Polisi apigwa mapanga, SMG yanyakuliwa

Polisi apigwa mapanga, SMG yanyakuliwa

Hapa naona ni UKAWA kwenda mbele na RAIA wema.
Maana post moja ya pili siasa.Uwezo wetu wa kufikiria ndio huo.

Polisi ataendelea kuwa polisi tu,na wao ni binaadam na timmings pia zipo.Mbona wanajeshi hata wale wenye weledi wa hali ya juu wa Marekani wanaingia kwenye mitego ya kitoto huko Iraq.

Polisi ataendelea kuwa polisi na heshima yake ipo pale pale.

Polisi ni kama mbwa wa boss. Akiambiwa kamata Huyo haraka keshaenda bila kujihoji. Tumechoka wacha wapigwe tu
 
Polisi sio legelege bana ni wauaji ucpime hao. Umesahau walivyomuua Daudi Mwangosi akiua wanapandishana veo

Wakati mwingine waapogombani wanawake (mapolisi wenzao) hawana utu. Zikiwapanda stimu wanaua utadhani anaua sisimizi
 
Sidhani kama kuna kitu cha ajabu hapo.Polisi imebaki jina tu,ni watu wa kuganga njaa na kuwaogopa waajiri wao.polisi mshahara duni,anaishi kwenye madebe,lakini hayuko tayari kudai maboresho ya maslahi yake.Matokeo yake ni kuomba rushwa kwa nguvu kama ilivyo sasa au kubambikiziwa kesi ili atoke.Kwa mara ya kwanza katika jamhuri yetu hii ya TZ sikuamini macho na masikio yangu siku moja nilipoingia JNIA kwa pikipiki nikadakwa na polisi kama saba hivi,kisa wameweka doria kwa kuwa pikipiki hata binafsi haziruhusiwi kuingia uwanja wa ndege!,Ubishi wangu uliisha kwa kuambiwa au niachane na pikipiki au niwakatie kitu ili waniachie,pesa waliotaka ni astronomical ila niliishia kuwaachia 20000,na bado wakaniruhusu kuingia uwanja huohuo ambao walidai hakuna pikipiki inayoruhusiwa kuingia.Cha kusikitisha ni kuwa walipokea pesa hiyo pamoja na kuwa na sare na vitendea kazi vya jeshi la polisi.Sihangai sana kusikia wamepigwa mapanga kwa kuwa hawako kikazi zaidi ya deals na deal yoyote ni maslahi,inageuka wakati wowote ule.
 
sikusikia ila nimesoma hotuba yake by skimming na hoja ya kiswahili nimeiona. Amemponda JK kuoenda kidhungu hata mahali pa kuongea lugha yetu adhim. amemsifia rais wa makonde kwa kuhutubia kwa lugha ya taifa lake bungen tz

Ningeshangaa sana kama mpinzani angemsifia Kikwete. Lakini hilo la upinzani kuponda hata mafanikio mbona tumelizowea. Na sisi tunapuyanga tu.
 
sasa utampendaje mtu asiyekupenda kwa sasa polisi wa kiafrika kubeba bunduki ni hatari kwa raia wema kuliko hata hao majambazi wanao wawinda mabepari tu siraha sasa zimekua za kuwaulia wapigania demokrasia tu? i hate them policeccm
 
Imetokea jana kama saa mbili usiku maeneo ya yombo lelini,nimepita mida ya saa nne na nusu usiku nikakuta habari hiyo na landcruser la police limepaki,Leo asubuhi wakati natoka maeneo hayo polisi kibao wapo eneo la tukio.

Mwenye habari zaidi atujuze hasa hali ya polisi aliyepigwa panga na kunyang'anywa smg!!

''wapigwe tu, maana hakuna namna nyingine'' kayanza
 
Kuna haja ya kurudisha Wakurya jeshini kwa wingi, hawa wazaramu na wakwere kazi imewashinda.
 
kuna watu hupenda kulalamika kwa niaba ya wengine a thing which leading to fallacy.

hebu izungumzie nafsi yako, lini polisi imekufanyia ubaya? kama hujafanyiwa baya na askar iweje uichukie? tumevurugwa na wanasiasa, ambao wao kuichukia polisi ni credit kwa wananchi.

pole sana soja, umeumia kazini maana ni rahisi kwa adui kukufanyia ambush kimya kimya lkn ni ngumu kukufanyia hujuma ukijua. pole sana

Wewe ndo unaingiza hili swala kwenye siasa za kutetea hawa polisi.Nimeshuhudia kwa macho yangu matendo yao mabovu tena hadharani hafu leo uje kusema siasa are you serious hayaja kukuta ndo mana unasema hivo. Labda nyie badala ya kusolve matatizo mnakimbilia kulaumu wanasiasa.
Kwahyo wewe ume komenti ulilotaka kwangu ndo nogwa imekua shida eti kulalamika on behalf. Msiambiwe ukweli nani hajui mambo ya fallacy sasa.
 
Polisi wakishindwa kupeleleza na kuwakamata wahusika nitashangaa sana hili ni tukio la kupangwa kwa 100%
 
Nyinyi vilaza hamna sababu ya kuwachukia polisi wetu hata siku moja wewe unaleta uchama wako kwenye mambo ya national security
Nadhani kosa lao kubwa ni kulinda chama badala ya kulinda raia na mali zao.
 
Polisi nchi hii wana changamoto nyingi mno makazi duni,mshahara hauridhishi lkn bado wanakumbatia CCM cjui wanapata nini aisee.
 
Mkuu pamoja na uozo uliokuwepo nchini mwetu kuhusu uendeshaji wa nchi haihusu kitu pale polisi wanapowambakizia kesi raia wasio na hatia tena kesi mbaya sana, wanapowadhulumu pesa zao halali, wanapowapiga na kuwatia vilema vya maisha na wakati mwingine hata kuwaua huku wakiwa hawana hatia yoyote (Mwangosi). Kuwa na viongozi DHAIFU walioshindwa kuiongoza nchi yetu isitumike kama ni kuhalalishwa kwa polisi kuwanyanyasa na kuwatesa hata kukatisha maisha ya Watanzania.

Sikatai unavyowachukia polisi, una sababu zako!

Ninachotaka mimi tusiishie kuwachukia polisi tu...twende mbele na kujiuliza ni nini kinasababisha haya? Tuichukie mifumo ya uendeshaji nchi, tuwachukie watunga sera maana ubovu wa watendaji wa huku chini ni matokeo ya ubovu wa sera na mifumo!
 
Mbona wanapigwaga vizuri tu polisi wako legelege sana wengine hadi wana bwebwa mgongoni unategemea nini?

Yaani huyo aliebebwa akiwa kwenye sare ya jeshi na kama kweli ni hapa Tanzania nategemea tayari awe alishafukuzwa kazi. Labda iwe ni mazoea yao kuendesha siasa jeshini kwani hata wale trafic police wa Kagera waliodiriki kutuma picha zao mitandaoni wakibusiana wakati wa kazi na kwenye sare za jeshi hilo walionywa tu na viongozi wao. Naamini kabisa huyu wa Yombo tena pale relini alikuwa kwenye ulevi akawahiwa. Haya ni mengi sana kwenye hili jeshi kwa askari wao kuingia sehemu za starehe na silaha ya serikali au pengine kutoroka hata lindo. Sehemu nyingine huaga wanaokosana nao maeneo ya starehe kuwa nisubirini niende nirudi na akirudi kweli anatinga na silaha ya moto. Nidhamu ilikuwepo miaka ileeee.
 
Nasema tuache siasa unashabikia polisi kuumizwa na bunduki kuchukuliwa alafu unajiita raia mwema! kivipi? Jiulize hiyo silaha italeta madhara kwa wangapi? usikoment ili uonekane na wewe humo, sipendi uhalifu,na napenda sana askari,pole kwa askar aliyeumia.
 
Back
Top Bottom