Polisi: Tuko tayari kumlinda Ulimboka!

Polisi: Tuko tayari kumlinda Ulimboka!

Kumbuka siku Uli aliporudi toka S.A alitoa shukurani kwa makundi karibu yote isipokuwa SERIKALI tu. Tujifunze nini kutokana na ile ubaguzi?
Kumbe wewe hujui kuwa SERIKALI ni watu? halafu usisahau pia kua Ulimboka sasa mwanasia wa kambi ya upinzani na amekwishaandaliwa jimbo la kugombea huko kwao, sasa isingekuwa rahisi aishukuru serikali inayoongozwa na chama tawala. Hata siku moja ulishasikia, MBOWE, SALAA au mwanasiasa uchwara asiyejua maana ya upinzani akiishukuru Serikali kwa jema lolote?
 
Dah..huyu ulimboka atakuja kuacha watu solemba kama mwakyembe...anatoa mpaka siku 40 ili atuletee story AU NDO IMETOKA HIYO.
 
Hivi Polisi ndiyo watuhumiwa wakuu wa sakata la Ulimboka au usalama wa Taifa? Naomba sasa mnadhihaki hivi vyombo vyetu vya ulinzi.

Yaani unajidai punguani kutokuliona hilo? Jamani acheni unafiki!!!!
 
Aiseeee mmeku embu kwanza 2mwache dr awataje kwa mdomo wake walio mdhuru na akitaja wale wale watu wa mwahahalisi ndio nitahamini kwamba jei kei si dhaifu bali ni tahira



naanza na mbege leo
 
Nimeiskia hii kwenye UCHAMBUZI WA MAGAZETI MAGIC FM,NIMEISHIA KUGUNA TU NA KUCHEKA,,,,,,,,,
MWEMA ANApOENDELEZA WEMA KTK JESHI LA POLISI
 
Wema wa Paka kwa panya, kama si unafiki ni nini? Danganywa Ully
Paka na Panya.jpg
 
HOFU YATANDA NYUMBANI KWAKE, MILANGO YATIWA KUFULI

JESHI la Polisi limesema liko tayari kumlinda kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka iwapo atahitaji ulinzi huo.Kauli hiyo imekuja siku mbili tangu daktari huyo wa magonjwa ya binadamu arejee nchini, huku usiri ukiwa umetawala taarifa zake kutokana na kutokuwapo kwa ndugu, jamaa au rafiki aliyekuwa tayari kusema chochote kumhusu.

“Nitachoweza kusema ni kwamba nashukuru mwanangu amerejea salama, lakini siwezi kusema chochote kuhusu mambo yanayomuhusu yeye,” alisema baba mzazi wa Dk Ulimboka, Mzee Mwaitenda.

Tofauti na juzi ambapo nyumbani kwake kulikuwa na watu kadhaa akiwamo Mweitenda, jana mageti yote ya nyumba hiyo iliyoko eneo la Kibangu, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, yalifungwa na hapakuwa na mtu yeyote ndani.
Katikati ya hofu hiyo ya usalama, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema Jeshi lake haliwezi kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka bila yeye mwenyewe kuomba.

"Kwanza walishaamua (madaktari) kuchagua ulinzi, sisi tufanyeje? Atakapoona kuna ulazima atatujulisha," alisema Kenyela na kuongeza;

"Hatuwezi kupeleka askari bila kuombwa. Ukipeleka halafu akasema hawahitaji, itakuwa embarrasing (fedheha) sana. Sisi tunajua amerudi na tunamtakia heri aendelee vizuri, apone na aungane na wenzake,"

Kamanda Kenyela alifafanua kuwa nyumbani kwa mtu ni eneo la faragha ambalo polisi hawawezi kwenda bila kuombwa na kufanya hivyo, ni kitu kisichokubalika.

"Mimi kama kamanda sijapokea ombi lolote kutoka kwa Ulimboka wala kusikia tishio lolote dhidi ya usalama wake. Akiona kuna haja ya kulindwa, aseme tutakwenda," alisema.

Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova alisema hawezi kuzungumzia ulinzi wa Dk Ulimboka kwa sababu tayari madaktari waliomba ulinzi UN.

UN wagoma kuongea

Msemaji wa Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Hoyce Temu hakutaka kueleza endapo taasisi hiyo ya kimataifa ilikubali ombi hilo au la akisema, suala la ulinzi halipaswi kuwekwa hadharani.

Alifafanua kuwa iwapo suala hilo litawekwa hadharani ni sawa na kuwapa nafasi maadui kujua namna mipango ya ulinzi ilivyopangwa.

"Suala la security (usalama) kama lilivyo si suala la kuwekwa wazi kwa public (umma)," alisema Temu.

Mwanzoni mwa Julai mwaka huu, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kiliomba ulinzi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) jijini Dar es Salaam kikieleza kuwa hakina imani na polisi.

Chama hicho kiliomba ulinzi huo baada ya kuwapo na madai kwamba kuna kikundi cha watu kimekusudia kumuua Dk Ulimboka wakati akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Katibu Mkuu wa MAT, Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa endapo UN ilikubali kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka alijibu "haikuwa lazima kwa UN kutujibu."

Aliongeza, "Sisi tuliwasilisha barua, tukitoa malalamiko yetu, namna gani watafanya kazi ya ulinzi siyo lazima watujibu, wao wanataratibu zao za kufanya kazi."

Daktari wake anena

Profesa Joseph Kahamba alisema hajaonana na Dk Ulimboka tangu arejee nchini Jumapili ila anaamini anaendelea vizuri.

Alipoulizwa imekuaje hajaonana na mgonjwa wake wakati yeye ndiye aliyemwandikia rufaa ya kutibiwa nje ya nchi alisema, "Siyo ajabu".

Alisema siyo lazima daktari aliyemwandikia mgonjwa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kuwasiliana naye anaporudi kwa kuwa hili linategemea hali aliyonayo mgonjwa husika.

"Hapa kuna mambo mawili; kuna kurudi akitakiwa tena kulazwa na kurudi kwa maana ya kupona," alieleza Profesa Kahamba baada ya kuulizwa kama ni lazima daktari aliyetoa rufaa awasiliane na mgonjwa baada ya kurudi kwenye matibabu.

Aliendelea "Angerudi (Dk Ulimboka) kwa state (hali) ya kulazwa, lazima angefikia kwangu nimwone, lakini kama amepona, anaweza kwenda kusalimia ndugu na kunywa bia kwanza halafu baada ya siku, wiki au mwezi akaja nikaonana naye."

Profesa Kahamba alieleza "Tangu Ulimboka arudi sijaonana naye zaidi ya kufanya mawasiliano na wenzake kwenye simu ila amepona kwa kuwa hajarudi kwangu."

MAT: Mwacheni apumzike

MAT kimewataka waandishi wa habari kutoendelea kumfuatilia Dk Ulimboka ambaye ni kiongozi wa jumuiya hiyo kwa kile walichoeeleza anatakiwa kupata fursa ya kupumzika.

Makamu wa Rais wa MAT, Dk Prinus Saidia alipotakiwa kueleza ni lini atajitokeza hadharani kufuta kiu ya Watanzania kuhusu kilichomsibu, alisema:

“Yeye mwenyewe ametuomba tumwache apumuzike kwa muda na sisi tumeona hili ni sahihi. Tumemwacha kwanza hadi hapo atakapotuambia kuwa yuko tayari kuungana nasi.”

Dk Saidia alisema madaktari kwa umoja wao wamefurahi kuona Dk Ulimboka amerejea akiwa mzima na kwamba hilo ndilo jambo bora zaidi kuliko kitu kingine chochote kwa sasa.

“Tunamshukuru Mungu Dk Ulimboka amerudi akiwa mzima, hili ndilo lilikuwa la msingi. Hata hivyo, suala liko wazi mgogoro baina yetu (madaktari) na Serikali haujafikia mwafaka. Inatakiwa pande zote zikae na kukubaliana na si upande mmoja kutumia nguvu,” alisema Dk Saidia.

Katika hatua nyingine habari kutoka ndani ya MAT zinasema viongozi wake wamekuwa wakifanya vikao vya ndani tangu juzi kujadili mambo mbalimbali likiwamo la kuandaa mazingira yatakayomwezesha Dk Ulimboka kuzungumza hadharani.

“Kuna vikao vinaendelea tangu jana (juzi), viongozi wanakutana kujadili mambo mbalimbali likiwamo namna Dk Ulimboka atakavyopata fursa ya kuzungumza,” kilisema chanzo hicho.

Dk Ulimboka alitekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.
 
POLISI ni Taasisi,SI WATU. Polisi itabakia kuwa Polisi kama mhimili wa dola na Kova au Mwema watabakia kuwa wao. kwa hiyo jukumu la usalama wa raia bado ni la Polisi na watatakiwa kumlinda kwa ya utashi wao.
 
Aiseeee mmeku embu kwanza 2mwache dr awataje kwa mdomo wake walio mdhuru na akitaja wale wale watu wa mwahahalisi ndio nitahamini kwamba jei kei si dhaifu bali ni tahira

si vibaya kuwaachia polisi kwani kuna msemo unao sema kama unahisi kuna mchawi ananyemelea mtoto wako dawa ni kumkabidhi huyo mtoto hata mhduru hata kidogo ataogopa kuumbuka!!!
 
Hapo si suala la Mchawi mpe mwanao akulelee, bali ni penye ukweli uongo hujitenga, Nadhani sasa ni wakati wa Wanaharakati, na watu kama akina KUBENEA kuumbuka kwa upotoshaji na hila zao za kuvichafua vyombo vya ulinzi.

Inaonekana dhahiri wewe mwezetu unaishi na kiwiliwili siamini kabisa kama una kichwa, maana ni hafadhali hata ya mkwele aliyezaliwa bila kichwa akawekea nazi kureplace kichwa.
 
POLISI ni Taasisi,SI WATU. Polisi itabakia kuwa Polisi kama mhimili wa dola na Kova au Mwema watabakia kuwa wao. kwa hiyo jukumu la usalama wa raia bado ni la Polisi na watatakiwa kumlinda kwa ya utashi wao.
Sidhani kama kichwa chako kina hata robo ya akili anayopaswa kuwa binadamu, ni nini kazi ya Private bodygurds na ni kwa nini nyumba za mawaziri hazilindwi na polisi bali kampuni za ulinzi binafsi?

Kuna kosa au tatizo lipi Dr Ulimboka kuwa na ulinzi binafsi kama Bernard Membe anavyolindwa na walinzi binafsi pale nyumbani kwake oysterbay karibu na Mambo Club?
 
Ninapredict kitakachotokea tutanyimwa misaada muda si mrefu,serikali itakuwa taabani kifedha,Ulimboka atakuwa anatoa evidence kwa mabalozi sasa
 
Ulimboka mwenyewe kisha sema anaujua ukweli yeye. Nadhani kukubali kulindwa na dola ni dhahiri kuwa pengine Serikali haikuhusika na anajua wabaya wake wanaomzunguka hawako Serikalini tena.

mdau mbona unajichanganya? kuna mahali popote amekubali kulindwa na vyombo usalama? kama huna cha kuandika kaa kimya, usitutoe kwenye mada.
 
ulinzi ni muhimu kupatiwa bila kujali ni serikali au ulinzi binafsi
 
Sidhani kama kichwa chako kina hata robo ya akili anayopaswa kuwa binadamu, ni nini kazi ya Private bodygurds na ni kwa nini nyumba za mawaziri hazilindwi na polisi bali kampuni za ulinzi binafsi?

Kuna kosa au tatizo lipi Dr Ulimboka kuwa na ulinzi binafsi kama Bernard Membe anavyolindwa na walinzi binafsi pale nyumbani kwake oysterbay karibu na Mambo Club?

taratibu mkuu,punguza hasira.mungu hapendi hapo kwenye red
 
Mbinu chafu za kisovieti ya zamani; ili wamsogelee wawe karibu naye zaidi ili wapate mwanya wa kumdhuru!!

kama jeshi la polisi lilishindwa kumlinda naibu waziri mzima Harison Mwakyembe hadi akalishwa sumu na kudhurika iweje leo wajinasibu kuwa wanataka kumlinda raia wa kawaida tu ka Dr. Ullimboka.

Madaktari na wanafamilia msikubali uchafu huo, tangu sakata hilo lianze wameshindwa kumuhoji Dr. Deo aliyekuwa na Ulli wakati wa tukio, kwa nini hawajawahoji Dr Hellen Kijo Bisimba badala yake wamekwenda kutafuta mkenya wa kutengeneza, hatudanganyiki n'go!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mashetani wengine bana
mbona shetani mkubwa akisikia unaingiaguest kuruka ukuta anakimbia nyie hata kwenye mauwaji
amwoni haya mnajitangaza kabisa kwa waandishi
shame
 
Back
Top Bottom