RRONDO
Platinum Member
- Jan 3, 2010
- 59,495
- 135,475
Wafanyabiashara wawili marafiki wauawa kikatili
Marehemu Reinald Chuwa
Marehemu Amedeus Nasau
Watu wanaosaidikiwa kuwa majambazi wamefanya kufuru Dar kwa kuwapiga risasi wafanyabiashara wawili, baada ya kuvamia nyumba zao eneo la Kimara Temboni juzi usiku, muda mfupi baada ya kutoka kwenye sehemu zao za biashara.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wafanyabiashara hao ambao ni marafiki wakazi wa eneo la Mtakuja, waliuawa kati ya majira ya saa 2.30 na 2:45 usiku ambapo mauaji hayo yalipishana kwa dakika 15 kutoka tukio la kwanza hadi la pili.
Wafanyabiashara hao ambao wametambulika kwa majina ya Reinald Chuwa (32) na Amedeus Nasua (40), imeelezwa ni marafiki wakubwa na wote ni wafanyabiashara wa maduka ya nguo mtaa wa Mchikichini Kariakoo.
Wakisimulia tukio hilo, ndugu wa marehemu hao walisema kwa ujumla bado kuna utata wa jinsi matukio hayo yalivyotokea kwa sababu watu hao waliwapiga risasi katika maeneo yanayofanana huku wote wakiuawa wakati walipokuwa wakiingia ndani ya geti za nyumba zao.
Mdogo wa marehemu Chuwa, aliyejitambulisha kwa jina la Robert Chuwa (16), alisema kaka yake alifika nyumbani kwao majira ya saa 2 usiku akitoka kwenye biashara zake akitumia gari lake dogo. Alipofika getini alipiga honi ili afunguliwe geti kubwa.
Alisema, alipokwenda kumfungulia na kuliingiza ndani gari, ghafla alishtukia watu wakilifuata geti kwa haraka kitu ambacho kilimshutua Chuwa na kumuamuru haraka mdogo wake kwenda kulifunga geti kabla watu hao hawajafanikiwa kuingia ndani.
"Hata hivyo sikufanikiwa kulifunga kwani wale watu walinionyesha bunduki na hapo nilipata hofu nikakimbilia ndani kuwaambia ndugu zangu ili tukimbilie nje," alisema Robert.
Alisema, baada ya kuona hivyo, Chuwa naye alijaribu kukimbilia ndani, lakini alipigwa risasi na watu hao hatua chache kabla ya kuufikia mlango na kuanguka sebuleni.
"Tusikia sauti ya bunduki ikilia, kumbe wakati huo kaka alipigwa risasi kifuani na kuanguka chini sebuleni... wale watu walimburuza hadi chumbani huku damu nyingi wakiacha zikisambaa sakafuni," alisema.
Katika tukio hilo mke wa marehemiu, Matron Emannuel alikamatwa akiwa nje ya nyumba na baadae walimuingiza chumbani alikokuwa mumewe na kuamuru kutoa pesa walizokuwa nazo.
Majambazi hayo walifanikiwa kuchukua Sh. 300,000 pamoja na simu mbili za mkononi na baadae waliondoka kuelekea nyumbani kwa Amedeus Nasua umbali wa nusu kilomita kutoka eneo hilo.
Ndugu wa marehemu Nasua, Sylvester Masawe (23), ambaye wakati marehemu anauawa alikuwa akishuhudia, alisema kabla ya ndugu yake kupatwa na tukio hilo, wakiwa njiani kaka yake alipigiwa simu ikimuarifu kuwa rafiki yake amevamiwa na kupigwa risasi.
Alisema, mtu huyo alikuwa akizungumza naye hadi walipofika nyumbani, ambapo mara walipofunguliwa geti na kuingia ndani, ghafla watu wanne waliingia na kulizunguka gari lao na kuwaamuru kufungua vioo vya madirisha.
"Mimi nilikua wa kwanza kufungua mlango, lakini kabla sijafungua wote nilishtukia nikitupwa nje na kukandamizwa chini kwa miguu na kisha mmoja wa majambazi mwenye silaha alimfuata kaka pale alipokaa na kuelekeza mtutu kwenye bega lake la kushoto na kumpiga risasi," alisema Masawe.
Baada ya kumpiga risasi, majambazi hayo walimpekua ndani ya mfuko wa suruali na kuchukua Sh. 350,000 na pesa zingine Sh. 205,000 walizichukua kutoka kwa Masawe.
Alisema, baada ya kufanya mauaji hayo waliingia ndani na kumpiga mke wa marehemu, Cicilia Nasua jiwe la kichwani na kusababisha kupoteza fahamu kabla ya kupora simu, pete na hereni za dhahabu na baadae waliondoka eneo hilo.
Pamoja na hayo, wakazi wa eneo hilo wamelilalamikia Jeshi la polisi kwa kutochukua hatua za haraka kutokana na kushamiri kwa matukio hayo kila wakati.
Wameeleza matukio kama hayo wamekuwa wakikumbana nayo kila baada ya miezi mitatu na tayari wamesharipoti katika chombo hicho cha kulinda usalama wa raia lakini hakuna hatua inayochukuliwa na kusababisha maisha yao kuwa mashakani kuhofia kuvamiwa na majambazi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, alipotakiwa kuelezea tukio hilo ka njia ya simu, alisema yupo kwenye kikao cha kujadili suala hilo na kisha alizima simu yake ya mkononi.
"Tafadhali najua mnachotaka kuniuliza, nipo kwenye kikao cha kujadili suala hilo," alisema na kisha alikata simu.
Hata hivyo alipopigiwa simu kwa mara nyingine simu yake ilionyesha imezimwa.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI