Polisi yamwachia Dk. Shika baada ya kujidhamini mwenyewe

Polisi yamwachia Dk. Shika baada ya kujidhamini mwenyewe

​

DK SHIKA NYUMBANI
'Tajiri mtata' akiwasili nyumbani kwake baada ya kuachiwa kwa dhamana leo. [HASHTAG]#MwananchiUpdates[/HASHTAG] [HASHTAG]#MCLDigital[/HASHTAG].
DK Shika URAIANI
Amesema bado mpango wake wa kununua nyumba za Lugumi upo palepale.
Amesema anachosubiri sasa ni fedha kuingizwa kwenye akaunti yake na kulipa asilimia 25 anayodaiwa.
[HASHTAG]#MwananchiUpdates[/HASHTAG] [HASHTAG]#MCLDigital[/HASHTAG]
Kamanda Mambosasa amesema ameagiza Dk Shika ajidhamini na awe anaripoti polisi
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limefikia uamuzi wa kumtaka Dk Louis Shika ‘bilionea wa nyumba za Lugumi’ ajidhamini yeye mwenyewe baada ya kukosa mtu yeyote aliyejitokeza kwenda kutaka kumwekea dhamana.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Novemba 14, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema “uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani anaishi kama mtu wa nyikani.”

Mambosasa ameongeza, “nimeagiza watendaji wangu wamwachie kwa dhamana yaani ajidhamini yeye mwenyewe na awe anakuja kuripoti,” amesema Mambosasa
Kamanda huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya Mwananchi kumtafuta kutaka kujua hatima ya Dk Shika ambaye ameshikiliwa tangu Novemba 9 akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba za kifahari za mfanyabishara Said Lugumi

Dk Shika tangu siku hiyo amekuwa gumzo sehemu mbalimbali kutokana na kile alichokifanya siku ya mnada alipokuwa akipandisha bei dhidi ya washindani wake na moja ya kauli zake zinaendelea kutumika hadi sasa ni ‘Mia 900 itapendeza.’
 
Mbona anaishi sehemu nzuri tu,,walikua wakisema ooh anaishi chumba kimoja sijui nini
 
Hata mie nimeona kuna fundisho hapa kwa upande wa jamaa wapiga mnada..pamoja na kwamba amevuruga mnada lakini kuna funzo (kimsingi faida) ya kuboresha zaidi hasa wanapopiga mnada mali za mamilioni ya fedha achilia mbali hivi vitu vyetu kama makochi na Tv set
Dr. kasaidia kupandisha dau kwenye huo mnada. Vinginevyo nyumba zingenunuliwa kwa bei chee. Tumpongeze kwa hilo.
 
eb4c599ab374fa002035a36be8a93086.jpg
 
Watanzania wanafiki sana. Ndiyo walijitokeza kwa wingi kumzika yule mbakaji pale kinondoni makaburini huku wakiongozwa na rais na baraza lake la mawaziri, na serikali mzima huku kale kabint kalikokua kakibakwa kakiwa ndani nyuma ya nondo za mahabusu

Huyo Mbakwaji alivuka Nyumba ngapi za Watu Wema mpaka akaenda kwa Mbakaji Tena Usiku na Alienda kufanya nini?

Mtoto anatoka alipotoka anaenda kuchezea Mzinga wa Nyuki Halafu unalaumu Nyuki!
 
Ahahahh nikiona habari zake nacheka tu
 
Usimung'unye maneno, Kanumba alikuwa ni mbakaji tu niliamini hivyo na ndio msimamo wangu mpaka kesho.
''Rapist'' of a ''kid'' who can fit a Balimi beer bottle into pretty much any hole in her body!
 
Yaani kawekwa ndani na Matajiri wenzake kina Mengi, Bakhresa, Dewji wala hawakuhangaika kumdhamini? kwa nini Wabongo hatu sapotiani.
 
Back
Top Bottom