Polisi apigwa risasi na kufa

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,173
3,345
Wana JF polisi mmoja akiwa katika uniform amepigwa risasi hadi kufa maeneo ya Arusha chini ya mti karibu na stand ya magari ya kwenda Kisongo, Kwamrombo.

Ilikuja gari aina ya RA4 ikiwa imewasha taa kisha baadhi ya magari yakapisha wakijua labda ilikuwa na dharura, lakini walipofika alipokuwa askari huyo alipokaa basi alishuka jamaa mmoja na kumpiga risasi kwa bastola kisha kuingia ndani ya gari na kutokomea kusikojulikana.

Hadi napost thread hakuna habari za kukamatwa kwa jamaa hao ambao haikujulikana walikuwa majambazi au walikuwa na visasi nae marehemu.
 
Nazani huu ni mwanzo-mana wanatakiwa wawe makini sana na kazi zao na wanatakiwa waheshimu wananchi-la sivyo watu watakuwa wanafanyiwa hivi kila siku
 
Duh ... A-town kiboko ...watu wake comfo mia moja.... sijui

RIP corporal .... missing in action
 
mambo ya USA yanaanza sasa visa kwa visa,anayeuwa nae auwawe,wamezidi kutuuwa bila hatia,wakibanwa utasikia tulikuwa tunapambana na jambazi
mla kuku wa mwenzie miguu humgeukia


msema ukweli hapendwi daimaaaaa
 
Msiongee tu hilo suala halijafafanuliwa kwamba kapigwa kwa kisasi au ni majambazi mie huwa siwezi kucomment kitu nisichokifahamu unaweza kuamka kesho ukakuta ni ishu tofauti embu subirini kamanda wa polisi au sehemu husika walielezee tukio hilo limetokeaje!!!

Sio vizuri kuanza tu kusifia wakati hujui cause ya tatizo ni nini si ajabu huyo askari hakuwa na kosa kabisa!yawezekana ameonewa! Tusubiri taarifa za magazetini na redioni ila mtoa taarifa tunakushukutu sana kwa informations!
 
Kauli za akina Pindi zinachochea watu hamaki kutokana na upindishwaji wa sheria na ukweli wa matukio. Viongozi wanatakiwa kusoma ishara za nyakati vinginevyo wanazidi kukoroga mambo baadaya hakuna pa kushika miti yote itateleza
 
mhh watanzania tumefikia huku,pole yetu halafu majambazi yakituvamia tunataka msaada wa polis
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom