Polisi wamshughulikie Mchange katika mambo haya 10...

Polisi wamshughulikie Mchange katika mambo haya 10...

Jaman kwenye mdahalo ule Mchange aliziwa kwa hoja sasa ili kujiokoa ikabidi aanze kujiroposha ndo ilikuwa nafuu yake
 
Matukio haya ya siku nyingi mbona uchaguzi umekaribia ndo yanaibuka? mchange leo ni polisi jamii? Mbona polisi mpaka leo hawajatoa hoja yoyote kuhusu hili huu mwaka wa tatu?
 
Nchi yetu bado inashida kubwa,watawala wetu hawapo tayar kubadilika na kujifunza kulingana na wakat.kwa kweli vijana wanaokubal kutumika ovyo ni udharirishaj,namuhurumia kijana mwenzangu kama Mchange jins alvojishushia heshima yake,badala ya kujijenga kisiasa na kuwatumikia watanzania amegeuka kuwatumikia watawala kuwavuruga wanaowapinga ktk udhalimu wanaofanya.
 
nimetokea kuli dharau sana jeshi la polis, weledi ni ziro kabisa, ni jambo baya sana jeshi la polis kufanya siasa.
 
Hyo kijana hajielewi,kama hawez kuchuja hata anavoongea bac akil yake ina matatizo taddy
 
Last edited by a moderator:
nimetokea kuli dharau sana jeshi la polis, weledi ni ziro kabisa, ni jambo baya sana jeshi la polis kufanya siasa.

Police haiwezi kuwa sahaulifu kiasi hiki jamani!, kuna ushahidi wa wazi kutoka huko polisi kulingana na walivyo handle swala lile, kama itafunguliwa kesi hoja zote zitapanguliwa kwa ushahidi huo.
 
JESHI LA POLISI KWA NINI MNATAKA KUWA CHANZO CHA MACHAFUKO TANZANIA? HUO NI UNAFIKI TU KWA SERIKALI AMA KUNA KITU KINGINE MNATAFUTA? WATANZANIA SI WAPUMBAVU. HILI MLIELEWE.

kwa mbaaaaali naanza kuona bora tulikotoka kuliko tulipo, yaana bora enziya Mwema kuliko hapa kwa...!
 
Polisi wasporud ktk mising ya kiapo chao,watadhalilika na kupuuzwa na wananchi.
 
Alinishangaza sana aliposema eti Mwangosi aliuawa na chadema, bila ile picha sijui cdm wangekuwa na hali gani sasa hivi- Lakini, kwa kuwa Mungu hakupenda mwana wake aonewe, alimtuma mtumishi wake, akamuelekeza achukue picha ile muhimu. Hata walipoanza kutunga uongo, akamuelekeza mtumishi wake atoe picha ile kwa wakati muafaka.

Ghafla uongo wa adui ukashindwa. Sasa iweje kijana mwenye mtindio wa ubongo anayeitwa Habibu Mchange apindue ukweli wa kuiita nyeupe kuwa nyeusi na sisi tumkubali wakati tunajua ubongo wake umevia? Penginepo na sisi bongo zetu ziwe na walakini hilo linaweza kutokea!
Ndiyo mpango waliopanga wote Policcm na genge la majambazi baba na mama zao!
image.tiff
 
Sasa polisi div 5 unafikiria watafanya nn ,zaidi ya kutumika kama condom.
 
Nalipongeza jeshi la Polisi Dar kwa kumkamata na kumuweka chini ya ulinzi kada wa chama cha ACT Bw.Habib Mchange, ili kuisaidia jeshi hilo juu ya tuhuma alizozitoa kwa CHADEMA.

Pamoja na mambo mengine, Mchange aulizwe maswali yafuatayo:

1.Kwa kuwa amekiri kutumiwa na CHADEMA kutekeleza mauaji mbalimbali, aseme kwa sasa huko alipo wamemtumia kufanya mauaji ya nani?

2.Kama CHADEMA walimtumia, kwanini tusiamini kuwa hata sasa anatumika kwa kuwa ameshakuwa mtu wa "kutumikatumika"?

3.Kama anakubali CHADEMA walimtumia kupanga mipango ya mauaji, mbona anakataa kuhusika na njama za kumuua Dr.Slaa zilizotolewa na madiwani wa Shinyanga?

4.Aeleze kwa kina nani alimuua Mwangosi na atoe na ushahidi wa kutosha.

5.Aeleze ni kivipi CHADEMA walivaa sare za Polisi na kutekeleza mauaji ya Mwangosi.

6.Aeleze ni Afisa gani wa Polisi aliyewapa CHADEMA hizo sare na silaha za kumuua Mwangosi, na kwanini Afisa huyo hakuchukuliwa hatua.

7.Na kama Polisi wanafanya dili ya kuwaazima CHADEMA sare zao pamoja na Silaha ili kufanya uhalifu, kwanini hakuripoti muda wote hadi alipokuja kusema leo? Miaka mitatu aliyokaa kimya haoni alichangia watanzania wengi wasio na hatia kuuawa na CHADEMA kwa kupewa sare na Polisi?

8.Kwanini hakumshauri Rais Kikwete amfukuze kazi RPC Kamuhanda? maana kwa mujibu wa maelezo yake ndiye aliyesimamia mauaji ya Mwangosi kwa kushirikiana na CHADEMA.

9.Kwa kuwa amekiri yeye ni mtu wa dili za "mauaji" aeleze alishiriki nafasi gani kutekeleza mauaji ya Mwangosi? Alisambaza silaha kwa CHADEMA? Aliwabebea CHADEMA sare za Polisi? Au mchango wake ulikua upi?

10.Mwisho, ASIPEWE DHAMANA kwa kuwa anatuhumiwa kwa kupanga mauaji ( Conspiracy to Commit Murder).

(Pichani ni Habib Mchange enzi za ujana wake).

Maswali ya nyongeza kwa MACHANGE:
1.Jeshi la polisi lilikuwa na maslahi gani kwa CHADEMA,mpaka litoe sare zake kinyume na sheria kuwapa chadema?
2.Kwa kiwango gani Mwangosi alikuwa tishio hadi yeye akakubali kupanga njama za kumwua?
3.Hiyo kazi aliyokuwa anapewa ya kupanga mauaji ilikuwa ni ya kiapo? kama ni ya kiapo kwanini amevunja kiapo?
4.Alipokuwa kuwa akipewa hiyo mipango alikua ana umri gani kiasi chakumfanya kushindwa kufanya mambo kwa utashi na sas hivi ndiyo agundue kuwa alikuwa anafanya vitu kinyume na sheria?
5.Je,machange anataka kutuambia zile sura za askari waliomzunguka mwangosi ni feki? kama ndiyo,mbona mahakama kuu ya Iringa ilijiridhisha alyefanya mauaji ni askari?
Mapendekezo:
Machange ni mhaini hastahili dhamana wala kuwa huru,sheria ichukue mkondo,atendewe haki yake kisheria
 
Maswali ya nyongeza kwa MACHANGE:
1.Jeshi la polisi lilikuwa na maslahi gani kwa CHADEMA,mpaka litoe sare zake kinyume na sheria kuwapa chadema?
2.Kwa kiwango gani Mwangosi alikuwa tishio hadi yeye akakubali kupanga njama za kumwua?
3.Hiyo kazi aliyokuwa anapewa ya kupanga mauaji ilikuwa ni ya kiapo? kama ni ya kiapo kwanini amevunja kiapo?
4.Alipokuwa kuwa akipewa hiyo mipango alikua ana umri gani kiasi chakumfanya kushindwa kufanya mambo kwa utashi na sas hivi ndiyo agundue kuwa alikuwa anafanya vitu kinyume na sheria?
5.Je,machange anataka kutuambia zile sura za askari waliomzunguka mwangosi ni feki? kama ndiyo,mbona mahakama kuu ya Iringa ilijiridhisha alyefanya mauaji ni askari?
Mapendekezo:
Machange ni mhaini hastahili dhamana wala kuwa huru,sheria ichukue mkondo,atendewe haki yake kisheria
 
Hii ishu wangeachiwa vijana wa Mwamunyange wamuhoji huyo Mchange ndipo ukweli ungejulikana

Wanajeshi hawashughuliki na mambo ya kiraia. Jeshi ni serikali ndani ya serikali ina kila kitu chake. Sema wao wamue kuifukuza ccm madarakani kama alivyofanya Morsi huko Misri.
 
Tatizo ni kwamba ama CCM wameishiwa mikakati ya kuudanganya umma au umma unajua mambo mengi zaidi sasa kuliko ilivyokuwa awali.
 
Nashindwa kuelewa,kwa nin mtu mwenye siri za mauaji anayoyaita Ugaidi asikamatwe na kuhojiwa ili kulisafisha jeshi linaloshutumiwa kuwa ndo limekuwa likitumika kuratibu mauaji hayo.
 
Back
Top Bottom