Polisi apigwa mapanga, SMG yanyakuliwa

Polisi apigwa mapanga, SMG yanyakuliwa

WAPOMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2012
Posts
689
Reaction score
175
Imetokea jana kama saa mbili usiku maeneo ya yombo lelini,nimepita mida ya saa nne na nusu usiku nikakuta habari hiyo na landcruser la police limepaki,Leo asubuhi wakati natoka maeneo hayo polisi kibao wapo eneo la tukio.

Mwenye habari zaidi atujuze hasa hali ya polisi aliyepigwa panga na kunyang'anywa smg!!
 
Huyo atakuwa polisi feki, polisi mwenye mafunzo kamili unanyang'anywa SMG na anayekunyang'anya ana panga.
 
Huyo atakuwa polisi feki, polisi mwenye mafunzo kamili unanyang'anywa SMG na anayekunyang'anya ana panga.

Mbona wanapigwaga vizuri tu polisi wako legelege sana wengine hadi wana bwebwa mgongoni unategemea nini?
 
Attachments

  • 1432798957872.jpg
    1432798957872.jpg
    6.8 KB · Views: 2,745
Wewe unashabikia jambazi kumiliki silaha ??? Hujawaona wakiwa kazini ndio maana. Kumbuka Jambazi sio binadamu na wakizirusha kwenye umati wa watu hawataangalia kama wanakuua wewe au ndugu yako

Kweli aisee, na inaonekana wenaowachukia Polisi wengi wao ni CHA KUFIA NINI. Yaani hana cha kupoteza hata nchi ikipinduliwa leo. Wanatamani vita/machafuko/ujambazi labda watatokea huko.

Hadi muda huu naandika haya ni kwasababu kuna watu wanakesha kazini. Tusiangalie mapungufu tu, hata mafanikio ni muhimu kuyasema.
 
Lkn wakipigwa wao tunawaita legelege. Wakipiga tutasema wanatumia nguvu/ubabe. Nahisi kuaminishana uongo hapa

Kwenye kusaidia raia legelege na kwenye rushwa na kupiga RAIA wasio na silaha wako strong sana tu.Huo ndo ukweli hamna uongo hapo. Wangekua wanafanya kazi zao kwa haki wasinge kua wana chukiwa na kila RAIA.
 
Mafunzo ya polisi Yana mapungufu makubwa, haiwezekani kila wakati wakawa wanaporwa bunduki na mbaya zaidi intelejensia yao imeshindwa kudhibiti uporaji wa bunduki wajitazame upya.
 
Mafunzo ya polisi Yana mapungufu makubwa, haiwezekani kila wakati wakawa wanaporwa Silaa na mbaya zaidi intelejensia yao imeshindwa kudhibiti uporaji wa Silaa, wajitazame upya.

Kweli mkuu hata mimi nahisi hili ndo moja ya mapungufu.
 
Kweli aisee, na inaonekana wenaowachukia Polisi wengi wao ni CHA KUFIA NINI. Yaani hana cha kupoteza hata nchi ikipinduliwa leo. Wanatamani vita/machafuko/ujambazi labda watatokea huko.

Hadi muda huu naandika haya ni kwasababu kuna watu wanakesha kazini. Tusiangalie mapungufu tu, hata mafanikio ni muhimu kuyasema.
kama si panga,rungu,na mkuki wangu vibaka wangeshanimaliza zamani,wewe unaishi maeneo gani,ikulu?huku kwetu ni mjini lakini polisi usiku wanalinda maduka ya wahindi na benki tu,kwetu hawana time napo,wapigwe tu.
 
Lisikie kwa mbali tu Jambaka ni hatari sana, polisi wetu wapo ktk wakati mgumu sana, Mungu awalinde.
 
Nyinyi vilaza hamna sababu ya kuwachukia polisi wetu hata siku moja wewe unaleta uchama wako kwenye mambo ya national security
 
Lkn wakipigwa wao tunawaita legelege. Wakipiga tutasema wanatumia nguvu/ubabe. Nahisi kuaminishana uongo hapa

Wanaonea raia wema wasio na silaha, yaani police mkakamavu una smg kibaka anakusogelea na panga, huyo police gani, anafaa aende kufanya kazi zingine siyo hiyo
 
Kwenye kusaidia raia legelege na kwenye rushwa na kupiga RAIA wasio na silaha wako strong sana tu.Huo ndo ukweli hamna uongo hapo. Wangekua wanafanya kazi zao kwa haki wasinge kua wana chukiwa na kila RAIA.

Sikatai unavyowachukia polisi, una sababu zako!

Ninachotaka mimi tusiishie kuwachukia polisi tu...twende mbele na kujiuliza ni nini kinasababisha haya? Tuichukie mifumo ya uendeshaji nchi, tuwachukie watunga sera maana ubovu wa watendaji wa huku chini ni matokeo ya ubovu wa sera na mifumo!
 
I like this kind of comment
 
Umeambiwa usibebe SMG kilegelege wewe umebeba na Mimi nasema UPIGWE TU!
 
Back
Top Bottom