Polisi watoa kituko cha kufungia mwaka leo

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,863
5,694
Ni Jana tuu ndugu wadau Jeshi la Polisi kupitia kwa kamanda wake wa operesheni na mafunzo akitoa ufafanuzi kuhusu zuio la mikutano ya nje na maandamano ya vyama vya SIASA alisema kuwa jeshi hilo huwa haliombi msaada toka kwa RAIA katika kupambana na uhalifu kwani hawana ujuzi Wa mafunzo ya KIJESHI na mbinu zake. Hivyo huwa wanaomba msaada ikibidi kutoka majeshi Mengine.

Na akasisitiza kuwa watu kujikusanya na kwenda kulisaidia jeshi hilo huko Dodoma ni kutaka kuvunja Amani na utulivu uliopo na atakaye kwenda atakiona cha mtema kuni.

Leo jeshi la polisi wakishrikiana na polisi ya kimataifa (INTERPOL) kupitia kituo cha habari ITV saa mbili usiku wametangaza kukamatwa kwa wahalifu wa kimataifa pamoja na mali mbalimbali na siraha walizokuwa nazo wahalifu hao.

Pia Jeshi hilo limeomba RAIA wema KULISAIDIA kupambana na uhalifu na walifu mbalimbali hapa nchini ili kudumisha Amani na utulivu.

Hapo sasa ndo nikapata maswali magumu kwangu matatu ya MSINGI.

1. Kwani sisi RAIA tumepata mafunzo ya kijeshi na mbinu hizo lini mpaka watuombe tuwasaidie kazi zao?

2. Au wanataka tuwasaidie kazi hizo halafu watushugulikie Kama walivyo tangaza Jana tuu hata wiki haijaisha?

3. Au kauli ile ya Jana ya Jeshi la polisi imebatilishwa usiku waa manane wakati tumelala?

Karibuni ndugu zangu tuchangie hoja.
 
Kupambana na uhalifu siyo lazima wewe ndiye ukakamate wahalifu.

Unapotoa taarifa police kuhusu uvunjifu wa sheria au amani katika sehemu uliyopo, kimantiki utakuwa umepambana na uhalifu au wahalifu.

Siyo kila mwananchi amefuzu mafunzo ya kupambana na wahalifu ana kwa ana. Kutoa taarifa police ni njia isiyo na gharama kubwa kwa mwananchi wa kawaida katika kupambana na wahalifu.

Hii ndiyo mantiki ya police.
 
Polis jamii haina maana tena...hili jeshi la polisi linatakiwa kufumuliwa
 
Back
Top Bottom