Polisi yamwachia Dk. Shika baada ya kujidhamini mwenyewe

Mara imetokea Paap Dr. Shika kapewa bonge shavu, mtaona jinsi ndugu zake wanavyoibuka na kujifanya kumjali. Kuna watu watafungashia Senene na sato na kumletea toka huko kanda ya ziwa.
Watanzania wanafiki sama. Ndiyo walijitokeza kwa wingi kumzika yule mbakaji pale kinondoni makaburini huku wakiongozwa na rais na baraza lake la mawaziri, na serikali mzima huku kale kabint kalikokua kakibakwa kakiwa ndani nyuma ya ndindo za mahabusu
Usimung'unye maneno, Kanumba alikuwa ni mbakaji tu niliamini hivyo na ndio msimamo wangu mpaka kesho.
 
Unaweza ukacheka sana lakini kwa upande mwingine inasikitisha sana, inakuwaje mtu anaishi bila ndugu wala jamaa, atakuwa na maisha magumu sana huyu jamaa... So sad
Ndugu watajitokeza akipata shavu kama Jamaa wa makande,na ndoa ya shs 2000 Kenya, ingekuwa Kenya brand mbalimbali zingekuwa zinamgombea yeye anacheza na day tu,Mungu awezampangia atoke Kwa njia hii.Ngoja amalizane na mambo ya polisi atatoboa tu.
 
Aisee, 900 itapendeza sasa..., hahahahahah... Huyu Dokta Shika kumbe nakaa nae mtaa mmoja na hata nilikuwa simjui maana alikuwa hatoki nje, akirudi tu namsubiri getini kwake nipige nae selfie za kutosha..., hahahahah
 
Chadema hawana tofauti na Dr. Bilionea maana kila mwaka wanaota ndoto ya kwenda ikulu wakati uwezo hawana.
 
shika.jpg


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefikia uamuzi wa kumuachia Dk Louis Shika ‘bilionea wa nyumba za Lugumi’ baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kujidhamini yeye mwenyewe baada ya kukosa mtu yeyote aliyejitokeza kwenda kutaka kumwekea dhamana.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Novemba 14, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema “uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani anaishi kama mtu wa nyikani.”

Mambosasa ameongeza, “nimeagiza watendaji wangu wamwachie kwa dhamana yaani ajidhamini yeye mwenyewe na awe anakuja kuripoti,” amesema Mambosasa

Kamanda huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya Mwananchi kumtafuta kutaka kujua hatima ya Dk Shika ambaye ameshikiliwa tangu Novemba 9 akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba za kifahari za mfanyabishara Said Lugumi

Dk Shika tangu siku hiyo amekuwa gumzo sehemu mbalimbali kutokana na kile alichokifanya siku ya mnada alipokuwa akipandisha bei dhidi ya washindani wake na moja ya kauli zake zinaendelea kutumika hadi sasa ni ‘Mia 900 itapendeza.’

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom