RIP. Ninalaani kwa nguvu zote mauji ya mtu asiye na hatia awe polisi, mtuhumiwa wa ujambazi, raia anayeandamana kwa amani. Kamwe watanzania tusianze kushabikia vifo vya raia wasio na hatia. Nina hakika kuwa polisi ni ndugu zetu, kama huna ndugu polisi basi utakuwa na jamaa au jirani mwenye ndugu polisi. Kamwe tuache mkondo wa sheria uchukue njia yake. Tusishabikie mauaji maana huwezi jua kuwa next target will be you, hizi chuki zinazoanza kujengeka miongoni hatuna budi kuziacha na kuwa wachamungu sana. Ila pia huu ni wakati wa vyombo vya usalama kuhakikisha tu haviwafurahishi watawala pekee bali pia wanajenga imani ya wananchi juu yao. Tumeona ya Egypt jinsi jeshi lilivyopata heshima kubwa toka kwa waandamani kisa tu hawakutumia vibaya nguvu za virafu vyao. KATIBA MPYA SULUHISHO LA KUJENGA AMANI YA KUDUMU TANZANIA.