17, 2025 katika hotel ya Seashells Millennium Hotel, iliyopo Makumbusho Dar es salaam, kwa maelezo kwamba chama hicho kimezuiwa na Mahakama kufanya shughuli za Siasa.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Brenda Rupia amesema wa wakati wakiandaa kwa mkutano huo, walifika watu waliojitambulisha kuwa ni maofisa wa polisi na kuzuia ufifanyike.

“Walikuja maofisa wa polisi wakasema CHADEMA imezuiwa kufanya kazi hivyo tusifanye mkutano. Lakini huu mkutano nimeuitisha mimi kama Brenda, sio wa chama,” amesema.

Alipoulizwa kuhusu zuio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amehoji, “wanalalamika nini? Basi tunafuatilia wasichokijua na ambacho wanakilalamikia.”

Gton_vqacAAlujq.jpg

Jeshi la Polisi limezuia kufanyika Mkutano wa CHADEMA na waandishi wa habari ulokuwa ufanyike leo Juni 17,2025 katika hotel ya Seashells Millennium Hotel, iliyopo Makumbusho Dar es salaam, kwa maelezo kwamba chama hicho kimezuiwa na Mahakama kufanya shughuli za Siasa.

POSTPONED (PP): John Heche anazungumza na Watanzania kupitia Waandishi wa Habari, Dar es Salaam, Julai 17, 2025
Laiti police wangejua pesa zinavyotafunwa huko CCM, kwenye mawizara na kwenye Taasis, wangepambania maslahi yao au kusapoti wanao wasemea, serikali wanayoipambania haina habari nao kimsingi polisi wanaishobokea Serikali, kinachofanyika IGP anapewa madili afu anatoa oda kwa police vichwa maji wao wanatekeleza oda, wakati IGP anakula maisha, endeleeni kutumika kama kondomu huku mishahara na posho zenu vikiwa duni.
 
Back
Top Bottom