TPF NET Arusha yasema elimu zaidi itamaliza vitendo vya ukatili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Mtaandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha umesema elimu Zaidi itasaidia kuibadilisha jamii ya watanzania katika kukabiliana na vitendo vya ukatili vinavyotokea katika maeneo tofauti tofauti huku likibainisha kuwa litaendelea kutoa elimu ili kubadilisha fikra potofu kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na kaimu mwenyekiti wa mtaandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha TPF-net mrakibu msadizi wa Polisi ASP Jane Magesa wakati walipofika kutoa elimu katika kituo cha nyumba salama ya amani Arusha ambapo amebainisha kuwa sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na kutokuelewa kwa wananchi juu ya ukatili wa kijinsia.
f72d1fa1-2a12-435c-ae75-e1d86d074fc5.jpeg

e51a3a30-37df-451e-b364-ff839b81f015.jpeg

Ameongeza kuwa mtaandao huo wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha utaendelea kutoa elimu ili kuifanya jamii kuendelea kuwa salama na kuepuka kutenda vitendo vya ukatili huku akiwataka wanawanchi kuendelea kukemea vikali tabaia ya baadhi ya watu wachache wanaofanya vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la jinsia na Watoto Wilaya ya Arusha Mkaguzi msadizi wa Polisi A/Insp Urusula Mosha amewahimiza wananchi wananchi kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili kwa Jeshi la Polisi huku akiwataka pia kutumia nyumba za ibada kutoa taarifa hizo za vitendo vya ukatili ili ziwafikie kwa haraka na kuzifanyia kazi.

Nae Mlezi wa kituo cha Nyumba salama ya amani Arusha mbali na kupongeza mtaandao wa Polisi wanawake TPF- net Mkoa wa Arusha amewaomba Jeshi hilo kuto ishia kituo hicho kutoa elimu wafike pia katika makundi mengine ya wahanga wa ukatili na kutoa elimu kwa wananchi ili kujenga jamii yenye uelewa mpakana juu ya vitendo vya ukatili.

Mbali na ellimu wametoa vitu mbalimbali kwa ajili ya kwafariji Watoto wa kituo hicho.
 
Elimu haimalizi vitendo vya kikatili, Maombi na hofu ya Mungu ndio itakayomaliza...

Hata asiye na Elimu hatafanya Ukatili
 
Back
Top Bottom