Pendekezo: Kiundwe Chombo kingine cha kuchunguza Jinai zinazofanywa na polisi

MINENE BOY

Member
Jun 3, 2017
17
14
Naomba niingie kwenye Mada moja kwa moja.

Kutokana na malalamiko ya wananchi kutendewa unyama na jeshi la polisi sehemu mbalimbali za nchi, kama vile raia kuuwawa vituo vya polisi, raia kubambikwa kesi n.k.

Napendekeza kiundwe chombo kingine cha kuchunguza jinai zinazofanywa na jeshi la polisi au afisa yoyote wa jeshi hilo, badala ya kutegemea jeshi la polisi lenyewe lijichunguze.

Kuundwa kwa chombo huru nje ya jeshi la polisi kuchunguza jinai zinazofanywa na polisi kutapunguza hisia hasi juu ya jeshi hilo kupendelea maafsa wake wapofanya makosa, pia, kutaongeza ufanisi na umakini kwa jeshi hilo nchini, baadala ya kuunda tume kila linapojitokeza jambo fulani fulani.

Naomba kuwasilisha.
 
kutapunguza hisia hasi juu ya jeshi hilo kupendelea maafsa wake wapofanya makosa, pia, kutaongeza ufanisi na umakini kwa jeshi hilo nchini, baadala ya kuunda tume kila linapojitokeza jambo fulani fulani

Ushauri wako ni mzuri ILA Watawala wana maslahi na hio Swala, pia wao ndio wenye uamuzi wa kuunda hicho chombo na Wananchi ni waoga hatuwezi kuamua jambo lolote.

Pia, Rais aliyepo madarakani kwa sasa hawezi kuamua jambo lolote zaidi ya Teuzi.

Hvyo, hilo swala haliwezekani kwa sasa. May be next time.

Asante.
 
Naomba niingie kwenye Mada moja kwa moja.

Kutokana na malalamiko ya wananchi kutendewa unyama na jeshi la polisi sehemu mbalimbali za nchi, kama vile raia kuuwawa vituo vya polisi, raia kubambikwa kesi n.k.

Napendekeza kiundwe chombo kingine cha kuchunguza jinai zinazofanywa na jeshi la polisi au afisa yoyote wa jeshi hilo, badala ya kutegemea jeshi la polisi lenyewe lijichunguze.

Kuundwa kwa chombo huru nje ya jeshi la polisi kuchunguza jinai zinazofanywa na polisi kutapunguza hisia hasi juu ya jeshi hilo kupendelea maafsa wake wapofanya makosa, pia, kutaongeza ufanisi na umakini kwa jeshi hilo nchini, baadala ya kuunda tume kila linapojitokeza jambo fulani fulani.

Naomba kuwasilisha.
Naunga mkono hoja.

Lakini, kwanza ni kurekebisha sheria inoiongoza jeshi la polisi yaani waziri wa mambo ya ndani apeleke mswaada bungeni wa kubadilisha utendaji wa jeshi la polisi yaani Police reform Act.

Kisha kiundwe hicho chombo unokipendekeza. Chombo hichi kitachunguza malalamiko yote yanohisu utendaji wa jeshi la polisi yakiwemo Yale ya watu kufia vituoni.

Chombo hichi ni lazima kiwe independent na chenye makamishna mchanganyiko wakiwemo pia walowahi kuwa maofisa wa polisi kwa ajili ya kufanya uchunguzi unohitaji utaalam wao.
 
Naomba niingie kwenye Mada moja kwa moja.

Kutokana na malalamiko ya wananchi kutendewa unyama na jeshi la polisi sehemu mbalimbali za nchi, kama vile raia kuuwawa vituo vya polisi, raia kubambikwa kesi n.k.

Napendekeza kiundwe chombo kingine cha kuchunguza jinai zinazofanywa na jeshi la polisi au afisa yoyote wa jeshi hilo, badala ya kutegemea jeshi la polisi lenyewe lijichunguze.

Kuundwa kwa chombo huru nje ya jeshi la polisi kuchunguza jinai zinazofanywa na polisi kutapunguza hisia hasi juu ya jeshi hilo kupendelea maafsa wake wapofanya makosa, pia, kutaongeza ufanisi na umakini kwa jeshi hilo nchini, baadala ya kuunda tume kila linapojitokeza jambo fulani fulani.

Naomba kuwasilisha.
Jambo hili kwa sasa halitawezekana kufanyika kwa hapa Tanzania kutokana na mazingira halisi ya Kikatiba na Kisheria yaliyopo.
Kiini cha kuwepo kwa janga hili baya na kubwa ni Ubovu uliopo kwenye Katiba ya nchi ambayo haitoi Mgawanyo sawa wa Mamlaka na Uhuru kwa Mihimili Mitatu ya Dola, yaani Serikali, Bunge na Mahakama.
Katiba iliyopo imesababisha Mhimili mmoja tu wa Dola yaani Serikali (Executive) kuhodhi Mamlaka yote kabisa ya nchi, huku Mihimili mingine imebaki kuwa kama vile "kanyaboya" na kukosa nguvu kabisa za kiutendaji. Hilo Jeshi la Polisi na TISS ndio vimekuwa vyombo muhimu kabisa kwa Mhimili huo wa Dola uliihoodhi nguvu zote na mamlaka yote ya nchi katika kuwatisha na kuwaangamiza wale watu wote wanaojaribu kukosoa, kuhoji au kuipa changamoto Serikali.Muundo wa Jeshi la Polisi hivi ulivyo siyo ni kwa bahati mbaya Bali ni makusudi kabisa ili kuunufaisha Mhimili wa Dola wa Serikali, hauwezi kubadilishwa kirahisi, labda kwa kushurutishwa vikali.
 
Back
Top Bottom