Polisi: Tuko tayari kumlinda Ulimboka!

Sidhani kama kichwa chako kina hata robo ya akili anayopaswa kuwa binadamu, ni nini kazi ya Private bodygurds na ni kwa nini nyumba za mawaziri hazilindwi na polisi bali kampuni za ulinzi binafsi?

Kuna kosa au tatizo lipi Dr Ulimboka kuwa na ulinzi binafsi kama Bernard Membe anavyolindwa na walinzi binafsi pale nyumbani kwake oysterbay karibu na Mambo Club?

SINA HAJA YA KUKUJIBU HAPO KWENYE RED, NA NINA UHAKIKA KWA KIWANGO HICHO ULICHOANDIKA NI MAWAZO YAKO NA YA FAMILIA NZIMA, HONGERENI SANA FAMILIA YA MATOLA. SASA TURUDI KWENYE MADA NA UFAFANUZI HUU SI KWAKO BALI NI KWA WATAKAOSOMA.

Kwanza kabisa SIJASEMA wala KUMFANANISHA Dr. Ulimboka na Waziri kama Membe sijui wa Oysterbay. Ulimboka is just the doctor and the Citizen who appeared to be the victim. Personal bodyguard hazuii polisi kufanya kazi yake polisi akikutwa Mtu anapigwa hawezi kuuliza kwani bodyguard wako yuko wapi?

Arafu matola ukishapona ntakuajili kama bodyguard wa gardener wangu.
 
Watu watendelea kushangaa sana, kwa sababu ya upotoshaji mkubwa uliofanywa na Makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, wanaharakati, na watu ambao hawaitakii mema nchi yetu na kuifanya issue ya Ulimboka kama nafasi pekee ya kuwahadaa watanzania ili waamini kuwa Serikali ndiyo iliyohusika.

Mbona watanzania wanaujua ukweli. Mwenye macho na akili timamu haambiwi tazama!
 
Watu watendelea kushangaa sana, kwa sababu ya upotoshaji mkubwa uliofanywa na Makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, wanaharakati, na watu ambao hawaitakii mema nchi yetu na kuifanya issue ya Ulimboka kama nafasi pekee ya kuwahadaa watanzania ili waamini kuwa Serikali ndiyo iliyohusika.

Naona unahangaika sana, pole sana watanzania wa leo wana uelewa tofauti
 
Mi sioni haja ya mchawi wa leo kumpa mtoto amlee! Huu ni mtego na hatari sana kwasasa wakati Dr ajasema chochote toka arudi.
 
yaani utakuwa ni ***** kupitiliza kama utadhani serikali haisiki kwa hali moja au nyingine, mambo yangekuwa rahisi sana kama jama wangemuua lakini sana kazi imekuwa nyingine baada ya Mungu kuwa karibu zaidi na ulimboka kuliko serikali, maan sasa ata kumua mara ya pili pia isue, maan hii ndiyo itakuwa mbaya zaidi, sasa macho yote yako kwa ulimboka. na kuhusu ulinzi jamaa azidi kumuomba Mungu naye ata mlinda, kwani mara ya kwanza aliye mlinda na kifo walikuwa ni polisi? Jmaani hii yote ni kuonesha Mungu yupo? mengi yanzidi kufichuka
 
Nahisi USALAMA WA TAIFA WAMO HUMU wanatuzuga,piga ua galagaza mnalo hilo ngoja ULLY afunguke!!!!!
 
gazeti la uhuru halijui kama Dr. ulimboka ameisha rudi! hivi hawa watu wanaojidai serikali haiusiki yanawatoka moyoni au wana tuzingua, lakini napata shida kuelewa unajisikiaje unapoongea uongo, ulaghai kwa watu na ukijua kabisa. mi nahisi ni aina fulani ya laana, ua mtu umepata ajira fulani wewe kazi yako ni kudanganya watu alafu unalipwa na serikali! ohhhh mi nachanganyikiwa... lazima ni laana si kawaida... ua kabisa ofisi yako imeandikwa mlangoni mkurugenzi wa propaganda! yaani unajidhiilisha mbele ya jamii wewe ni muongo....Ohooo Mungu wangu hurumia hiki kizazi cha nyoka siku wakija kufungua macho watakuwa wameisha chelewa
 
Mkuu unaonekana kuipenda sana nchi yako na serikali yako sikivu lakini ndio hivyo tena hujui uliyempa dhamana ya usalama wa nchii pendwa kama kweli anailinda au anaihujumu!
Fikra uliyo nayo ni potofu sana, kama kungekuwa hakuna usalama nchi hii basi hata wewe usingekuwa na la kuongea humu, usalama sasa hivi ni 100% isipokuwa kwa wale wanaotemper nao ndo wanaweza kujikuta pabaya, lkn kwa raia mwema ni fuull kujiachia, kwa hilo umechemsha labda useme lingine.
 
IMG_1331.JPG
 
Wakuu hii imekaaje, eti polisi wako tayari kumlinda Dr Ulimboka. Nimeshangazwa sana na kauli hii ya polisi kwani ndio watuhumiwa wakuu wa yote yaliyomkuta huyu daktari.

Tahadhari: Dr kama hana njia nyingine ya kujilinda ni afadhali amwachie Mungu kuliko kujikabidhi mikononi mwa hawa wanaojiita wanausalama kirahisi mamma hiyo.

CHANZO: Gazeti la Mwananchi

JESHI la Polisi limesema liko tayari kumlinda kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka iwapo atahitaji ulinzi huo.

Kauli hiyo imekuja siku mbili tangu daktari huyo wa magonjwa ya binadamu arejee nchini, huku usiri ukiwa umetawala taarifa zake kutokana na kutokuwapo kwa ndugu, jamaa au rafiki aliyekuwa tayari kusema chochote kumhusu.

“Nitachoweza kusema ni kwamba nashukuru mwanangu amerejea salama, lakini siwezi kusema chochote kuhusu mambo yanayomuhusu yeye,” alisema baba mzazi wa Dk Ulimboka, Mzee Mwaitenda.

Tofauti na juzi ambapo nyumbani kwake kulikuwa na watu kadhaa akiwamo Mweitenda, jana mageti yote ya nyumba hiyo iliyoko eneo la Kibangu, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, yalifungwa na hapakuwa na mtu yeyote ndani.

Katikati ya hofu hiyo ya usalama, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema Jeshi lake haliwezi kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka bila yeye mwenyewe kuomba.

"Kwanza walishaamua (madaktari) kuchagua ulinzi, sisi tufanyeje? Atakapoona kuna ulazima atatujulisha," alisema Kenyela na kuongeza;

"Hatuwezi kupeleka askari bila kuombwa. Ukipeleka halafu akasema hawahitaji, itakuwa embarrasing (fedheha) sana. Sisi tunajua amerudi na tunamtakia heri aendelee vizuri, apone na aungane na wenzake,"

Kamanda Kenyela alifafanua kuwa nyumbani kwa mtu ni eneo la faragha ambalo polisi hawawezi kwenda bila kuombwa na kufanya hivyo, ni kitu kisichokubalika.

"Mimi kama kamanda sijapokea ombi lolote kutoka kwa Ulimboka wala kusikia tishio lolote dhidi ya usalama wake. Akiona kuna haja ya kulindwa, aseme tutakwenda," alisema.

Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova alisema hawezi kuzungumzia ulinzi wa Dk Ulimboka kwa sababu tayari madaktari waliomba ulinzi UN.

UN wagoma kuongea
Msemaji wa Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Hoyce Temu hakutaka kueleza endapo taasisi hiyo ya kimataifa ilikubali ombi hilo au la akisema, suala la ulinzi halipaswi kuwekwa hadharani.

Alifafanua kuwa iwapo suala hilo litawekwa hadharani ni sawa na kuwapa nafasi maadui kujua namna mipango ya ulinzi ilivyopangwa.

"Suala la security (usalama) kama lilivyo si suala la kuwekwa wazi kwa public (umma)," alisema Temu.

Mwanzoni mwa Julai mwaka huu, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kiliomba ulinzi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) jijini Dar es Salaam kikieleza kuwa hakina imani na polisi.

Chama hicho kiliomba ulinzi huo baada ya kuwapo na madai kwamba kuna kikundi cha watu kimekusudia kumuua Dk Ulimboka wakati akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Katibu Mkuu wa MAT, Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa endapo UN ilikubali kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka alijibu "haikuwa lazima kwa UN kutujibu."

Aliongeza, "Sisi tuliwasilisha barua, tukitoa malalamiko yetu, namna gani watafanya kazi ya ulinzi siyo lazima watujibu, wao wanataratibu zao za kufanya kazi."

Daktari wake anena

Profesa Joseph Kahamba alisema hajaonana na Dk Ulimboka tangu arejee nchini Jumapili ila anaamini anaendelea vizuri.

Alipoulizwa imekuaje hajaonana na mgonjwa wake wakati yeye ndiye aliyemwandikia rufaa ya kutibiwa nje ya nchi alisema, "Siyo ajabu".

Alisema siyo lazima daktari aliyemwandikia mgonjwa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kuwasiliana naye anaporudi kwa kuwa hili linategemea hali aliyonayo mgonjwa husika.

"Hapa kuna mambo mawili; kuna kurudi akitakiwa tena kulazwa na kurudi kwa maana ya kupona," alieleza Profesa Kahamba baada ya kuulizwa kama ni lazima daktari aliyetoa rufaa awasiliane na mgonjwa baada ya kurudi kwenye matibabu.

Aliendelea "Angerudi (Dk Ulimboka) kwa state (hali) ya kulazwa, lazima angefikia kwangu nimwone, lakini kama amepona, anaweza kwenda kusalimia ndugu na kunywa bia kwanza halafu baada ya siku, wiki au mwezi akaja nikaonana naye."

Profesa Kahamba alieleza "Tangu Ulimboka arudi sijaonana naye zaidi ya kufanya mawasiliano na wenzake kwenye simu ila amepona kwa kuwa hajarudi kwangu."

MAT: Mwacheni apumzike

MAT kimewataka waandishi wa habari kutoendelea kumfuatilia Dk Ulimboka ambaye ni kiongozi wa jumuiya hiyo kwa kile walichoeeleza anatakiwa kupata fursa ya kupumzika.

Makamu wa Rais wa MAT, Dk Prinus Saidia alipotakiwa kueleza ni lini atajitokeza hadharani kufuta kiu ya Watanzania kuhusu kilichomsibu, alisema:

“Yeye mwenyewe ametuomba tumwache apumuzike kwa muda na sisi tumeona hili ni sahihi. Tumemwacha kwanza hadi hapo atakapotuambia kuwa yuko tayari kuungana nasi.”

Dk Saidia alisema madaktari kwa umoja wao wamefurahi kuona Dk Ulimboka amerejea akiwa mzima na kwamba hilo ndilo jambo bora zaidi kuliko kitu kingine chochote kwa sasa.

“Tunamshukuru Mungu Dk Ulimboka amerudi akiwa mzima, hili ndilo lilikuwa la msingi. Hata hivyo, suala liko wazi mgogoro baina yetu (madaktari) na Serikali haujafikia mwafaka. Inatakiwa pande zote zikae na kukubaliana na si upande mmoja kutumia nguvu,” alisema Dk Saidia.

Katika hatua nyingine habari kutoka ndani ya MAT zinasema viongozi wake wamekuwa wakifanya vikao vya ndani tangu juzi kujadili mambo mbalimbali likiwamo la kuandaa mazingira yatakayomwezesha Dk Ulimboka kuzungumza hadharani.

“Kuna vikao vinaendelea tangu jana (juzi), viongozi wanakutana kujadili mambo mbalimbali likiwamo namna Dk Ulimboka atakavyopata fursa ya kuzungumza,” kilisema chanzo hicho.

Dk Ulimboka alitekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.

hivi huyu dokta ULIMOBOKA ana umaarufu gani au hadhi gani hadi kuomba ulinzi kutoka UN . watanzania kweli tuna mambo .kisa daktari tu. hivi nchi hii yote kwake sio salama hadi akaombe msaada UN. haya yetu macho.
 
Wema huu wa Jeshi la Polisi kwa Dr Ulimboka, hata mimi unanitia shaka!! Anyway wanastahili kupongezwa!!
....Unawapongeza kwa lipi aisee? hawa si ndio walichakachua taarifa kuwa aliyemteka Ulimboka amepatikana alienda kutubu kanisani? Uongo na uzandiki wa kupindukia!!!
 
Wednesday, 15 August 2012 07:27

HOFU YATANDA NYUMBANI KWAKE, MILANGO YATIWA KUFULI
Waandishi Wetu
JESHI la Polisi limesema liko tayari kumlinda kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka iwapo atahitaji ulinzi huo.Kauli hiyo imekuja siku mbili tangu daktari huyo wa magonjwa ya binadamu arejee nchini, huku usiri ukiwa umetawala taarifa zake kutokana na kutokuwapo kwa ndugu, jamaa au rafiki aliyekuwa tayari kusema chochote kumhusu.

“Nitachoweza kusema ni kwamba nashukuru mwanangu amerejea salama, lakini siwezi kusema chochote kuhusu mambo yanayomuhusu yeye,” alisema baba mzazi wa Dk Ulimboka, Mzee Mwaitenda.

Tofauti na juzi ambapo nyumbani kwake kulikuwa na watu kadhaa akiwamo Mweitenda, jana mageti yote ya nyumba hiyo iliyoko eneo la Kibangu, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, yalifungwa na hapakuwa na mtu yeyote ndani.
Katikati ya hofu hiyo ya usalama, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema Jeshi lake haliwezi kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka bila yeye mwenyewe kuomba.

"Kwanza walishaamua (madaktari) kuchagua ulinzi, sisi tufanyeje? Atakapoona kuna ulazima atatujulisha," alisema Kenyela na kuongeza;

"Hatuwezi kupeleka askari bila kuombwa. Ukipeleka halafu akasema hawahitaji, itakuwa embarrasing (fedheha) sana. Sisi tunajua amerudi na tunamtakia heri aendelee vizuri, apone na aungane na wenzake,"

Kamanda Kenyela alifafanua kuwa nyumbani kwa mtu ni eneo la faragha ambalo polisi hawawezi kwenda bila kuombwa na kufanya hivyo, ni kitu kisichokubalika.

"Mimi kama kamanda sijapokea ombi lolote kutoka kwa Ulimboka wala kusikia tishio lolote dhidi ya usalama wake. Akiona kuna haja ya kulindwa, aseme tutakwenda," alisema.

Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova alisema hawezi kuzungumzia ulinzi wa Dk Ulimboka kwa sababu tayari madaktari waliomba ulinzi UN.

UN wagoma kuongea
Msemaji wa Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Hoyce Temu hakutaka kueleza endapo taasisi hiyo ya kimataifa ilikubali ombi hilo au la akisema, suala la ulinzi halipaswi kuwekwa hadharani.

Alifafanua kuwa iwapo suala hilo litawekwa hadharani ni sawa na kuwapa nafasi maadui kujua namna mipango ya ulinzi ilivyopangwa.

"Suala la security (usalama) kama lilivyo si suala la kuwekwa wazi kwa public (umma)," alisema Temu.

Mwanzoni mwa Julai mwaka huu, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kiliomba ulinzi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) jijini Dar es Salaam kikieleza kuwa hakina imani na polisi.

Chama hicho kiliomba ulinzi huo baada ya kuwapo na madai kwamba kuna kikundi cha watu kimekusudia kumuua Dk Ulimboka wakati akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Katibu Mkuu wa MAT, Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa endapo UN ilikubali kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka alijibu "haikuwa lazima kwa UN kutujibu."

Aliongeza, "Sisi tuliwasilisha barua, tukitoa malalamiko yetu, namna gani watafanya kazi ya ulinzi siyo lazima watujibu, wao wanataratibu zao za kufanya kazi."

Daktari wake anena

Profesa Joseph Kahamba alisema hajaonana na Dk Ulimboka tangu arejee nchini Jumapili ila anaamini anaendelea vizuri.

Alipoulizwa imekuaje hajaonana na mgonjwa wake wakati yeye ndiye aliyemwandikia rufaa ya kutibiwa nje ya nchi alisema, "Siyo ajabu".

Alisema siyo lazima daktari aliyemwandikia mgonjwa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kuwasiliana naye anaporudi kwa kuwa hili linategemea hali aliyonayo mgonjwa husika.

"Hapa kuna mambo mawili; kuna kurudi akitakiwa tena kulazwa na kurudi kwa maana ya kupona," alieleza Profesa Kahamba baada ya kuulizwa kama ni lazima daktari aliyetoa rufaa awasiliane na mgonjwa baada ya kurudi kwenye matibabu.

Aliendelea "Angerudi (Dk Ulimboka) kwa state (hali) ya kulazwa, lazima angefikia kwangu nimwone, lakini kama amepona, anaweza kwenda kusalimia ndugu na kunywa bia kwanza halafu baada ya siku, wiki au mwezi akaja nikaonana naye."

Profesa Kahamba alieleza "Tangu Ulimboka arudi sijaonana naye zaidi ya kufanya mawasiliano na wenzake kwenye simu ila amepona kwa kuwa hajarudi kwangu."

MAT: Mwacheni apumzike

MAT kimewataka waandishi wa habari kutoendelea kumfuatilia Dk Ulimboka ambaye ni kiongozi wa jumuiya hiyo kwa kile walichoeeleza anatakiwa kupata fursa ya kupumzika.

Makamu wa Rais wa MAT, Dk Prinus Saidia alipotakiwa kueleza ni lini atajitokeza hadharani kufuta kiu ya Watanzania kuhusu kilichomsibu, alisema:

“Yeye mwenyewe ametuomba tumwache apumuzike kwa muda na sisi tumeona hili ni sahihi. Tumemwacha kwanza hadi hapo atakapotuambia kuwa yuko tayari kuungana nasi.”

Dk Saidia alisema madaktari kwa umoja wao wamefurahi kuona Dk Ulimboka amerejea akiwa mzima na kwamba hilo ndilo jambo bora zaidi kuliko kitu kingine chochote kwa sasa.

“Tunamshukuru Mungu Dk Ulimboka amerudi akiwa mzima, hili ndilo lilikuwa la msingi. Hata hivyo, suala liko wazi mgogoro baina yetu (madaktari) na Serikali haujafikia mwafaka. Inatakiwa pande zote zikae na kukubaliana na si upande mmoja kutumia nguvu,” alisema Dk Saidia.

Katika hatua nyingine habari kutoka ndani ya MAT zinasema viongozi wake wamekuwa wakifanya vikao vya ndani tangu juzi kujadili mambo mbalimbali likiwamo la kuandaa mazingira yatakayomwezesha Dk Ulimboka kuzungumza hadharani.

“Kuna vikao vinaendelea tangu jana (juzi), viongozi wanakutana kujadili mambo mbalimbali likiwamo namna Dk Ulimboka atakavyopata fursa ya kuzungumza,” kilisema chanzo hicho.

Dk Ulimboka alitekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.
 
Ha ha te te te Mutuhumu na mtuhumiwa! =~%=%9#%~%*~%~%#~49#7=%4:7#8=~45?
 
Watu watendelea kushangaa sana, kwa sababu ya upotoshaji mkubwa uliofanywa na Makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, wanaharakati, na watu ambao hawaitakii mema nchi yetu na kuifanya issue ya Ulimboka kama nafasi pekee ya kuwahadaa watanzania ili waamini kuwa Serikali ndiyo iliyohusika.

ita chochote upendacho lakini ukweli utabaki ni ukweli alpha mpaka omega uwe unapenda au haupendi; you are stuck with it and thats how it shall remain in the annals of history, period.
 
ikitokea wanaenda kumlinda na mimi nitawaomba siku moja waje wanilinde kwangu!!!!!!! Sijawahi hata siku moja polisi wanaomba kumlinda mwananchi wa kawaida . Ninachojua ni kwamba kwama kuna mwananchi ametishiwa basi atatoa taarifa polisi na wao watashauri inavyopasa lakini sijawahi sikia eti wanakwenda kutoa ulinzoi kwa aliyetishiwa
 
Back
Top Bottom