Polisi: Tuko tayari kumlinda Ulimboka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi: Tuko tayari kumlinda Ulimboka!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Straight corner, Aug 15, 2012.

 1. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wakuu hii imekaaje, eti polisi wako tayari kumlinda Dr Ulimboka. Nimeshangazwa sana na kauli hii ya polisi kwani ndio watuhumiwa wakuu wa yote yaliyomkuta huyu daktari.

  Tahadhari: Dr kama hana njia nyingine ya kujilinda ni afadhali amwachie Mungu kuliko kujikabidhi mikononi mwa hawa wanaojiita wanausalama kirahisi mamma hiyo.

  CHANZO: Gazeti la Mwananchi

  JESHI la Polisi limesema liko tayari kumlinda kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka iwapo atahitaji ulinzi huo.

  Kauli hiyo imekuja siku mbili tangu daktari huyo wa magonjwa ya binadamu arejee nchini, huku usiri ukiwa umetawala taarifa zake kutokana na kutokuwapo kwa ndugu, jamaa au rafiki aliyekuwa tayari kusema chochote kumhusu.

  "Nitachoweza kusema ni kwamba nashukuru mwanangu amerejea salama, lakini siwezi kusema chochote kuhusu mambo yanayomuhusu yeye," alisema baba mzazi wa Dk Ulimboka, Mzee Mwaitenda.

  Tofauti na juzi ambapo nyumbani kwake kulikuwa na watu kadhaa akiwamo Mweitenda, jana mageti yote ya nyumba hiyo iliyoko eneo la Kibangu, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, yalifungwa na hapakuwa na mtu yeyote ndani.

  Katikati ya hofu hiyo ya usalama, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema Jeshi lake haliwezi kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka bila yeye mwenyewe kuomba.

  "Kwanza walishaamua (madaktari) kuchagua ulinzi, sisi tufanyeje? Atakapoona kuna ulazima atatujulisha," alisema Kenyela na kuongeza;

  "Hatuwezi kupeleka askari bila kuombwa. Ukipeleka halafu akasema hawahitaji, itakuwa embarrasing (fedheha) sana. Sisi tunajua amerudi na tunamtakia heri aendelee vizuri, apone na aungane na wenzake,"

  Kamanda Kenyela alifafanua kuwa nyumbani kwa mtu ni eneo la faragha ambalo polisi hawawezi kwenda bila kuombwa na kufanya hivyo, ni kitu kisichokubalika.

  "Mimi kama kamanda sijapokea ombi lolote kutoka kwa Ulimboka wala kusikia tishio lolote dhidi ya usalama wake. Akiona kuna haja ya kulindwa, aseme tutakwenda," alisema.

  Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova alisema hawezi kuzungumzia ulinzi wa Dk Ulimboka kwa sababu tayari madaktari waliomba ulinzi UN.

  UN wagoma kuongea
  Msemaji wa Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Hoyce Temu hakutaka kueleza endapo taasisi hiyo ya kimataifa ilikubali ombi hilo au la akisema, suala la ulinzi halipaswi kuwekwa hadharani.

  Alifafanua kuwa iwapo suala hilo litawekwa hadharani ni sawa na kuwapa nafasi maadui kujua namna mipango ya ulinzi ilivyopangwa.

  "Suala la security (usalama) kama lilivyo si suala la kuwekwa wazi kwa public (umma)," alisema Temu.

  Mwanzoni mwa Julai mwaka huu, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kiliomba ulinzi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) jijini Dar es Salaam kikieleza kuwa hakina imani na polisi.

  Chama hicho kiliomba ulinzi huo baada ya kuwapo na madai kwamba kuna kikundi cha watu kimekusudia kumuua Dk Ulimboka wakati akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

  Katibu Mkuu wa MAT, Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa endapo UN ilikubali kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka alijibu "haikuwa lazima kwa UN kutujibu."

  Aliongeza, "Sisi tuliwasilisha barua, tukitoa malalamiko yetu, namna gani watafanya kazi ya ulinzi siyo lazima watujibu, wao wanataratibu zao za kufanya kazi."

  Daktari wake anena

  Profesa Joseph Kahamba alisema hajaonana na Dk Ulimboka tangu arejee nchini Jumapili ila anaamini anaendelea vizuri.

  Alipoulizwa imekuaje hajaonana na mgonjwa wake wakati yeye ndiye aliyemwandikia rufaa ya kutibiwa nje ya nchi alisema, "Siyo ajabu".

  Alisema siyo lazima daktari aliyemwandikia mgonjwa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kuwasiliana naye anaporudi kwa kuwa hili linategemea hali aliyonayo mgonjwa husika.

  "Hapa kuna mambo mawili; kuna kurudi akitakiwa tena kulazwa na kurudi kwa maana ya kupona," alieleza Profesa Kahamba baada ya kuulizwa kama ni lazima daktari aliyetoa rufaa awasiliane na mgonjwa baada ya kurudi kwenye matibabu.

  Aliendelea "Angerudi (Dk Ulimboka) kwa state (hali) ya kulazwa, lazima angefikia kwangu nimwone, lakini kama amepona, anaweza kwenda kusalimia ndugu na kunywa bia kwanza halafu baada ya siku, wiki au mwezi akaja nikaonana naye."

  Profesa Kahamba alieleza "Tangu Ulimboka arudi sijaonana naye zaidi ya kufanya mawasiliano na wenzake kwenye simu ila amepona kwa kuwa hajarudi kwangu."

  MAT: Mwacheni apumzike

  MAT kimewataka waandishi wa habari kutoendelea kumfuatilia Dk Ulimboka ambaye ni kiongozi wa jumuiya hiyo kwa kile walichoeeleza anatakiwa kupata fursa ya kupumzika.

  Makamu wa Rais wa MAT, Dk Prinus Saidia alipotakiwa kueleza ni lini atajitokeza hadharani kufuta kiu ya Watanzania kuhusu kilichomsibu, alisema:

  "Yeye mwenyewe ametuomba tumwache apumuzike kwa muda na sisi tumeona hili ni sahihi. Tumemwacha kwanza hadi hapo atakapotuambia kuwa yuko tayari kuungana nasi."

  Dk Saidia alisema madaktari kwa umoja wao wamefurahi kuona Dk Ulimboka amerejea akiwa mzima na kwamba hilo ndilo jambo bora zaidi kuliko kitu kingine chochote kwa sasa.

  "Tunamshukuru Mungu Dk Ulimboka amerudi akiwa mzima, hili ndilo lilikuwa la msingi. Hata hivyo, suala liko wazi mgogoro baina yetu (madaktari) na Serikali haujafikia mwafaka. Inatakiwa pande zote zikae na kukubaliana na si upande mmoja kutumia nguvu," alisema Dk Saidia.

  Katika hatua nyingine habari kutoka ndani ya MAT zinasema viongozi wake wamekuwa wakifanya vikao vya ndani tangu juzi kujadili mambo mbalimbali likiwamo la kuandaa mazingira yatakayomwezesha Dk Ulimboka kuzungumza hadharani.

  "Kuna vikao vinaendelea tangu jana (juzi), viongozi wanakutana kujadili mambo mbalimbali likiwamo namna Dk Ulimboka atakavyopata fursa ya kuzungumza," kilisema chanzo hicho.

  Dk Ulimboka alitekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Eti nini?
   
 3. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Wema huu wa Jeshi la Polisi kwa Dr Ulimboka, hata mimi unanitia shaka!! Anyway wanastahili kupongezwa!!
   
 4. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Mchawi mpe mwanao akulelee!
   
 5. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,224
  Likes Received: 1,069
  Trophy Points: 280
  Mimi naona ni sawa tu,atakuwa kwenye mikono salama zaidi akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwasababu polisi watataka kuondoa fikra kwa watu kuwa wao wanahusika (Sina uhakika kama wanahusika na lile tukio) hivyo watajitahidi kwa kila namna kuhakikisha anakuwa salama. Kuwepo kwake salama pia kutaisafisha image ya serikali juu ya uhusika wa lile tukio,jamani haiwezekani aendelee kukaa mafichoni akilindwa na madaktari wakati wanaomuwinda wanaonekana kuwa ni watu hatari uki-reffer lile tukio lililomkuta.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hivi Polisi ndiyo watuhumiwa wakuu wa sakata la Ulimboka au usalama wa Taifa? Naomba sasa mnadhihaki hivi vyombo vyetu vya ulinzi.
   
 7. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wonderful!
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ulimboka mwenyewe kisha sema anaujua ukweli yeye. Nadhani kukubali kulindwa na dola ni dhahiri kuwa pengine Serikali haikuhusika na anajua wabaya wake wanaomzunguka hawako Serikalini tena.
   
 9. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hahahaaa! Sio rahisi Namna hii.
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Watu watendelea kushangaa sana, kwa sababu ya upotoshaji mkubwa uliofanywa na Makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, wanaharakati, na watu ambao hawaitakii mema nchi yetu na kuifanya issue ya Ulimboka kama nafasi pekee ya kuwahadaa watanzania ili waamini kuwa Serikali ndiyo iliyohusika.
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hapo si suala la Mchawi mpe mwanao akulelee, bali ni penye ukweli uongo hujitenga, Nadhani sasa ni wakati wa Wanaharakati, na watu kama akina KUBENEA kuumbuka kwa upotoshaji na hila zao za kuvichafua vyombo vya ulinzi.
   
 12. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,862
  Likes Received: 4,244
  Trophy Points: 280
  Ulichosema hapo ni majibu, sasa uliza swali.
   
 13. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kubenea alikuja na evidence zilizojaribu kuonyesha jinsi gani Polisi wamehusika, majina na namba za simu...ambazo polisi hawakukanusha wala kutoa evidence zao kuwa hawajahusika...Polisi ndio mchawi hapa, na mchawi akiumbuka mara zote ubaki akijikanganya tuu! Iweje mtu aliyesema 'wewe ndio umenipiga'...umpe ofa ya kumlinda?!
   
 14. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  kuhusu kushiriki kwa serikali katika uovu huu ondoa shaka 100% imehusika! mimi nina wasiwasi Ulimboka ana maadui wengine zaidi ya serikali pia maadui wa serikali nao huenda wakamuwinda Ulimboka his issue is very complex more than we can imagine!!
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Familia ya Ulimboka msikubali kuingia kwenye mtego wa polisi......Ighondu @ Work
   
 16. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kumbuka siku Uli aliporudi toka S.A alitoa shukurani kwa makundi karibu yote isipokuwa SERIKALI tu. Tujifunze nini kutokana na ile ubaguzi?
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Baada ya Kubenea kuanika mawasiliano ya wauaji na ulimboka na ikulu wakakimbilia kulifungia gazeti la mwanahalisi!bila kujibu yaliyoandikwa na Mwanahalisi!!
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hata mimi naungana na Mamaisara, mbona ilisemekana kuwa mtuhumiwa namba moja ni idara ya usalama wa Taifa? Kesho tutaambiwa ni mghambo na mwishowe tutaambiwa ni sungusungu ndiyo walihusika, "NI HABARI ZA UCHUNGUZI ZA SAID KUBENEA?. teh teh teh, mimi napita tu jamani.
   
 19. d

  dalunda Member

  #19
  Aug 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  sikiliza bro, kubenea alikuja na evidence kwa kuwataja zaidi usalama wa taifa waliohusika na tukio zima, mpaka wakalifungia gazeti lake, na watu walifukuzwa kazi kule tigo mtu kibao walipigwa chini,

  wahusika wakuu ni usalama wa taifa, unless wale wengineo wawe ni polisi, polisi wanahusishwa na ku-support kilichofanywa na usalama wa taifa, maana baada ya kutekwa walikwenda na migari yao eneo la tukio na hawakutoa ushirikiano, wakawa wanarandaranda kupotezea, vilevile ulimboka alipopelekwa polisi wakawa wanapotezea hawana time kumharakishia kwenda hospitalini mapema, na walikuwa wako kuhakikisha anakufaaaaa

  lakini zaidi ni usalama wa taifa
   
 20. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu unaonekana kuipenda sana nchi yako na serikali yako sikivu lakini ndio hivyo tena hujui uliyempa dhamana ya usalama wa nchii pendwa kama kweli anailinda au anaihujumu!
   
Loading...