Polisi wadai Dr Slaa alikuwa na bunduki

walianzisha na sasa wanalalamika nini walidhani yataishia viwanja vya NMC Arusha?
 
Sheria Tz inatumika tu kwa watu walioko agaist ccm, otherwise ukiwa ndani ya magamba uko juu ya sheria
 
Ni jana tu tumeambiwa ukombozi utaanzia Arusha mbona sasa nasikia sauti za vilio vya wafuasi wa chadema wameshindwa kuiteka benghaz?
 
Maswala ya kumiliki silaha tena kutupiana risasi kwa wanasiasa yamesemwa yametokea sana kwenye Uchaguzi Igunga na mpaka sasa hatua za msingi hazionekani zikilingana na ukali wa taarifa zilizokuwa zikitolewa ktk kipindi kile cha uchaguzi wa Igunga.

Mengi yatasemwa ili kutisha watu ila kimsingi na kiuhalali kila mwenye silaha anapaswa kuwa na silaha yake popote alipo hata mimi binafsi nilikua njugu 17 kiononi(halali) ila sikudhubutu wala sikufikiria kuigusa silaha yangu kwa sababu sikuwa na matumizi nayo kwa wakati ule pale NMC kwenye mkesha.

Dah ungejifanya kichaa ndugu yangu ata umzabe afande mmoja,mi ningekukumbuka daima alaf kukuenzi mtoto wangu anayekuja ningemuita
DAUDI ONXXXXXXY MCHAMBUZI
 
Faiza Foxy mbona unakuwa na element za UDINI hivi ndo unavyofundishwa na viongozi wako tabia hizo? unatia kichefuchefu
 
Tripol imeshindikana kutekwa na wafuasi wako ndani mahabusu wanasubiri kukataa dhamana
 
Kukutwa na silaha ni sahihi kabisa, pale NMC haikuwa kwenye kampeni za kuomba kura,tulikuwa kikazi zaidi na kujihami iwezekanavyo.
 
kama mahabusu ni kuzuri Dr Balaa akapate kusimuliwa na Lema. Lema alikataa dhamana akidhani kuna mahabusu ya wabunge kumbe mahabusu hakuna sheria wakikutamani wanajichukulia kwa nguvu alipotaka kutoka wafungwa wameomba aendelee kubaki
nitakusaidia tu mana naona huna upeo wa kutafakari na kuelewa, 1. KAMANDA LEMA HAKUWA NA KOSA LLT LA KUWAFANYA POLISI WAMKAMATE NA KUMUWEK JELA 2. ALICHOKIFANYA LEMA KUKATAA DHAMANA KITAKUA FUNDISHO KWA KWA SERIKALI NA JESHI LK KUELEWA KW RUMANDE HAPAOGOPEWI TENA 3. KISHERIA LEMA ALIPASWA KUTOLEWA JANA KWA REMOVE ORDER AKAHUDHURIE BUNGE 4.SERIKALI YA CCM IPEOGOPA KUMTOA LEMA JANA KWA KUHOFIA HY PRINCE USHOGA ANAYEENDA ARUSHA KESHO ASIJE AKAKUTANA NA SHAMBPASHAMBRA ZA CDM 5. POLISI WANADHANI KUMZUIA LEMA ASITOKE JELA NI KUZIMA MOTO KUMBE WAMEZIMA MOTO KWA PETROLI.
 
Polisi mkoani Arusha wanadai kuwa baadhi ya wana-CHADEMA waliokuwa kwenye Mkesha wa NMC jumatatu usiku walikuwa na silaha za moto.

Kaimu Kamanda, Akili Mpwapwa amesema kuwa Dr Wilbroad Slaa alikutwa na Bastola “Walther Pistol T2-CAR-61074-327963” wakati alipokamatwa na Bwana Daniel Ezekiel Ogongo ambaye pia alikamatwa kwenye tukio hilo akidaiwa kuwa na ‘Pietro Beretta H-447577 CAT5802’

Cha kushangaza ni kwamba wakati Polisi ikiwaburuza mahakamani wafuasi wa CHADEMA wale wanachama wa CCM ambao wiki kadhaa zilizopita walikutwa na kosa hilo hilo la kuandamana na kufanya mikutano bila kibali mjini Arusha ‘wamesamehewa’ na kupewa ‘onyo kali!’

Polisi wamekiri kuwa pamoja na kwamba wakeshaji pale NMC walikuwa hawajajiandaa na walipovamiwa walikuwa tayari wamechoka kwa kuimba usiku kucha, bila chakula na kwenye mvua na baridi kali bado wasingeweza kuwadhibiti na hivyo kulazimika kutumia magari nane pamoja na lile lori lenye maji ya kuwasha.

Na haikuwa rahisi pia, pamoja na zana zote hizo.

Kama wana akili wangetakiwa kujua kuwa hakika hali inaenda kuwa mbaya.

Hilo la silaha ni sawa tu maana siku zote silaha ni ya kujilinda ila huonekana una hatia pale unapoitumia vibaya. Kwani hizo silaha wameiba? Halafu cha kushangaza Kamanda wa Polisi anasema kiushabiki kuwa ilikuwa na risasi saba! Yeye kama kamanda na mtaalam wa silaha hajui kuwa ili bunduki iitwe silaha lazima iwe na risasi? hizi akili za kukopa pamoja na kufundishwa jinsi ya kutoa maelezo utajua tu. Sasa siamini kama huu moto waliouchokoza wataweza kuuhimili. Kimya kingi kina mshindo, halafu usione adui kakimbia ukadhani amekuacha, huenda anabadili mbinu tu. Poleni ccm kwa kufikiri kwa mambo mnayoyafanya mnavunja watu nguvu. Wadhaifu tu ndio watakaorudi nyuma
 
Hizi sherea Za TZ bana
Ni vichekesho vya Mr..Bean ..

Okay amekutwa na silaha.
Halafu hawasemi alikuwa na
License ya hiyo Silaha au la.
 
Kwa niaba ya uongozi wa CHADEMA ukombozi umeshindika tunaomba radhi kwa Rais kikwete hatutarudia tena kukusanyika kama Libya tunajuta
 
slaa chama umekijenga mwenyewe utakiharibu mwenyewe
user-online.png
kuzou



Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png



Join Date : 20th October 2011
Posts : 43
Rep Power : 0
 
Nakumbuka kunawakati serikali ilitangaza ukaguzi wa silaha nchi nzima,walishawahi kumpiga picha Dr.Slaa akiwa katika foleni ya kusubiria ukaguzi wa silaha yake,kwa hiyo yule jamaa yuko makini atakua anazimiliki kiahali kama ni kweli alikutwa nazo zote mbili na hajabambikiwa,halafu kuhusu kuvamiwa na polisi na kukamatwa ni kitu ambacho mtu yeyote mwenye upeo mkubwa lazima aexpect kwa hiyo kama alikua anazimiliki isivyohalali asingethubutu kutembea nazo kwenye mazingira kama yale.Ishu nyingine nikua raia unaruhusiwa na sheria kutembea na silaha ambayo unaimiliki kihalali,kinachokatazwa ni kuionyesha hadharani.
 
Kamanda MBOWE mbona alisepa na kuteleza kama kambale tofauti na kauli zake za nguvu pepoooooooooooooo pawa, Binafsi nilidhani angeonyesha ukakamavu kwa wafuasi wake kwa kubaki uwanjani mpaka akamatwe
 
Kamanda MBOWE mbona alisepa na kuteleza kama kambale tofauti na kauli zake za nguvu pepoooooooooooooo pawa, Binafsi nilidhani angeonyesha ukakamavu kwa wafuasi wake kwa kubaki uwanjani mpaka akamatwe

Hiyo ni moja ya mbinu ya vita, kwa vile hujui nyamaza tu.
 
slaa chama umekijenga mwenyewe utakiharibu mwenyewe
Masaburi at work. Kajenge CCM inamomonyoka hadi sasa hivi tusi la akina mama ni "Una akilih ovyo kama CCM?" Nadhani ndiyo akili yako
 
Back
Top Bottom