Polisi kuwapiga raia huu ujeuri wanautoa wapi? Naomba mwenye ushahidi wowote wa raia wa Tanzania kupambana na Polisi auweke hapa

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Tabia ya polisi wa Tanzania kuwatisha, kuwapiga na kuwaumiza wananchi wanaotumia haki yao ya kuhoji utendaji wa serikali inazidi kuota mizizi na kuibua maswali kuhusu wajibu wa polisi kwa raia wanaotuhumiwa kuvunja sheria.

Kwa hali isiyoeleweka Polisi wa Tanzania wameamua kutoheshimu uhuru wa mikusanyiko na uhuru wa mawazo kama ilivyooanishwa kwenye Katiba kama vile ni uvunjaji wa sheria na hivyo kujipa mamlaka ya kuwaadhibu watuhumiwa kwa vipigo.

Kauli za maafande wa polisi katika miaka ya karibuni imezidi kuwa ya kibabe na ya kiuonevu kiasi cha kutishia amani ya nchi kama wananchi wataamua kujibu mapigo kama invyotokea katika mataifa mengine ndani na nje ya Afrika.

Imekuwa kawaida polisi, ambao jukumu lao la msingi ni kuwalinda raia na mali zao, wamesikika wakitoa kauli za vitisho utadhani muda wote wako vitani na raia ambao kimsingi ndio waajiri wao kupitia serikali yao waliyoichagua wao.

Baadhi ya kauli hizo ni kama ifuatavyo...
  • Wanaopanga kuandamana kesho watakiona cha moto
  • Wakiandamana watapigwa kama mbwa koko.
  • Watu watakaoandamana kwa amani watapigwa hadi wachakae
Kwa kauli kama hizi, wananchi waelewe nini? Kwa nini vyombo ambavyo vinatakiwa kulaani kauli kama hizi viko kimya? Hii jeuri ya polisi mbona imeachwa kukomaa hadi polisi kuonekana wako juu ya sheria? Kwa nini serikali haikemei kauli kama hizi? Je ni serikali inawatuma na kuwaruhusu polisi kuwaumiza wananchi?

Katika ombi langu hapo juu, nimeomba mwenye ushahidi wowote wa raia wa nchi hii kujibu mapigo kama inavyotokea katika nchi nyingine auweke hapa. Binafsi sina, ila naona kila mara polisi wakitoa vipigo kwa raia wasio hata na fimbo.

Hawaishii kupiga tu watu wazima wanaume kwa wanawake, wamethubutu kuwapiga hadi vitoto wa shule na hakuna tamko lolote limewahi kutolewa na vyombo vyenye jukumu la kuhakikisha raia wanatendewa haki.

Watu wanapigwa kabla ya kukamatwa, wanapigwa baada ya kukamatwa, wanapigwa wakiwa mikononi mwa polisi tayari iwe ndani ya gari au kwenye vituo vya polisi kama vile jukumu la polisi kwa sasa ni kupiga, kuumiza na hata kuua.

Watu waliokamatwa wamefikishwa mahakamani wakiwa na majeraha makubwa hadi kutembea wanashindwa lakini sijawahi kuisikia hata Mahakama ikitaka kujua kilichotokea au hata kuhoji kwa nini mtuhumiwa anachechemea.

Wananchi wamekamatwa majumbani wakiwa na afya zao lakini baada ya muda mfupi kwenye kituo cha polisi, wanapelekwa mahakamani wamebebwa hawawezi kutembea. Je ni kitu gani kinawapata hawa raia kwenye vituo vya polisi?

Juzi nimemsikia IGP mwenyewe kwa kauli yake akiwatishia wananchi waliopanga kufika mahakamani kusikiliza kesi ya Mbowe aliyeshtakiwa kwa kosa la ugaidi kwamba wasithubutu la sivyo watakiona cha moto na serikali ya SSH kimyaa!

Na siku hiyo ikafika. Polisi walivyotanda utadhani wanaenda vitani. Kila aina ya silaha ilikuwepo kupambana na maadui waliopanga kuhudhuria kesi. Wakaona hata hiyo hiitoshi wakakumbuka mbinu ya makaburu ya kuwatumia mbwa!

Kweli tumefika huko! Na hata miezi sita haijafika tayari hatuna tofauti na makaburu wa Afrika Kusini miaka karibu sitini enzi za Nelson Mandela na wenzake walipofunguliwa kesi ya ugaidi na serikali ya kibaguzi ya wakati huo.

Je ikitokea wananchi wakachoka na uonevu, wakaamua potelea mbali, kama ni keba keba kama inavyotokea sehemu mbali mbali duniani, je kutakalika? Tumshukuru Mungu aliyetujaalia Watanzania uvumilivu lakini mpaka lini?
 
Jeuri wanapata kwa aliyewateua.
Sisi ni kunyonywa kwa TOZO tu.
Ushahidi tayari unao huo ambao uliuona kisutu na mbwa

2871893_IMG_20210806_092415_947.jpg
 
Hao polisi Wana mizuka ya kupiga raia hadi suruali na boksa zinachanika.
Utadhani wanalipwa milioni mia moja kwa mwezi.!!
 
Sote tunajua ukatili waliofanyiwa raia wa nchi hii na Polisi wakati wa awamu ya mwendakuzimu aliyesalimu amri kwa corona mwezi wa tatu. Hebu tazameni simulizi hii...

Part I



Part 2


Part 3


Hawa Waliomtendea hivi Elisha Mwanjala waliingia vipi Jeshi la Polisi?
Hiyo ilikuwa awamu ya tano na sasa tunashuhudia ya awamu ya sita.
 
Mkuu, nijibu mada yako kwa kifupi sana.

Hizi mbinu za polisi zimefikia mwisho, haziwezi tena kuzuia manbadiliko nchini mwetu.

Jambo zuri kabisa, ni kwamba tuliodhani uoga wa waTanzania kutopambana wanapoonewa ni udhaifu, ni wazi kwamba hata kama ilikuwa ni uoga, uoga huo utazaa matunda bora zaidi bila ya kuwaumiza wananchi wetu wala kupoteza maisha yao ili kupata mabadiliko wanayoyataka.

Kwani siku hizi unaona kuna mtu anayehaha sana na vitisho vinavyotolewa na polisi, si watu wanajinyamazia tu na kupuuza kama polisi ni wenda wazimu fulani wanaojipayukia mambo yasiyowasumbua wananchi. Lakini ni nani asiyejuwa kwamba mabadiliko yanaendelea katikati ya ujuha wote huu unaofanywa na polisi na hao wanaowatuma kuwatisha wananchi.

Hakuna mwananchi anayepoteza maisha yake, hata kama kuna watu wanaumizwa bila hata ya wao kujitetea, jambo ambalo ndilo polisi na wanaowatuma wanayataka sana yatokee ili wazidi kujichimbia kuwanyanyasa waTanzania, kutojibu mapigo huko kunazidi kuwadhoofisha sana wadhalilishaji.
Hii imekuwa ni mbinu muhimu sana, hata kama haikupangwa ifanyike hivi.
 
Tabia ya polisi wa Tanzania kuwatisha, kuwapiga na kuwaumiza wananchi wanaotumia haki yao ya kuhoji utendaji wa serikali inazidi kuota mizizi na kuibua maswali kuhusu wajibu wa polisi kwa raia wanaotuhumiwa kuvunja sheria...
Polisi ni majeshi ya wahuni jeshi la nchi Kama jwtz ndio la kuheshimu.
 
kila ubaya utalipwa


Hata makaburu hawakuwa hivi...hii ni zaidi ya ukichaa, shuhudia eti mazoezi ya kuwapa wananchi kipigo cha mbwa koko yakifanyika mtaani!



Nimetembea nchi nyingi ulimwenguni na sijawahi kuona wana usalama wakifanya mazeoezi kama haya mitaani lengo ikiwa ni kuwadhibiti wananchi kwa kudai katiba mpya!

Polisi huwa wanaitwa tu kama fujo inatokea na hapo ni kwamba wanaenda kutuliza hali.
 
Hata makaburu hawakuwa hivi...hii ni zaidi ya ukichaa, shuhudia eti mazoezi ya kuwapa wananchi kipigo cha mbwa koko yakifanyika mtaani!

View attachment 1889030

Nimetembea nchi nyingi ulimwenguni na sijawahi kuona wana usalama wakifanya mazeoezi kama haya mitaani lengo ikiwa ni kuwadhibiti wananchi kwa kudai katiba mpya!

Polisi huwa wanaitwa tu kama fujo inatokea na hapo ni kwamba wanaenda kutuliza hali.
Aibu kubwa sana
 
Hiyo tabia ya polisi kuwapiga raia imeota mizizi mpaka sasa wameshaona ni haki yao kuwapiga raia.

Hili linasababisha kila mara tusikie raia wamefia vituo vya polisi, na inakuwa rahisi kuamini vifo hivyo vimesababishwa na polisi kuwapiga raia kwasababu ya tabia zao mbovu walizozoea kutuonesha uraiani.
 


Raia lazima waheshimu dola. Ukijaribu kushindana na polisi utaumia kama huyu hapa.
 
Tabia ya polisi wa Tanzania kuwatisha, kuwapiga na kuwaumiza wananchi wanaotumia haki yao ya kuhoji utendaji wa serikali inazidi kuota mizizi na kuibua maswali kuhusu wajibu wa polisi kwa raia wanaotuhumiwa kuvunja sheria...
Mama kesha sema mikutano ni vurugu za kisiasa! Msimamo huu ndiyo unamfanya aukatae mchakato wa katiba akijua ikipatikana itamzuia kunyanyasa.
 
Inaonekana wazi hujui maana ya neno "Kuheshimu"; na pengine wewe huelewi kabisa maudhui ya mada hii hapa ni nini.

Ni watu kama nyinyi ndio mnaosababisha matatizo mengi wanayofanyiwa raia na hao unaowaita dola isiyoheshimu haki za watu.
Una hakika mimi sielewi? Jaribu tena kusoma OP na conclusion aliyofikia utajua maana ya nilichoandika. Video niliyoweka ni mwananchi naye aliyechoka uonevu wa polisi akaamua potelea mbali. Liwalo na liwe. Yalimtokea umeyaona.
 
Mama kesha sema mikutano ni vurugu za kisiasa! Msimamo huu ndiyo unamfanya aukatae mchakato wa katiba akijua ikipatikana itamzuia kunyanyasa.
Kwa jinsi anavyohangaika asipokuwa makini yatamshinda.
 
Back
Top Bottom