Polisi Kuwasaka Waliompa JK Siku 100

Status
Not open for further replies.
Sina hakika kama kuna mtu humu Jf anaunga mkono Rais kutishwa kwa namna yoyote ile; lakini unaonaje kama zitafanyika jitihada za kuondoa mapungufu na kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano? Hivi kutakuwa na vitisho vyovyote kwa Rais? Kutakuwa na maandamano? Hebu tusaidiane njia ya kufika huko.

Njia ya kufika huko ni kuwepo na watu kama Mwanakijiji na wengineo sote kwa pamoja na vyama vya upinzani ambao kazi yetu ni kukosoa. Vile vile kama nilivyosema mwanzo kuandamana ni haki yetu ya msingi hata kama serikali ikitumia mabavu dunia ya sasa ni ya uwazi na kama serikali ikiwa inatumia nguvu basi wafadhili wapo watawazuia na ICC vile vile.

Kama serikali haitaki kutusikiliza watanzania dunia itatusikiliza na mfano mzuri ni Syria Bashir Al-Assad katumia mabavu mwisho amesalimu amri ya kuleta mabadiliko. Ndio demokrasia inavyokwenda kwa akili na maarifa ndugu zetu wazanzibari ni wazoefu katika kudai haki ya kidemokrasia labda tukajifunze kutoka kwao.
 
Kwa mujibu wa Bwana Vuai Nahodha. Anampango wa kuzibana kampuni za simu ziwataje wanaosambaza hizo meseji, laa watakula ban ya kufanya biznez. Yangu macho. Source ITV.

He hivi kumbe huu upuuzi umewaweka roho juu jamaa. Obama kwa siku anapata threats zaidi ya 100. Hebu wafanye kazi za kuendeleza nchi. Otherwise watachanganyikiwa katika dunia hii ya utandawazi. Kuanza kutishia kampuni za simu ni sawa na kushutumu kiwanda cha karatasi kwa kupokea barua ya kutukanwa na mpuuzi usiyemfahamu.

Wanachotakiwa kufanya ni kuwa underground na kuona credibility ya msg hizo. Hii dunia kuna watu vichaa wengi. Uki-engage nao wewe sasa utachanganyikiwa kabisaa.
 
Haya, kazi ni kwao!
 
Mdondoaji anajaribu ku emphasize kitu tangible hapa, kutisha Rais might not be a good/proper move, though binadamu tuko tofauti hasa linapkuja suala la kuhamanika na kupoteza matumaini.
 
Kwa suala hili la state kupewa siku 100,katika kila aspect ya jambo hili kuna haja ya serikali ya CCM kukaa chini na kutafuta kwanza sababu iliyopelekea ama watu, kikundi cha watu au mtu mmoja kuandika waraka kama huo ulio mzito.

Hivyo basi kwangu mimi kabla ya kutangaza hadharani kuwatafuta walitakiwa kutafuta kilichowafikisha hapo.ikumbukwe hata mtoa taarifa hiyo ametoa option ya wao kujirekebisha au la aondoke, sasa hapa kama ni wazo la mtu au watu kuna kitu ambacho wanaona hawajatendewa haki hivyo isije ikawa tuna mpata mmoja na kumbe jamii kubwa ya watanzania wanaathirika na jambo au mambo yale yale yaliyopelekea kuandikwa waraka huo. Na isitoshe huenda kuna watu au mtu ndani ya sysytem anaejua mambo yao yate ya kiintelejensia sidhani kama ni mpiga depe anaweza kuwa aware na mambo mazito ya kimkakati.wasiwasi wangu ni kwamba kama ni mtu au watu 4 hivi je tukiwapata hao ndo tutakuwa tumekomesha?hofu yangu yasije yakawa ni mawazo yanayojengeka kwa mitindo tofauti lakini ni ya ku-sabotage, tutakuwa tunahangaika na jambo hili kila wakati,Namshauri Nahodha wakati wanawatafuta hao watafute na kilichopeleka kuandikwa hivyo.

Kibaya zaidi ziliwahi kupatikana taarifa za viongozi wa chadema kutengenezewa kesi na kweli baada ya muda yamejitokeza hayo, hii inanipa picha ya kwamba kuna tatizo ndani ya mfumo wa kiusalama,ujue pamoja kila kazi ina maadili lakini ni kweli kila mtu ana roho, akili na ubinadamu sasa pale ambapo ndani yao wengine wanaona kuna ama uonevu au ukandamizaji wa haki za watu wengine ndipo hali ya ku-protest huanza na kupelekea jambo kuwa diclosed.

Nahodha kila la heri lakini chambua pia mawazo ya watu mabali mabali ili utoke na suluhu. Maana kama kweli Al shabab watakuwa washirika hapo i tatizo hao wako advanced kwenye uhalifu na mpaka leo mimi sijajua hasa wao wanatetea nini na ni rafiki wa nchi gani na dhahiri misismamo yao ni ya kiwendawazimu.

NINI CHANZO CHA TATIZO HILI LA WARAKA?
 
Leo kuna dada mwenye stationary yake maeneo ya sakina amekamatwa na yuko lockup kwa kukutwa na waraka wa lema na ule wa wanajeshi ambao aliletewa na wateja wake ili awatolee 4tocopy.
 
He hivi kumbe huu upuuzi umewaweka roho juu jamaa. Obama kwa siku anapata threats zaidi ya 100. Hebu wafanye kazi za kuendeleza nchi. Otherwise watachanganyikiwa katika dunia hii ya utandawazi. Kuanza kutishia kampuni za simu ni sawa na kushutumu kiwanda cha karatasi kwa kupokea barua ya kutukanwa na mpuuzi usiyemfahamu.

Wanachotakiwa kufanya ni kuwa underground na kuona credibility ya msg hizo. Hii dunia kuna watu vichaa wengi. Uki-engage nao wewe sasa utachanganyikiwa kabisaa.

umenena mkuu
 
Njia ya kufika huko ni kuwepo na watu kama Mwanakijiji na wengineo sote kwa pamoja na vyama vya upinzani ambao kazi yetu ni kukosoa. Vile vile kama nilivyosema mwanzo kuandamana ni haki yetu ya msingi hata kama serikali ikitumia mabavu dunia ya sasa ni ya uwazi na kama serikali ikiwa inatumia nguvu basi wafadhili wapo watawazuia na ICC vile vile.

Kama serikali haitaki kutusikiliza watanzania dunia itatusikiliza na mfano mzuri ni Syria Bashir Al-Assad katumia mabavu mwisho amesalimu amri ya kuleta mabadiliko. Ndio demokrasia inavyokwenda kwa akili na maarifa ndugu zetu wazanzibari ni wazoefu katika kudai haki ya kidemokrasia labda tukajifunze kutoka kwao.
Hivi unajuwa Bashar kauwa wangapi?

Kwahiyo ina maana hadi dunia ituskilize kama ilivyotokea Syria na ccm nao wauwe wananchi?
 
leo kuna dada mwenye stationary yake maeneo ya sakina amekamatwa na yuko lockup kwa kukutwa na waraka wa lema na ule wa wanajeshi ambao aliletewa na wateja wake ili awatolee 4tocopy.

kazi kweli kweli kama watu wanaoishi mwisho wa dunia kama alaska wanao huo waraka wanadhani kwa kumkamata huyo dada ndiyo watapata suluhisho? Yawezekana kuvuja kwa hizo siri kama zile za akina balali zimeiweka serakali ktk wakati mgumu hata hivyo katika dunia ya utandawazi hawawezi kuzuia hilo, wanatakiwa waende kwenye vioo wajiangalie mara mbili.
 
Hivi unajuwa Bashar kauwa wangapi?

Kwahiyo ina maana hadi dunia ituskilize kama ilivyotokea Syria na ccm nao wauwe wananchi?

Mushi,

Bashar kauwa wengi lakini umesikia wamempindua? Mapinduzi ya Tunisia yalianzaje si baada ya maandamano ya muda mrefu kudai haki yao? Egypt wananchi wameandamana hadi Mubarak ameondoka (wamisri zaidi ya 300 wameuwawa according to UN Human Rights watch). Libya wamempindua rais but watu wamesahau maandamano ya walibya kule Benghazi yaliyodumu muda mrefu. Hadi ilipofikia wakati serikali za kimataifa zilipokuja kuintervene wananchi wa libya waliandama muda mrefu na wengi waliuwawa.

Tusiende mbali tuna Zanzibar hapo mwaka 2001 wameuwawa watu 21 katika maandamano. Wengine waliuwawa Pemba idadi yao inasemekana wanafikia zaidi ya mia ingawa hakuna taarifa kamili. But leo wazanzibari wanaenjoy mabadiliko ya katiba na umoja na mshikamano.

Daini haki yenu kwanza kwa mujibu wa sheria za nchi. Kuvunja sheria is not an excuse to demand haki yenu.
 
By kokboy we unaogopa kufa, kwa TZ sasa ni bora kuukumiwa kunyongwa kuliko kuishi kwenye haya madudu

wacha mchezo na kifo wewe. waisraeli wanajiita taifa teule la mungu na bado wanaogopa kufa itajakuwa wewe? kifo ki sikie tuu kwa mwenzako.. mi napita tuu hapa

Mwenzetu ulishawahi kufa?
 
Uhuru wa kuongea una mipaka yake japo kuwa hao waliotishia wana madai ya msingi lakini ifahamike walichotaka kukifanya ni uhaini na kosa lake ni kifungo cha maisha au kuhukumiwa kunyongwa last time I check. Section 39 and Section 40 of the penal code ya Tanzania stipulates that treason is punishable by death penalty.

Vile vile misprision of treason (someone who knows there are some activities of treason) is punishable by life imprisonment.

Kuweni waangalifu jamani na sheria za nchi sio mnakurupuka.

Tukumbuke kuwa na makampuni ya simu yanawajibu wakulinda wateja wao "protect customer privacy" na wao wakienda kinyume na sheria hiyo basi mtu unawashtaki; unahakikisha ukipata msukosuko (wekwa ndani) familia yako nayo inafidiwa na kampuni ya simu. Ni lazima hizi kampuni za simu ziheshimu makubaliano yao na wateja.
 
My brother/sister you are lying sheria inasema hivi:-

customer privacy can be repudiated when it is a matter of judiciary request, a matter of national interest or protecting the society. Makampuni ya simu hayawezi kuzuia kitu kikishakuwa a matter of national interest. Wanakutosa wazi wazi na hawana liability yeyote kwa kufanya hivyo kwani wametekeleza wajibu wao kisheria.

Misukosuko utakayoipata ni matatizo umeyatafuta mwenyewe. Kuwa mwangalifu tu.
 
Kwa mujibu wa Bwana Vuai Nahodha. Anampango wa kuzibana kampuni za simu ziwataje wanaosambaza hizo meseji, laa watakula ban ya kufanya biznez. Yangu macho. Source ITV.
Haya ndiyo matokeo ya ile kazi ya kusajili namba za simu...
 
Guys kuna mtu mwenye hiyo messeg maana wengine hatujaiona kabisa....
 
Haaaaaa kumbe waheshimiwa wanapitiaga JF nimemuona Nahodha anasema wao wametumwa wawatafute hao watu wanaosambaza ujumbe,makampuni yamemgomea kumpa details kwa ajili ya kulinda mteja na kutopoteza wateja wao...
Mbona walitoa details za Mchange na M-pesa alizotuma kwa wajumbe?
 
Afadhali hao ambao wamesema walio kimya ni wengi. Kama ni ulinzi wamlinde kweli kweli huku nje hakufai na hana hata akili afanyeje. Hebu angali kamfano kadogo ka sakata la jairo. Kama ruhanjo anasema ni kawaida kufanya alivofanya jairo alivyofanya ina maana wateule wa rais wanafanya kazi wa kuambiwa mambo tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom