Polisi apigwa mapanga, SMG yanyakuliwa

Polisi apigwa mapanga, SMG yanyakuliwa

Mkuu pamoja na uozo uliokuwepo nchini mwetu kuhusu uendeshaji wa nchi haihusu kitu pale polisi wanapowambakizia kesi raia wasio na hatia tena kesi mbaya sana, wanapowadhulumu pesa zao halali, wanapowapiga na kuwatia vilema vya maisha na wakati mwingine hata kuwaua huku wakiwa hawana hatia yoyote (Mwangosi). Kuwa na viongozi DHAIFU walioshindwa kuiongoza nchi yetu isitumike kama ni kuhalalishwa kwa polisi kuwanyanyasa na kuwatesa hata kukatisha maisha ya Watanzania.

Yote hayo uliyoyaainisha yamechukuliwa hatua gani?

Yote hayo uliyoyaainisha yalisababishwa na nini?

Utaelewa kwa nini hatutakiwi kuchukia polisi au TRA au taasisi nyingine yeyote ya serikali inayotoa huduma mbovu kwa raia!
 
Matukio ya kuvamia askari wakiwa lindoni, vituo na vizuizi vya polisi nchini yameendelea kulitafuna Jeshi la Polisi na safari hii, Askari wa Kikosi cha Tazara, Jijini Dar es Salaam, ameporwa SMG na kujeruhiwa vibaya.

Tukio hilo lilitokea juzi usiku saa sita kwa watu wanaosadikiwa ni majambazi wakiwa na silaha za jadi kumvamia askari huyo akiwa kwenye lindo la Tazara na kupora silaha hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, watu wawili wakiwa na silaha za jadi, nyakati za saa sita usiku walivamia eneo hilo na kupora silaha hiyo na kutokomea nayo.

Taarifa hizo zinafafanua kuwa askari huyo alijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili na amelazwa hospitali kwa matibabu zaidi, ingawa jina lake halikutajwa wala hospitali aliyolazwa.

Kamanda wa Kikosi hicho, Kamanda Bieteo, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa hawezi kutoa ufafanuzi kwa simu bali kwa taarifa ya maandishi.

"Tukio lipo ni kweli wamemvamia askari akiwa lindoni kumjeruhi na kumpora silaha…siwezi kutoa ufafanuzi zaidi kwa simu, leo nitatoa taarifa kwa maandishi," alisema.

Alipotakiwa kueleza zaidi alijibu kwa mfupi: "Nitafute kesho (leo), nitaandaa taarifa ya maandishi, sipo tayari kueleza kwenye simu."

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (pichani), alipoulizwa, alithibitisha, lakini akamuelekeza mwandishi kuwasiliana na Kamanda Bieteo.

Januari 21, mwaka huu, usiku huko kituo cha Polisi Ikwiriri - Rufiji majambazi wakiwa na bunduki walivamia kituo cha Polisi na kuwaua askari wawili na kupora bunduki aina ya SMG 2, SAR 2, Anti Riot gun moja, Shotgun moja na risasi 60.

Machi 30, mwaka huu barabara ya Kilwa kwenye kizuizi cha Polisi eneo la Shule ya Sekondari St. Mathew Kongowe kata ya Vikindu Wilayani Mkuranga, majambazi wasiofahamika wakiwa na mapanga na silaha zingine za jadi walimuua askari mmoja kisha kupora bunduki moja aina ya SMG ikiwa na risasi 30.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alisema idadi ya matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi imeongezeka kutoka sita kwa mwaka 2014 hadi nane kwa mwaka 2015.

Alisema katika matukio hayo jumla ya askari saba waliuawa kwa mchanganuo kwenye mabano Chamazi (2), Mkuranga (2) na Ushirombo (3)

Bunduki zilizoporwa ni bunduki 22 na mchanganuo wake ni Chamazi (2), Mkuranga (1), Ushirombo (17) na Tanga (2).

CHANZO: NIPASHE
 
Yachukuliwe hatua na nani? Kwa mfano kesi ya Mwangosi nani alitakiwa achukue hatua? Muuaji polisi wachunguzi polisi unadhani kuna haki itatendeka hapo? Mpaka hii leo hatujui hatima ya mauaji ya Mwangosi. Yalisababishwa na jeshi la polisi ambalo rushwa, unyanyasaji umekithiri kupita kiasi na pia kujiona wao wako above the law wanaweza kufanya lolote lile na kwa kuwa wao ni polisi basi hawachukuliwi hatua. Ndiyo sababu kubwa leo hii polisi wanachukiwa sana na Raia walio wengi.

Yote hayo uliyoyaainisha yamechukuliwa hatua gani?

Yote hayo uliyoyaainisha yalisababishwa na nini?

Utaelewa kwa nini hatutakiwi kuchukia polisi au TRA au taasisi nyingine yeyote ya serikali inayotoa huduma mbovu kwa raia!
 
Yachukuliwe hatua na nani? Kwa mfano kesi ya Mwangosi nani alitakiwa achukue hatua? Muuaji polisi wachunguzi polisi unadhani kuna haki itatendeka hapo? Mpaka hii leo hatujui hatima ya mauaji ya Mwangosi. Yalisababishwa na jeshi la polisi ambalo rushwa, unyanyasaji umekithiri kupita kiasi na pia kujiona wao wako abave the law wanaweza kufanya lolote lile na kwa kuwa wao ni polisi basi hawachukuliwi hatua. Ndiyo sababu kubwa leo hii polisi wanachukiwa sana na Raia walio wengi.

Wanaopeleleza kesi marekani ni watu gani...au tusiende mbali, Kenya?
 
Mie naona unazunguka zunguka tu, ukweli utabaki kwamba polisi kumekithiri kwa unyanyasaji, rushwa, uhuni na wengine kushirikiana na majambazi ndio sababu leo hii wengi wa Watanzania wanawachukia sana polisi hata kufurahia pale polisi anapopigwa au kuuwawa. Hali hii inaweza kabisa kurekebishwa na uongozi wa polisi lakini hawafanyi hivyo labda wanasubiri mpaka mauaji ya polisi nchini yaongezeke kwa kiwango cha kutisha ndio waone umuhimu wa kukaa chini kupambana na uozo mkubwa ndani ya jeshi hilo.

Kuwachukia polisi kumetatua nini? Sikatai kuwachukia kama wamefanya kinyume na sheria au haki! Lakini, kiwango hiko cha chuki tungekielekeza kwa mifumo na watunga sera za usimamizi wa uongozi wa nchi/taasisi, chuki hizo zisingekuwepo!
 
Sasa wewe ulitaka pamoja na Watanzania kubambikiwa kesi, kunyanyaswa, kuporwa mali zao ikiwemo pesa na kuuwawa waendelee kuwapenda polisi!? Unadhani kibao kikigeuka na polisi kati ya watatu mpaka watano wakawa wanauwawa kila siku uongozi wa polisi hautakaa chini na kuangalia tatizo ni lipi mpaka polisi wauwawe kwa idadi kubwa hivyo!? Unadhani watanyoosha mikono juu na kusema system yote imeoza hivyo hatuna la kufanya ili kuangalia kwanini raia wanawauwa polisi kwa idadi kubwa kiasi hiki na nini kifanywe ili kuzuia mauaji hayo ya polisi!? Siku zote mkuki kwa nguruwe......

Uwe na weekend njema Mkuu Mentor

Kuwachukia polisi kumetatua nini? Sikatai kuwachukia kama wamefanya kinyume na sheria au haki! Lakini, kiwango hiko cha chuki tungekielekeza kwa mifumo na watunga sera za usimamizi wa uongozi wa nchi/taasisi, chuki hizo zisingekuwepo!
 
Mbona wanapigwaga vizuri tu polisi wako legelege sana wengine hadi wana bwebwa mgongoni unategemea nini?

Bado waliwe tigo maana matumbo makubwa utendaji mdogo wao rushwa tu ukipeleka kesi ya hela wanakunyenyekea kama wewe mkuu wao wa kazi....peleka kesi za kawaida sisizohusu ulaji utaona kila mtu anajifanya busy na kazi

Tumetembea mataifa mengi sana dunia wenzetu Wanakuwa na mapenzi na walinda raia wake yani polisi kwakuwa husaidia usalama lakini kwa huku kwetu sio kabisa yani ni wachache saaaana wanaowakubali polisi wetu kwa Kuwa nidhamu zao mbovu na rushwa inayonuka
 
Hakuna nchi polisi anapendwa.na haitakuja kutokea.unajua ni kwanini???

Sababu hamna Uhuru usio na mipaka,basis pale palipo na Uhuru mwingi kiasi gani kukiwa na mipaka tu polisi atahusika.ndio msimamizi Wa hizo limitation.

Hapendwi polisi sababu.

Ukibaka,atakubaka
Ukiiba,atakutaka urudishe.
Ukipiga mtu,atakupiga.
Ukiendesha vibaya,atakushika.
Ukiandamana,atakuzuia.

Sasa kama kuna nchi polisi wanaruhusu yote hayo,hiyo ndio nchi polisi wanapendwa kuliko zote.

Wewe jua wajibu wako,kuwachukia hakukusaidii zaidi ya kujiweka kwenye risk,maana unaweza kumtukana sababu unamchukia ukajaikuta una mimba yake unatakiwa umzalie.
 
Sambazeni upendo ***** , au mwataka waende likizo wote? Msipende kugeneralize mambo aisee!
 
Matukio ya kuvamia askari wakiwa lindoni, vituo na vizuizi vya polisi nchini yameendelea kulitafuna Jeshi la Polisi na safari hii, Askari wa Kikosi cha Tazara, Jijini Dar es Salaam, ameporwa SMG na kujeruhiwa vibaya.

Tukio hilo lilitokea juzi usiku saa sita kwa watu wanaosadikiwa ni majambazi wakiwa na silaha za jadi kumvamia askari huyo akiwa kwenye lindo la Tazara na kupora silaha hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, watu wawili wakiwa na silaha za jadi, nyakati za saa sita usiku walivamia eneo hilo na kupora silaha hiyo na kutokomea nayo.

Taarifa hizo zinafafanua kuwa askari huyo alijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili na amelazwa hospitali kwa matibabu zaidi, ingawa jina lake halikutajwa wala hospitali aliyolazwa.

Kamanda wa Kikosi hicho, Kamanda Bieteo, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa hawezi kutoa ufafanuzi kwa simu bali kwa taarifa ya maandishi.

“Tukio lipo ni kweli wamemvamia askari akiwa lindoni kumjeruhi na kumpora silaha…siwezi kutoa ufafanuzi zaidi kwa simu, leo nitatoa taarifa kwa maandishi,” alisema.

Alipotakiwa kueleza zaidi alijibu kwa mfupi: “Nitafute kesho (leo), nitaandaa taarifa ya maandishi, sipo tayari kueleza kwenye simu.”

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (pichani), alipoulizwa, alithibitisha, lakini akamuelekeza mwandishi kuwasiliana na Kamanda Bieteo.

Januari 21, mwaka huu, usiku huko kituo cha Polisi Ikwiriri - Rufiji majambazi wakiwa na bunduki walivamia kituo cha Polisi na kuwaua askari wawili na kupora bunduki aina ya SMG 2, SAR 2, Anti Riot gun moja, Shotgun moja na risasi 60.

Machi 30, mwaka huu barabara ya Kilwa kwenye kizuizi cha Polisi eneo la Shule ya Sekondari St. Mathew Kongowe kata ya Vikindu Wilayani Mkuranga, majambazi wasiofahamika wakiwa na mapanga na silaha zingine za jadi walimuua askari mmoja kisha kupora bunduki moja aina ya SMG ikiwa na risasi 30.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alisema idadi ya matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi imeongezeka kutoka sita kwa mwaka 2014 hadi nane kwa mwaka 2015.

Alisema katika matukio hayo jumla ya askari saba waliuawa kwa mchanganuo kwenye mabano Chamazi (2), Mkuranga (2) na Ushirombo (3)

Bunduki zilizoporwa ni bunduki 22 na mchanganuo wake ni Chamazi (2), Mkuranga (1), Ushirombo (17) na Tanga (2).

CHANZO: NIPASHE

Mmmmmh Hii ni hatari kubwa sana! waandishi wa habari ni vizuri kwenda eneo la tukio na kutafuta ukweli!!.Ilikuwa saa mbili usiku na hawakuwa lindoni ina maana wewe mwandishi hujamsikia masau bwire na wapo redio jana jioni!!.Badilikeni waandishi wa habari!.
Ilikuwa saa mbili usiku walienda na mwenzie b..r kupata chakula wakati wanaulizia chakula kukatokea ugomvi wa w......i polisi mmoja akaenda kuamlia wakageuka na kumchapa mapanga na kuondoka na smg full magazine,Huku mwenzake akiwa anaulizia msosi au kuangalia tu na askari huyo yupo mahabusu na aliyechapwa mapanga yupo temeke hospital-Source wapo radio by masau bwire!!
 
Kwenye kusaidia raia legelege na kwenye rushwa na kupiga RAIA wasio na silaha wako strong sana tu.Huo ndo ukweli hamna uongo hapo. Wangekua wanafanya kazi zao kwa haki wasinge kua wana chukiwa na kila RAIA.

Nani alikuambia wanachukiwa na RAIA? Wanachukiwa na ninyi wahalifu tu
 
Bavicha+ukawa ndo ambao huwachukia polisi 7b ya utukutu wao.
 
Bado waliwe tigo maana matumbo makubwa utendaji mdogo wao rushwa tu ukipeleka kesi ya hela wanakunyenyekea kama wewe mkuu wao wa kazi....peleka kesi za kawaida sisizohusu ulaji utaona kila mtu anajifanya busy na kazi

Tumetembea mataifa mengi sana dunia wenzetu Wanakuwa na mapenzi na walinda raia wake yani polisi kwakuwa husaidia usalama lakini kwa huku kwetu sio kabisa yani ni wachache saaaana wanaowakubali polisi wetu kwa Kuwa nidhamu zao mbovu na rushwa inayonuka

Zenj mbona wanaliwa.
 
Back
Top Bottom