Polisi kitengo cha loss report Arusha hili limekaaje?

Hivi huwa kina kitengo cha loss report, au kitu hiki huwa kinafanywa na polisi yoyote anayehusika kama ilivyo katika kukamata wahalifu?
Sina hakika mkuu lkn nilipofika wao dawati lao liko nje ya kituo sasa sijajua ni kitengo maalum au kimekuwa combined na vitengo vya matukio mengine au vp
 
sema jambo la ajabu ambalo lipo na nahisi ni mwanya mkubwa wa rushwa ni kuombwa vitu ambavyo huna.. nitatoa mfano wa kilichonikuta mimi mpaka nikastaajabu..

nilipoteza bag ambalo ndani yake kulikuwa na simu pamoja na vitambulisho vingine ( leseni,kadi za bank,kura na uraia na cha kazi). mtandaoni nikajaza loss report kama zilivyohitajika kila kimoja hapo unaweka report yake maana unavifatilia sehemu tofauti toafuti hivyo must uende na copy yake (loss report yake).

maajabu ni kuwa nilipokwenda pale kituo ........ na ni kikubwa mno kile kituo kina power zote..

1..kwa laini nikaombwa zile serial number,au vibati vile vya line (ukinunua line inakuwa kwa kiplastiki flani, (jiulize uratoa wapi laini ina almost 7years)

2. kwa vitambulisho vingine
....kadi za bank..nikaambiwa nikaombe barua za bank kuwa mepoteza ndio nirudi kituoni,
..uraia na leseni.. nikaambiwa nilete copy zake.. hivi mtu vitambulisho mepoteza copy zake natoa wapi kwa wakati huo???

.... na cha kazi ..nifate barua ya muajiri wangu nirud nayo..

kimazingira hayo je ni mepesi kwli?? ..pia kuna muda maalumu wa loss report.. japo online ni muda wote kuverify ndio kwa muda maalumu ila bado changamoto
 
Sina hakika mkuu lkn nilipofika wao dawati lao liko nje ya kituo sasa sijajua ni kitengo maalum au kimekuwa combined na vitengo vya matukio mengine au vp
Inaweza ikawa ni special unit kwa ajili ya kitu kingine kabisa isispokuwa sasa hawawezi kuacha ktoa loss report kwa sabubu nayo pia ni mojawapo ya kazi zao. Polisi hawawezi kujitenga sehemu fulani kwa ajili ya kutoa loss report tu, lazima kuna kitu kingine kikubwa wanafanya.
 
Loss report ipo online ni wewe tu tena ukitumia namba ya nida inapita hakuna haja ya kwenda polisi.
Online utapata loss report kwa mali zote isipokuwa simu ya mkononi, hii haitoki pale, unalipa lakini haitoi ripoti.

Nafikiri ndio mpaka uende kituoni na barua ya mtandao wa simu kama alivyoeleza mdau humu
 
Wewe ndiyo unamatatizo. Siku hizi loss report inapatikana online na huna sababu ya kwenda kuomba wakupe loss report.

Infact wewe ndiyo ulitakiwa uende na loss report central maana ungeweza kuioatabhata mtaani kwa kufuta procedure zao mtandaoni. Pale central lazima wangekuzungusha maana nao ninwanadamu na huu mfumo umewekwa ili watu wasiende pale. Kitenda cha kwenda pale ni kuwasababisha hata wawaombe rushwa kwa kitu amacho hata kwa kuazima simu ya jamaa yako ungefanumikisha mwenyewe.
Line za sim, wallet na mali nyingine sawa utapata loss report bila kwenda polisi, lakini ikiwa iliyopotea ni simu ya mkononi, loss report yake huipati online aisee inakataa
 
sio kweli haipiti ni mpaka uende polisi baada ya kulipia ile control number kule ukimaliza ndio utaweza kuiona online na kuidownload ..
Acha uongo wewe, kama wewe ulienda polisi ni uzembe wako mi nilitoa bila kutimba polisi
 
Acha uongo wewe, kama wewe ulienda polisi ni uzembe wako mi nilitoa bila kutimba polisi
Loss report ya kupotea kwa simu? Yaani ulijaza IMEI na ukapata loss report online moja kwa moja bila kwenda polisi?
 
Saizi kila kitu online, haina haja kwenda police, kwaajili ya loss report kuna watu wapo karibu na vituo vya Police wamepata fursa, wanakujazia online 2500,nimewaona hapo Msimbazi kkoo karibu na kituo ,wanawasaidia wale wenye vitochi na wasiojua kutumia computer
 
Saizi kila kitu online, haina haja kwenda police, kwaajili ya loss report kuna watu wapo karibu na vituo vya Police wamepata fursa, wanakujazia online 2500,nimewaona hapo Msimbazi kkoo karibu na kituo ,wanawasaidia wale wenye vitochi na wasiojua kutumia computer
Inategemea na mali iliyopotea mkuu
 
Loss report ipo online ni wewe tu tena ukitumia namba ya nida inapita hakuna haja ya kwenda polisi.
Ndiyo
Unainstall huduma ya malipo ya serikalu kwenye simu yako GEPG then unaomba loss report unalipua Tsh 500 kupitia mpesa au tpesa au benki, unaiprint then peleka kwa mtandao husika wa simu.
Polisi wanakazi nyingi jamani tuwahurumie.
 
Acha uongo wewe, kama wewe ulienda polisi ni uzembe wako mi nilitoa bila kutimba polisi
Kwenda polisi sioni kama ni uzembe mkuu kumeharibika sana unaweza ukaibiwa line asubuhi ikaenda kupiga tukio huna hili wala lile unashangaa pingu papu!..mbaya zaidi hujareport hapo ndio utajua kwnn Makufuli aliitwa pombe....hata ukija kutoka ushapoteza muda na fedha juu...VP kama ulireport? Msala unakuwa mwepesi sio uzembe hata kidogo.
 
Polisi lazima uende ili waithibitishe na wakuruhusu ku print.

Ila unaanza kufanya online.
Kama ni lazima kwenda polisi haina msaada mkubwa. Vituo vya polisi kuna uzembe mwingi. Hata karatasi za kuandika taarifa unapewa moja unaambiwa ukatoe nakala kumi.
 
Huko Polisi mambo mengi wanaanzisha siyo kwasababu ya kusaidia wananchi ila ni kutengeneza ulaji kwa polisi, jiulize kwanini simu zinaibiwa kila siku hazikamatwi na kitengo cha cybercrime kipo? Wanafanya kazi gani?

Kule Morogoro askari mmoja alianza kumtaka binti kimapenzi baada ya kumwomba amsaidie kutrack simu yake, binti alivyoona yamekuwa hayo aka surrender simu

Kuna mtu alisema simu zinazoibiwa askari wanazifuatilia wanazichukua wao
Cyber crime utafutaji simu ni dili zuri sana kwao. Huzifuatilia simu na pindi wakizipata humbandika mtu kesi ya mauaji. Kujinasua hapo ni mamlioni ya shilingi. Mpotezaji hudaiwa, anaepatikana nayo ni balaa.
 
tatizo vipengele vilivyowekwa ni vigumu inakulazimu utoe rushwa kama unavyojua ukienda polisi utazungushwa,kumbe watu wanataka ulaji
 
Back
Top Bottom