Polisi yamwachia Dk. Shika baada ya kujidhamini mwenyewe

Kamanda Mambosasa amesema ameagiza Dk Shika ajidhamini na awe anaripoti polisi


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limefikia uamuzi wa kumtaka Dk Louis Shika ‘bilionea wa nyumba za Lugumi’ ajidhamini yeye mwenyewe baada ya kukosa mtu yeyote aliyejitokeza kwenda kutaka kumwekea dhamana.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Novemba 14, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema “uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani anaishi kama mtu wa nyikani.”

Mambosasa ameongeza, “nimeagiza watendaji wangu wamwachie kwa dhamana yaani ajidhamini yeye mwenyewe na awe anakuja kuripoti,” amesema Mambosasa


Kamanda huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya Mwananchi kumtafuta kutaka kujua hatima ya Dk Shika ambaye ameshikiliwa tangu Novemba 9 akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba za kifahari za mfanyabishara Said Lugumi

Dk Shika tangu siku hiyo amekuwa gumzo sehemu mbalimbali kutokana na kile alichokifanya siku ya mnada alipokuwa akipandisha bei dhidi ya washindani wake na moja ya kauli zake zinaendelea kutumika hadi sasa ni ‘Mia 900 itapendeza.’


Chanzo: Mwananchi

=====

UPDATES: Dr Shika ameachiwa baada ya kujidhamini mwenyewe



Hahahahahhahahahahahhhahahaha . Dr Shika man of the Year
 
Kwa jinsi alivotupa raha watanzania wamwachie tu, tena ikiwezekana aandae na tamasha lake pale Mlimani City tukalipie kumuona tu, iwe kila anayeingia anashikana naye mkono huku anamwambia "MIA TISA ITAPENDEZA ZAIDI"
 
Unaweza ukacheka sana lakini kwa upande mwingine inasikitisha sana, inakuwaje mtu anaishi bila ndugu wala jamaa, atakuwa na maisha magumu sana huyu jamaa... So sad
njia za MUNGU hazitambuliki na wanadamu inawezekana hii ndio ikawa fursa yake ya kufanikiwa kimaisha.
 
Ukiangalia alivyokuwa anahojiwa na Millard syo bado Dr anasema cash anayo so Tumpe muda tu atazinunua nyumba hizo....
Time will tell

OvA
 
Hoja tajwa yahusika

Wengi ktk watu kwa takriban wiki sasa wameshawishika na huyu jamaa hususan issue nzima ya mnada wa nyumba za lugumi, wako waliocheka kwa kukenua na wako waliocheka kwa kutabasamu provided that kila mtu ameonesha furaha pale habar za huyu jama zinapotajwa, kwa kweli habar zake znapendezesha kama cio kunogesha mitandao kwa sasa.

Aidha, itapendeza kama kila mtanzania mwenye chochote amchangie kama sehem ya kumboost kiuchum ikizingatiwa hata kula yake ni ya shida kodi ya nyumba ndo usiseme. Kumchekesha comedian ni zaid ya ubunifu lkn huyu jamaa alimchekesha hadi joti, joti akakopy na kupest kichekesho hiki bt kwa kunadi cover ya cmyake, sio makazin, vjiwen, majumban na hata nyumban watu wanavinjari na comedy ake bila kuilipia ata sent (mia tisa itapendeza). Tusiishie kumfurahia tuu bt tumchangie ata chenchi kidogo afurahi na yeye

Kiwango nashauri iwe ile ile miasaba , mianane au miatisa itapendeza, na ataekaezidisha hata hamsini ni vzr zaidi, kuhusu namba ipi itumike kukusanyia michango namba yake ihusike direct au toa ushauri wako(eg via moderator, kampun ya cm directly etc)

Kama hujapiga mswaki bas kaa kimya maana maneno yako pia ni uchafu
 
Angetafutiwa kazi ili awe anapata pesa kila mwezi kuliko kumchangia mara moja halafu mkamuacha
"Usimpe samaki mpeleke mtoni mfundishe kuvua"
 
Back
Top Bottom