Polisi: Benki bongo zimeajiri majambazi

Polisi: Benki bongo zimeajiri majambazi

Kuna ukweli mwingi katika hili lakini pia baadhi ya police pia ni washirika wakuu wa majambazi na ujambazi


Ndiyo na shangaa hakulisemea hilo!
Hata wateja nao wanaopiga foleni ndani ya Benki nao ni sehemu ya tatizo! .
Lakini siku hizi kwa uwapo wa TCRA na matumizi ya Simu kama kweli Polisi ina Wapelelezi makini na waaminifu ushiriki wa Wafanyakazi wa Benki au Wateja ndani ya Benki kuwasiliana na Majambazi kufanyia kazi ni rahisi.

Kuondokana na Ujambazi Kitengo cha Upelelezi cha Polisi kinatakiwa kifanyiwe Marekebisho makubwa ili kuleta Ufanisi.

Kuna haja Idara hii iwe kwenye Makundi /Grade-kupitia hizi grade Mishahara yao uwe unaendana na hadhi na mazingira ya Makundi hayo.Hili litasaidia kupima ufanisi na kuhakikisha Uchunguzi na ukusanyaji wa Vielelezo na ufanikishaji wa Mtuhumiwa kuhukumiwa-kupitia mafanikio hayo ndiyo kutako msaidia askari kupanda vyeo na Mishahara yenyewe.
Lakini pia kuwe na kitengo itakayojumuisha Polisi,Usalama wa Taifa ,Magereza na JTWZ ya kufanya Ukaguzi ndani ya Operation ya Kitengo hicho-labda baada ya muda tutaweza kufika mahali tukajipongeza wenyewe kwa kazi nzuri

https://www.google.com/url?sa=t&rct...mmary/&usg=AFQjCNHL2L2_RWlXkd0vHBK-nphlmJfEfA
Classifying Crimes - Murder, Felony, Misdemeanor ...

  • Murder 1 – Death or life in prison
  • Murder 2 – Life
  • Felony 1 – More than 10 years
  • Felony 2 – Not more than 10 years
  • Felony 3 – Not more than 7 years
  • Misdemeanor 1 – Not more than 5 years
  • Misdemeanor 2 – Not more than 2 years
  • Misdemeanor 3 – Not more than 1 years
  • Summary – Not more than 90 days
 
Iweje wanaouwawa wawe ni wanaotoa tu, sio wanaopeleka? kuna cku watu wa mabenk walikuwa wanajitetea ooh wateja wenyew wanajitangaza lkn kwa hii kaul inabid wajitathmin, na ndio maana inwezekana lazima wanawaua ili kuondoa ushahidi manake kila dili unackia mtu kauwawa wakat sio rahisi mtu kukatalia pesa na ameshaona jambaz lenye silaha. Manake wanawaua ili wasihojiwe kuonesha taarifa zili leak wapi, marehemu kama wangekuwepo lazima wangejua tatizo liko wapi.
 
basi kama tatizo ni hilo ipo haja ya kufatilia mawasiliano ya wafanyakazi wa benki zote yawe recorded ili tujue zaidi,hilo halina ubishi wizi mwingi unaotoka bank ni mchongo toka ndani kabisa ya wafanyakazi wa bank wenyewe
 
Ni Afisa gani wa polisi aliepandishwa cheo hasa kanda maalumu hakuwahi kusema"majambazi wote waanze kufunga virago"na hawakufunga virago? Polisi nao wanasiasa tu.
 
Polisi kazi imewashinda. Inakuaje wanashindwa kufuatilia mawasiliano ya hao wafanyakazi wa mabenki tuhumiwa ili kupata ukweli? Wasijitoe kwenye hii dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao. Excuse is a lie. Polisi wakitimiza wajibu wao hao wafanyakazi wa benki wanaotuhumiwa ni rahisi kuwashika.
 
Ukishazipata hela baada ya kuvuja jasho la damu....pia mashaka yanaanza jinsi ya kuitunza...

Ukisema upeleke benki ndio majanga kama hayo...

Ukisema uweke kwenye kibubu,kikijaa wanakihamisha....

Basi hakuna jinsi zaidi kuzichimbia ardhini kama tulivyokuwa tunafanya zamani...maana haya ni majanga juu ya majanga....
 
Kuna ukweli mwingi katika hili lakini pia baadhi ya police pia ni washirika wakuu wa majambazi na ujambazi
Kama una majina au taarifa zozote zitakazosaidia kuwabaini hao askari wanaojihusisha na ujambazi au uhalifu mwingine wowote yafikishe kwa IJP moja kwa moja usiishie kuandika hapa JF tu.
 
Kuna siku niliingia NMB Bank ku-draw kiasi cha pesa,wana kijitabia cha ajabu maana nilikuwa nataka mill4.5 tu nikapewa 5,000/= mil2,10,000/=mill1,,2,000/=mill1 na 1,000/= laki5 nikamwambia muhudumu kaka naomba nipe angalao 3mill tatu 10,000/= hiyo nyengine 5,000/= coz sina bag la kubebea na niko pekeangu kubeba hizo fedha itakuwa hatari kwa maisha yangu(maana nilizitia kwenye ile mifuko yao ya khaki ikaonekana kama nimebeba 20mill)akanijibu ndiyo sheria yetu inavyosema..na hii ilikuwa k/koo tawi lao lililopo mtaa wa Congo,kwa anaepajua jiulize unatokaje pale umeshika jifuko limetuna watu wasikuone wakakudhuru kumbe mna mill4.5 tu,sometimes hata kama hawatoi taarifa kwa majambazi ila jinsi wanavyotoa pesa nayo inahusika sisi raia kudhurika.
 
Nimecheka sana, hapo nani anawapa taarifa kwamba kibubu kimejaa?
Najua basi mkuu....ni kama vile kuna mtu anakagua maana kikiwa chepesi wala hana shughuli nacho......
Katika vibubu nilivyoweka nimefanikiwa kuvunja vibubu vinne tu....vilivyobakia wamechukua wawekezaji....
 
benki si kuna camera. waangalie wafanyakazi wanao wasiliana na simu kipindi mteja aliyeibiwa ametoka au yupo anachukua pesa.
 
Najua basi mkuu....ni kama vile kuna mtu anakagua maana kikiwa chepesi wala hana shughuli nacho......
Katika vibubu nilivyoweka nimefanikiwa kuvunja vibubu vinne tu....vilivyobakia wamechukua wawekezaji....

Kaka leo umenifurahisha sana (wawekezaji)....
Ndio maana tunashauriwa kutoa sadaka na kuwasaidia wenye uhitaji, hapo tutakua tumejihifadhia mali zetu kwenye sehem salama kabisa.
 
benki si kuna camera. waangalie wafanyakazi wanao wasiliana na simu kipindi mteja aliyeibiwa ametoka au yupo anachukua pesa.
Mkuu kama muhusika ni mfanyakazi wa ndani ya benki naamini anajua vizuri kuwa kuna kamera kwaiyo ni lazima kama ana nia ya kumchomesha mtu lazima atatafuta blind spot ili asionekane na kamera,
 
Mjinga sana ina ukipewa pesa hakuna anayeona

Unajua nafikiri kuna watu wanaliangalia hili jambo kijuujuu na kulalia upande mmoja wa wafanyakazi wa benki, kwa uzoefu wangu wa kufanya kazi benki kwa zaidi ya miaka mitano, nakubaliana na wewe kabisa kwamba jinsi wahudumu wanavyowahudumia wateja na kutoa pesa inaweza kabisa kuweka wazi kwa asiyehusika kiasi cha pesa anachopewa mteja. Pili, hata wale walinzi, ma askari wa ndani nao wanaweza kuwa watoa habari kwa majambazi/wahalifu juu ya mwenendo wa wateja. Tatu kuna wateja unakuta wamekaa tu ndani ya benki muda mrefu bila shughuli maalum, hao nao wanaweza kuwa chanzo kizuri cha habari kwa wahalifu. Kwa hiyo hayo yote yanawezekana, hapo bado sijaongelea ushirikiano kati ya polisi na majambazi, mtandao ni mpana kuliko tunavyofikiria.
 
Mnaweza kuwa mnawaonea wafanyakazi wa mabenki kwani wafanyakazi wa mabank muda mwingi wanakuwa wako busy kudili na wateja hasa tellers kwa maana akitoka mteja huyu anaingia huyu sasa muda wa kuwapigia simu wanatoa wapi?? na kuna camera kibao pale

Mimi ninachohisi and it maybe true ni kuwa kuna watu pale wanakaa benki wakipose kama wateja kumbe majambazi wakimuona mtu ana draw pesa na wao wanaondoka nae bila ya mteja aliye draw pesa kujua kama anafuatiliwa

Majambazi wengine wanakuwa kwa nje yule ambaye alikuwa ndani akitoka nae anawabonyeza wenzake kwa nje kuwa mtu mwenyewe ni huyu hapa na ana milioni kadhaa then baada ya hapo majambazi wale wanamfuatilia taratiibu mpaka wanamwibia.

Polisi wakitaka kumjua mtu anayepiga dili za hawa watu waangalie tu cctv camera za pale mlimani city watajua mengi sana yanayotendeka pale.

Kingine si sahihi polisi kuweka hadharani plan zao kwa maana majambazi hayo watabadilisha style sasa
 
Mabenki waweke system Za ku-deactivate cell phones kwa kila anayeingia Benki.

Wafanyakazi wa Benki wengi mishahara midogo na wanafanya kazi kwa Muda mrefu na bado nao wanataka kuishi kama hadhi ya Benki zao.
 
Ilitakiwa mteja akipigwa risasi basi hilo tawi la hiyo benki ambayo mteja ametoka linatakiwa kufungwa kwa muda kupisha uchunguzi wa polisi...

Na wafanyakazi wote wanatakiwa wapelekwe mahabusu hadi wamtaje aliyechonga hilo deal...

Inasikitisha mtu unakuwa mtumwa wa hela zakoo..
Kuwakamata ni simple tu...likitokea tukio tu, askari waangalie huyo mteja alichukua pesa benki ipi na alihudumiwa na nani hapo benki.

Baada ya hapo huyo banker achunguzwe mawasiliano yake ya simu ya siku hiyo...watajua tu.

MUHIMU: Ipigwe marufuku bankers kutumia simu zao za mkononi muda wa kazi, kada nyingi tu wanazuiwa.
 
Back
Top Bottom