KITAULO
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 1,926
- 2,778
Wadau,
Jana asubuhi nikiwa njiani kwenye mwendo kasi nikiwa nakwenda kwenye mihangaiko yangu ya kila siku vijana wa mjini (wezi wa mifukoni) walinikwapulia simu yangu na vijisenti kiasi kadhaa. Nilistuka baada ya kusikia kijana wa pemebeni yangu alipokuwa analalama amekwapuliwa simu yake, na mimi kwa mstuko nikaanza kujipiga sachi ndipo nilipogundua na mimi ni muhanga pia.
Nilikwenda kwenye ofisi za mitandao yangu ya simu kuzifunga laini zangu kama ilivyo ada ili kuepuka matumizi mabaya wa wale mafedhuli walioniibia.
Changamoto ilianza pale nilipotakiwa kufuatilia loss report ili waweze kunirudishia line zangu (ofisi za haya makampuni zipo ndani ya jengo la J-MALL-Posta). Aisee hapo ndipo nilipoanza kuona namna gani kuna shida. Nilielekezwa kwenda kwenye stationary moja ya jirani ndani ya jengo hilohilo, nilipofika kwenye ile stationary kuulizia utaratibu na gharama, hapo niliambiwa gharama ni 4500/= kwa kila line, nikabaki na maswali mengi inakuwaje gharama inakuwa kubwa hivyo.
Nikaona hata hela imekuwa ngumu mno ngoja nisogee pale Police Central. Nikapewa maelekezo na Afisa mmoja pale nje, ila akaniambia zunguka kwa mbele kuna watu watakusaidia hapo nje. Kufika kwa wale vijana naambiwa gharama kwa line ni shilingi 3000/=
Kwa mimi niliyekuwa nimepoteza line zangu tatu gharama ilikuwa ina range kwenye 13500-10500
Hivi ni kweli tumefikia huku…na katika gharama zote serikali kupitia jeshi lapolisi linaingiza shilling 500/= kwa kila line hela iliyobaki inaishia kwenye mifuko ya watu wachache.
Wito wangu kwa jeshi la polisi naomba waliaangalie hili. Siyo haki kuwaumiza wanchi kwa maslahi binafsi ya watu wachache. Inakuwaje serikali inaingiza 500/= wakati mtu binafsi anajizolea kati ya 2500-4000/=?