Polisi Kuwasaka Waliompa JK Siku 100

Status
Not open for further replies.
Ngoja tuone kama watafanikiwa, kumbe wameshaona ni noma na inaweza ikawa kweli. Binafsi naona ni vigumu sana kwani huwezi kupigana na "IDEOLOGY" ambayo ipo vichwani mwa watu. ikumbukwe kuwa kama wanavyo sema wametapakaa sehemu mbalimbali hadi ikulu hii itakuwa ngumu sana. Wanaogopa yale ya EPA.

Ikulu tamu asikuambie mtu, lakini swali dogo tu Nahodha alitakiwa alijibu kabla ya kutoa hiyo ultimatum, je kuna ukweli wa madai yaliyotolewa? ikiwa ni kweli nini kifanyike au walikosea wapi mpaka hali hii ikafika ilipo? Kitakachofuatia hapa ni kama ile sinema ya kuuawa kwa Kabila. Huwezi kuamuru baadhi ya walinzi wako wauawe wakati jamaa zao bado wanakulinda wapi na wapi.
Wapuuzi hao.Polisi amkamate Mwanajeshi wapi na wapi?Wanajifurahisha tu.Na wakiwakamata TUTAWAKOMBOA,wasituletee vitisho vya ki **** hapa.Tutaanza na yeye NAHODHA.
 
ngoja wahangaike, hii ndyo fursa ya pekee kujua wanachokipanga na namna kujipanga namna ya kuwakwepa na kutekeleza huu mpango adhumu wa kuikomboa nchi.
 
soma thread yangu vizuri.

Sijakuambia wewe nimesema kwa yeyote hata anayesoma hapa JF ni kuwa makini na unayoyafanya kwani hii inaitwa World Wide Web na kwa vyovyote their is source of an information. Ni kuwa makini na utumiaji wako wa internet.
 
Ha ha ha haaa! Kumbe waoga mko wengi eeeh?

Ukisoma kwa makini ujumbe ule utagundua kwamba baadhi ya waliotoa taarifa au pengine pia ni wahusika wakuu ni close associates wa mkulu au wa aides wa mkulu (inaelekea wanajua wanahoji nini). Yaliyohojiwa kama hayajakuathiri wewe directly yatawaathiri nduguzo. Sheria zipo ili ziwe tested!

Usiabudu sana sheria, ziheshimu ukiweza; ukiona hutendewi haki put them to test.

Sheria zimewekwa ili tupate kuwa watu wastaarabu. Kutojua sheria au kuvunja sheria ni kosa na haitetewi na madai ya kudai haki yako ya msingi. Hao wanaojiita sijui nani walitakiwa kufahamu misingi ya sheria inasemaje na sio kukurupuka.

Mkuu umejuaje kama pengine baadhi yao ni close associates wa mkulu? au aides wa mkulu angalia ndugu misprison of treason carries a life imprisonment sentence.

Tujifunze kudai haki zetu kwa misingi ya sheria tulizozitunga kama hatuziheshimu basi kuna haja gani tukatunga sheria? Bora tuishi kama wanyama tu tukichinja na kupigana wenyewe kwa wenyewe. Lakini kama hii nchi ya kufuata sheria kuna umuhimu wa sheria za nchi ziheshimiwe.

Hatuzungumzii madai yao bali namna walivyopeleka ujumbe wao ni uhaini na wasubirie joto la jiwe wakipatikana shauri zenu sheria zimewekwa ili zilinde raia.
 
Ubarikiwe
 
Wewe ungekuwa sio muoga ungekuja na jina lako halisi usingejificha na ilo Kombo!..

Unaleta porojo wakati upo nyuma ya laptop jitokeze
 
Mdondoaji naona umetumwa humu ndani. Sheria zinazolinda raia tunaziheshimu. Zinazolinda vitambi vya watawala wabovu tutazivunja ili kufikia haki.
 
Wanawasaka kabla ya hizo siku mia kwisha ama zikishapita wanapowapotea?
 
Sheria zimewekwa ili tupate kuwa watu wastaarabu. Kutojua sheria au kuvunja sheria ni kosa na haitetewi na madai ya kudai haki yako ya msingi. Hao wanaojiita sijui nani walitakiwa kufahamu misingi ya sheria inasemaje na sio kukurupuka.

Mkuu umejuaje kama pengine baadhi yao ni close associates wa mkulu? au aides wa mkulu angalia ndugu misprison of treason carries a life imprisonment sentence.

Tujifunze kudai haki zetu kwa misingi ya sheria tulizozitunga kama hatuziheshimu basi kuna haja gani tukatunga sheria? Bora tuishi kama wanyama tu tukichinja na kupigana wenyewe kwa wenyewe. Lakini kama hii nchi ya kufuata sheria kuna umuhimu wa sheria za nchi ziheshimiwe.

Hatuzungumzii madai yao bali namna walivyopeleka ujumbe wao ni uhaini na wasubirie joto la jiwe wakipatikana shauri zenu sheria zimewekwa ili zilinde raia.

Sasa wape ushauri kuhusu wanavopaswa kuwaletea "nyie wakubwa" madai yao.

Samahani Mkuu, Uliusoma ule waraka kabla haujaondolewa humu Jf? Kama uliusoma kwa makini na kuuelewa bila shaka utaelewa kwa nini nimeuhusisha na watu wa karibu na mkulu.
 
Mdondoaji naona umetumwa humu ndani. Sheria zinazolinda raia tunaziheshimu. Zinazolinda vitambi vya watawala wabovu tutazivunja ili kufikia haki.

Hakuna mtu kutumwa bali tunaambiana ukweli acheni kudanganya umma. Sheria zipi zinalinda umma unazoziheshimu na zipi zinalinda watawala wabovu huziheshimu?

Unafikiri kumpindua rais kitu kidogo nyie watu angalieni mnayoyasema na sio mnasukumwa tu na nguvu fulani nyuma yenu. Mtalamba matapishi yenu shauri zenu.
 
Usalama wa Taifa na CCM kwa propaganda ndio wenyewe yaani wameandika waraka kuusambaza kwenye mitandao kudivert kasi ya majadiliano ya muswaada wa Katiba
Lakini kama ni kweli kwa nini kuwe na double standard wakati wa uchaguzi mbona zilisambazwa email na sms za kumtishia DR Slaa na wala serikali haikusimama kusema watawatafuta mpaka wa wapate
 
Sasa wape ushauri kuhusu wanavopaswa kuwaletea "nyie wakubwa" madai yao.

Samahani Mkuu, Uliusoma ule waraka kabla haujaondolewa humu Jf? Kama uliusoma kwa makini na kuuelewa bila shaka utaelewa kwa nini nimeuhusisha na watu wa karibu na mkulu.

Kombo,

Niliusoma ule waraka ingawa uliondolewa immediately baadae lakini niliusoma ujumbe mzima vizuri. Wanayoyadai yana msingi ila vp wanadai ndio wamekosa heshima na adabu. Unapomtishia rais kumpindua ni uhaini (treason) wameshindwa nini kuandamana kudai madai hayo?

Maandamano ya amani ni fundamental right of a human being leo hii unaona Syria President Al-Assad amesalimu amri kwa waandamanaji. Mubarak and Gadaffi have fallen kwa sababu ya maandamano. Watafuteni wanasheria wawashauri vp wafanye kufikisha ujumbe na sio kumtisha rais hapo siwaungi hata kidogo.
 
Kwa mujibu wa Bwana Vuai Nahodha. Anampango wa kuzibana kampuni za simu ziwataje wanaosambaza hizo meseji, laa watakula ban ya kufanya biznez. Yangu macho. Source ITV.

Wanajifanya wametoa uhuru mwingi wa ktuoa maoni wakati ndani ya miyo yao ni udikteta, ufalme.
 
Kombo,

Niliusoma ule waraka ingawa uliondolewa immediately baadae lakini niliusoma ujumbe mzima vizuri. Wanayoyadai yana msingi ila vp wanadai ndio wamekosa heshima na adabu. Unapomtishia rais kumpindua ni uhaini (treason) wameshindwa nini kuandamana kudai madai hayo?

Maandamano ya amani ni fundamental right of a human being leo hii unaona Syria President Al-Assad amesalimu amri kwa waandamanaji. Mubarak and Gadaffi have fallen kwa sababu ya maandamano. Watafuteni wanasheria wawashauri vp wafanye kufikisha ujumbe na sio kumtisha rais hapo siwaungi hata kidogo.

Sina hakika kama kuna mtu humu Jf anaunga mkono Rais kutishwa kwa namna yoyote ile; lakini unaonaje kama zitafanyika jitihada za kuondoa mapungufu na kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano? Hivi kutakuwa na vitisho vyovyote kwa Rais? Kutakuwa na maandamano? Hebu tusaidiane njia ya kufika huko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom