sokwe
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 2,022
- 1,065
Tatizo ni kuwa,wale waliokuwa hawaelewi hatima ya maisha yao itakuwaje baada ya kushindwa kielimu, ndiyo wengi wao waliojoin police force. Ni watu wasiostaarabika,ni wahuni na pia ni majambazi waliohalalishwa kuvaa Police uniforms, sasa mkuu unategemea nini kukutana na jambazi lililohalalishwa kiserikali kufanya uhaini kwa wananchi!
Sifa za huyu jambazi ndani ya uniform ni kuwa Hana shule,anachuki binafsi kwa waliofanikiwa,hana muda wa kuangalia vitambulisho unavyompa, kwani hataelewa hata akisoma,pia utakuwa unampotezea muda wake kuvamia sehemu nyingine.Nahisi watakuwa na malengo maalumu ya makusanyo kwa kila siku,ni mijitu isiyo na maadili. Sasa ukikuta utawala dhaifu unashiriki uhalifu wao, hali ya wahanga wao inakosa maelezo sahihi ya kuelezea. Itabakia ni Mungu pekee kuwa mtetezi wa wanyonge.
Kulinganisha wahaiuni hawa na police wa nchi hizo mkuu ni vitu viwili tofauti kabisa.
Sisi Tz hatuna police,tunao wahalifu walioidhinishwa na serikali dhaifu na kupewa uniform ili kurahisisha dhuluma kwa wananchi.
Mfano mzuri wa police ambao taifa limewahikuwanao ni kama akina Chris Lukosi.
Kama ulishawahi fuatilia mada za huyu mpuuzi, ndiyo ujue tunao wengi wa namna yake hapa Tz.
Utategemea nini mkuu kwa wahanga wao?
Inasikitisha sana mkuu, maana kule kituoni wanaita mtu mmoja mmoja chumbani halafu unapigwa mkwala mzito watakusweka lockup upelekwe mahakamani!! Kwa vile utakataa kupoteza muda wako lockup na hatimaye mahakamani basi inabidi utoe pesa ili utoke kumbuka pia wanapokufikisha kituoni wote mnasachiwa na wallet zenu zote wanazo! Kwahiyo wanajua una kiasi gani kutoka kwako kutategemea utakata pochi kiasi gani, yaani hii topic imeamsha hasira zangu vibaya mno, hela utoe, muda wako upotee bure na vibaka nao wameshaiba kwenye gari lako,Nashukuru sina bunduki vinginevyo na sitokuja ninunue maana unaweza kujikuta ukimlipua mtu kichwa.