Polisi wadaiwa kuua raia kwa risasi Ngara

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera linadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mkazi wa eneo ya Nyamiaga wilayani humo aliyewatisha kwa shoka askari waliokwenda kumkamata.

Katika tukio hilo la Jumatatu jioni, askari sita wanadaiwa kumuua Philbert Protas ( 30) kwa kumpiga risasi kadhaa mwili baada ya kuwatisha kwa shoka askari hao waliokwenda kumkamata akituhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa mtaa huo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamiaga Robert Choya anasema aliwaita askari hao baada ya kutokea vurugu kwenye eneo lake na walipofika, mtu hyo alikataa kutoa ushirikiano kwa polisi na kuwatisha kuwashambulia kwa shoka ambapo walimpiga risasi na kufariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika hositali ya wilaya hiyo, Nyamiaga.

Hata hivyo, Baba mdogo wa marehemu, Posian Apolinary amesikitishwa na kitendo cha polisi kumpiga risasi mtoto wake na kupelekea kifo wakati wangeweza kutumia njia nyingine kumdhibiti kwani inadaiwa awali alipigwa risasi mguuni na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kujisalimisha.

Diwani wa kata ya Nyamiaga, James Bazisa amesema maziko ya mtu huyo yanafanyika leo nyumbani kwao eneo la Nyamiaga.
 
Sasa wewe watu wana bunduki wewe unawatishia kuwadhuru na kashoka kako kama sio kifo kinakuita ni nini? Watu hawasomi hata alama za nyakati, yani watu wapo na silaha lethal, unapambana nao na shoka? Akufe tu
 
Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera linadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mkazi wa eneo ya Nyamiaga wilayani humo aliyewatisha kwa shoka askari waliokwenda kumkamata.

Katika tukio hilo la Jumatatu jioni, askari sita wanadaiwa kumuua Philbert Protas ( 30) kwa kumpiga risasi kadhaa mwili baada ya kuwatisha kwa shoka askari hao waliokwenda kumkamata akituhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa mtaa huo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamiaga Robert Choya anasema aliwaita askari hao baada ya kutokea vurugu kwenye eneo lake na walipofika, mtu hyo alikataa kutoa ushirikiano kwa polisi na kuwatisha kuwashambulia kwa shoka ambapo walimpiga risasi na kufariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika hositali ya wilaya hiyo, Nyamiaga.

Hata hivyo, Baba mdogo wa marehemu, Posian Apolinary amesikitishwa na kitendo cha polisi kumpiga risasi mtoto wake na kupelekea kifo wakati wangeweza kutumia njia nyingine kumdhibiti kwani inadaiwa awali alipigwa risasi mguuni na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kujisalimisha.

Diwani wa kata ya Nyamiaga, James Bazisa amesema maziko ya mtu huyo yanafanyika leo nyumbani kwao eneo la Nyamiaga.
No comment marehemu alijitakia kifo mtu ana bunduki wewe unatishia kwa shoka
 
Aliyeomba u IGP apewe atakuwa na muarobaini wa kadhia hizi si bure.
 
Mtu una bunduki unatishwa na aliyeshika shoka. Shoka lilivyokua zito polisi wangeweza likwepa. Si wangempa ya mguuni
 
Acha uchama mpuuzi wewe. Saa nyingine akili iwe inakurudi. Unaambiwa marehemu aliwatishia askari hao na shoka wewe ulitaka askari wafanyeje? Au wao ndiyo wenye haki ya kuuawa? Akili kisoda mjinga wewe.
PGO inasemaje?
Wasingeweza kumpiga risasi ya mguu ili kumtuliza?
Huu ni uhuni wa kishamba
 
Back
Top Bottom