Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,234
Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara linawashikilia watu13 kwa tuhuma za wizi wa pembejeo za wakulima wa korosho msimu wa 2024/2025.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano, Kamanda wa Polisi Mkoa huo SACP Issa Sulemani amesema mnamo Agosti 29, 2025 polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na Bodi ya Korosho (CBT) walifanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) katika Halmashauri ya Mji Nanyamba na baadhi ya watumishi wa serikali.
Watuhumiwa wanadaiwa kugawa pembejeo kwa “wakulima hewa” na kusababisha upotevu wa pembejeo za maji lita 308 na mifuko 12 ya sulphur aina ya simba zenye thamani ya zaidi ya milioni 15.8.
Kamanda Issa amesema uchunguzi bado unaendelea na pindi utakapokamilika wote watafikishwa mahakamani, na amewaonya wananchi kutojihusisha na wizi wa pembejeo kwa kuwa jeshi la polisi na vyombo vya usalama vitachukua hatua kali.