Foffana
JF-Expert Member
- Oct 29, 2022
- 3,124
- 5,379
#HABARI Mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina Gift Mtanda, amekumbwa na mkasa mkubwa baada ya nyumba yake kupigwa mnada kufuatia mkopo wa benki alioudhamini kwa rafiki wa familia.
Inadaiwa kuwa nyumba hiyo iliwekwa dhamana benki ili kumsaidia rafiki huyo kupata mkopo, lakini baadaye alishindwa kurejesha fedha hizo, hali iliyosababisha hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mdhamini.
Akizungumzia tukio hilo, Gift amesema mabaunsa walifika nyumbani kwake asubuhi ya Machi 25, 2026 na kuanza kutoa vitu vya ndani ya nyumba wakidai wametumwa na benki.
Akieleza kuwa tukio hilo lilimshtua na kumuumiza sana kwa kuwa yeye hakuwa mkopaji moja kwa moja, bali alimdhamini rafiki wa familia ambaye alishindwa kulipa deni, na hivyo kusababisha nyumba yake kupigwa mnada kufidia mkopo huo.
Chanzo: EastAfricaTV