Ajali yaua wawili Mpanda, Wananchi wachoma gari

Ajali yaua wawili Mpanda, Wananchi wachoma gari

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,093
Reaction score
7,112
Watu wawili wanadaiwa kufariki dunia baada ya kugongwa na gari walipokuwa wakisafiri kwa pikipiki, kufuatia gari hilo kupoteza mwelekeo, kuacha njia na kutumbukia mtaroni.

Wakizungumzia tukio hilo, mashuhuda wamesema lilitokea katika mtaa wa Mpanda Hotel, ambapo waliogongwa ni dereva wa bodaboda pamoja na abiria aliyekuwa amembeba, na wote walifariki dunia papo hapo.

Baada ya tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walijichukulia sheria mkononi na kulichoma moto gari hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Katavi, Lilian Wana, alisema walipokea taarifa ya ajali hiyo na kufika eneo la tukio ambapo walichukua miili ya watu hao wawili na kuipeleka hospitali.
 
Back
Top Bottom