Kumbe chadema ni zaidi ya vile tunavyokijua.... Aliyoyazungumza mchage yanatufanya sisi watoto wa masikini tuwe na hofu kufunua midomo hasa katika maswala yanayohusu chama hiki.... Kumbe they are capable of doing anything (kama aliyozungumza ni kweli) ... Nawausia masikini wenzangu tujikalie kimyaa tuangalie tu mambo yanavyokwenda .. Na tuviachie vyombo husika vitusaidie kuujua ukweli ........kwa kifupi ukombozi bado uko mbali sana
Unaacha kuogopa matendo ya magamba wenzio, eti unawaogopa CDM?
Ngoja nikupe mifano michache, ya yaliyofanywa na 'washirika' wako.
Kutekwa na kuteswa sana kwa Dr Ulimboka.
Kuumizwa hadi kunyofolewa jicho, kwa Mwanahabari, Absolom Kibanda.
Kuuawa na askari, Mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, (upo ushahidi wa wazi wa tukio hilo wa picha)
Kuuawa kwa Dr Sengondo Mvungi.
Kuuawa kwa bomu kwa wananchi wasio na hatia, pale kanisani Olasiti, Arusha.
Kuuawa kwa bomu, kwa wananchi wasio na hatia pale Arusha, kwenye mkutano wa Chadema.
Kuuawa kwa bomu, na askari walinda usalama kwa yule muuza magazeti, asiye na hatia pale Msamvu, Morogoro.
Na wewe, waweza ongezea unyama mwingine unaoukumbuka, uliofanywa na serikali ya magamba.
Hakika, damu iliyomwagika ya wananchi wasio na hatia, itaendelea kuwalilia serikali ya magamba, hadi mwisho wa dunia!