BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,383
- 8,132
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewafukuza kazi askari wake watatu kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo.
Aidha, limewatahadharisha wengine wenye tabia kama hizo kuziacha.
Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Septemba 15, 2022 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alipokuwa akizungumza na Mwananchi Digital ofisini kwake.
Kamanda Masejo amesema askari hao kwa nyakati tofauti wamebainika kwenda kinyume na maadili ya kazi ya jeshi la polisi ikiwemo kushindwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utendaji kazi.
"Hao askari tumewaondoa katika jeshi letu na tutaendelea kufuatilia na wengine watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na kiapo walichokikubali wakati wanajiunga na jeshi hilo,” amesema Kamanda Masejo
"Niwatake askari wengine wenye tabia kama hizo kama wanataka kuendelea na kazi ya kulitumikia jeshi la polisi basi wahakikishe wanafuata nidhamu na maadili ya kazi," amesema
Hata hivyo, Kamanda huyo amesema kwa sasa hawezi kuwaweka wazi waliofukuzwa kwani bado upelelezi unaendelea wa kuwachunguza askari wengine na wataendelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wale watakaobainika kuvunja sheria za nchi basi watawafikisha katika mikono husika.
Mwananchi
Pia soma: Vigogo wa Polisi Arusha wadaiwa kumpora mfanyabiashara milioni 3, watupwa lokapu