Polisi: Benki bongo zimeajiri majambazi

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,016
2,194
DSC09011.jpg

Baadhi ya benki nchini zinadaiwa kuajiri baadhi ya wafanyakazi walio kwenye mtandao wa majambazi kutokana na wateja wengi kupigwa risasi na kufa wakitoka kuchukua pesa, uchunguzi wa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi Tanzania umebaini.

Hayo yalisemwa na baadhi ya askari hao wiki iliyopita walipozungumza na mwandishi wetu na kusema kwamba, waajiri wasipokuwa makini katika kuajiri watashangaa kuona wateja wao wanapigwa risasi na kuuawa kila kukicha.

“Haiwezekani kuwa wanaonyang’anywa fedha ni wale wanaotoka kuchukua benki kuliko wanaopeleka! Ina maana wezi wapo katika baadhi ya mabenki hivyo kunatakiwa kuwepo na umakini wakati wa kuwaajiri,” alisema askari mmoja kutoka makao makuu ya jeshi hilo, Dar akiomba hifadhi ya jina lake kwa vile yeye si msemaji.

Afande huyo aliendelea kusema kuwa, baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wa benki hizo wanapoona mteja anachukua fedha nyingi hufanya mawasiliano kwa njia ya simu kuwaeleza majambazi walio nje namna alivyovaa mteja huyo na kiasi cha fedha alichochukua.

Uchunguzi zaidi unaonesha kuwa, endapo hali hiyo haitadhibitiwa haraka huenda wananchi wakapatwa na hofu ya kuweka fedha zao benki kwa kuogopa kuporwa na kupigwa risasi wakienda kuzichukua.

Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Simon Sirro (pichani) ambapo alikiri kuwepo kwa baadhi ya wafanyakazi wenye mtandao na majambazi huku akisema jeshi lake limeweka mikakati kuhakikisha mtandao huo unasambaratishwa mara moja.

“Ni kweli kwamba, baadhi ya mabenki, si yote, yameajiri baadhi ya wafanyakazi, si wote wenye mtandao na majambazi. Kwa hiyo hata wao ni majambazi tu.

“Sasa tumejipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kukamata pikipiki zinazohusika katika uhalifu. Pia tumeamua kuweka makachero nje na ndani ya mabenki, wapo polisi wa miguu, pikip iki na magari. Nina uhakika tutawadhibiti,” alisema Kamanda Sirro.

Aliendelea kusema kuwa, majambazi waliopo katika Kanda ya Dar es Salaam waanze kufunga virago kwani bila kufanya hivyo wajue watakamatwa wote na mtandao wao kumalizika. Pia aliwataka wamiliki wa mabenki kuwa makini wakati wa kuajiri wafanyakazi ili kuwapata wenye sifa njema na kuweka imani kwa wateja wao.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova aliwahi kutamka kuwa, baadhi ya wafanyakazi wa ndani wa baadhi ya benki wana ushirikiano na majambazi. Akawatahadharisha wamiliki kuwa makini wakati wa kuajiri.


Chanzo: Gazeti la Uwazi
 
Last edited by a moderator:
Ilitakiwa mteja akipigwa risasi basi hilo tawi la hiyo benki ambayo mteja ametoka linatakiwa kufungwa kwa muda kupisha uchunguzi wa polisi...

Na wafanyakazi wote wanatakiwa wapelekwe mahabusu hadi wamtaje aliyechonga hilo deal...

Inasikitisha mtu unakuwa mtumwa wa hela zakoo..
 
Namna huduma inavyotolewa nayo inachangia tatizo,unakuta mteja anakaa muda mrefu halafu bank teller anamuita mteja kwa jina!(kimantiki kama kuna mtu mbaya,ataanza kumfuatilia huyo aliyeitwa kwa jina)
Namna nyingine ni kuwa na watu wanaokaa muda mrefu bila kupewa huduma,na wala hawaulizwi wanasubiri nini?!
Shida nyingine askari hawaangalii waingiao,wanaotoka wala kuhoji watu wanaokaa muda mrefu maeneo ya benki bila kupata huduma.
Vile vile unaweza kukuta askari anapiga stori au anasoma gazeti kwenye lindo!
 
Wanaouliwa ni wanaotoa pesa na sio wanaoleta pesa benki, A VERY BIG STATEMENT kuwa wafanyakazi wanavujisha habari kuwa kuna mzigo unatoka!
Hii statement ni ya kuitilia maanani sana.........Nimeshuhudia watu wengi wanakuja benki kuweka hela kwa mifuko ya rambo ila wanaopigwa risasi wengi ni wanaotoa hela hata milioni tatu tu!
 
Mnaweza kulaumu wafanyakazi bure kumbe kuna majambazi yanakuwa ndani ya benki yanatoa taarifa kwa wenzao nje yaani siku hizi benki watu wanatumia simu ndani mule.
 
The fact kwamba wanaoshambuliwa na kuporwa fedha ni wale wenye fedha nyingi ina maana kwamba either kuna information zinatoka ndani ya benki husika, au waanga wa matukio hayo walikuwa wanafuatiliwa na majambazi hao toka huko walipotoka i.e kwa mfano kama mtu ame declare anaenda benki kuchukua fedha nyingi siku na saa fulani na habari hii ikavuja na kuwafikia majambazi inakuwa imewarahisishia majambazi kazi.

Pia benki zinaweza kuwa na kitengo maalumu cha ku- deal na bulk cash ambapo wateja wanaohitaji huduma hii wanaweza kuhudumia haraka na pia kupatiwa escort kwa cost kidogo. Wahudumu wote wa kitengo hiki wabadilishwe kila baada ya masaa kadhaa na wakiwa kwenye huduma wasiwe na mawasilino yoyote ya simu au internet
 
Dawa yao ndogo sana hawa! Kuwasweka ndan benki nzima, watatajana wenyewe tu!
Haiingiii akilini mtu anaibiwaje hela akitoka kuchukua hela benki, kwann hao wezi wasiingie bank kuiba hela nyingi zaidi! Lazima wanajuana na wahudumu wa bank tu hakuna maelezo mbadala wa hayo
 
Namna huduma inavyotolewa nayo inachangia tatizo,unakuta mteja anakaa muda mrefu halafu bank teller anamuita mteja kwa jina!(kimantiki kama kuna mtu mbaya,ataanza kumfuatilia huyo aliyeitwa kwa jina)
Namna nyingine ni kuwa na watu wanaokaa muda mrefu bila kupewa huduma,na wala hawaulizwi wanasubiri nini?!
Shida nyingine askari hawaangalii waingiao,wanaotoka wala kuhoji watu wanaokaa muda mrefu maeneo ya benki bila kupata huduma.
Vile vile unaweza kukuta askari anapiga stori au anasoma gazeti kwenye lindo!
Upo sahihi
 
Back
Top Bottom