Polisi ajitambulisha yeye ni MTANGANYIKA

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,358
153,996
SUALA la Muungano limeibuka karibu katika kila mkutano wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Mabadiliko ya Katiba, ambapo juzi askari Polisi Josephat Mwamunyange, alijitambulisha mbele ya mabosi wake, kuwa yeye ni Mtanganyika.

Akitoa maoni mbele ya wajumbe hao kwenye kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, ya 411 KJ, Ruhuwiko, wilayani hapa, Mwamunyange alisema yeye si Mtanzania bali Mtanganyika.

"Mimi ni Mtanganyika, si Mtanzania … Muungano unanufaisha wakubwa na kutuacha sisi masikini. Zanzibar wanatubagua, niliwahi kwenda katika safari ya mafunzo nikiwa kidato cha tatu, hata namba ya mpirani sikupewa, kwa kuwa natoka Bara," alisema Mwamunyange.

Polisi huyo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), alitaka Muungano uvunjwe na kuongeza kuwa wakati Wabara wanabaguliwa wakiwa Zanzibar, Tanzania Bara, Wazanzibari wamegeuza kuwa ‘shamba la bibi' bila kufafanua, lakini akaongeza kuwa kwa bibi ndiko hata ukirudi nyumbani saa saba usiku, hasemi neno.
 
Nadhani ndiyo utaratibu unaofaa kuutumia kwa sasa!! Hakuna haja ya kuendelea na mazingaombwe ya muungano!!
 
I like it, big up afande nimekukubali na huo ndo ukweli, mimi wakati nipo Muhas tulikuwa na mshikaji mzanzibar jamaa tukawa tunaishi naye vizuri kama ndugu, mimi na wenzangu tukapangwa intern Mnanzi mmoja nilishangaa jamaa kama hatujui na anasaidiana na wenzake kutubagua eti sisi wabara tulikuwa tukimbagua. Sioni haja ya muungano kwa sasa bora uvunjike ili tujue tunanchi jirani na twende kwa passports kuliko ilivyo sasa mara mkaazi sijui pakaenda pakarudi watoke zake wajinga sana wazanzibar.
 
Wewe ulitaka ajitambulishaje wakati nchi moja kati ya mbili zilizoungana imeisha jitangazia uhuru.
 
Mtikila alikwenda kudai uhuru wa Tanganyika Newyork(UN) mwaka 1995, wakasema ana kichaa. Akauliza, tuliunganisha nchi mbili Tanganyika na Zanzibar; leo hii kuna serikali ya Tanzania na Zanzibar. Serikali ya Tanganyika aliuziwa nani? Bila kupepesa macho ndugu zetu wazenj ni wabaguzi sana ukiwa Zenj. Ni sisi tunaowang'ang'ania wao. Imefika wakati washuke migongoni mwetu! Big up afande!
 
Tutafika.
Kama Jaji Warioba alikuwepo lazima alikasirika sana. Warioba ndie aliyefuta neno Tanganyika na kuingiza Tanzania bara.(kwa amri ya bosi wake)

Nashauri tuache kutumia hili jina Tanzania bara badala yake tuige mfano wa polisi, mtanganyika, Tanganyika.

Pia hili wabara tuliache. Watanganyika ni sahihi.
Watu wa Mafia na Ukerewe ni wabara au wavisiwani?
Na watu wa Zanzibar ni wazanzibari au wavisiwani?

Soma hapa link mtanganyika

Tanzania ipo na muungano wa baadhi ya mambo baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Ni sisi tu wadanganyika ndio tunajisahau. Muungano haufuti jina la sehemu(mshiriki)
link uknanchizake
 
Huyo lazima atahamishiwa kulee! Chezeiya maagizo ya wakubwa weye!
 
Mchakato wa katiba mpya unaendelea wadau,wala msitoke povu humu jamvini twendeni tukatoe maoni yetu!Hata mimi binafsi natamani siku moja kujitambulisha mbele za watu kama mtanganyika,kwa kweli wazanzibari si sehemu yetu kabisa hata kidogo na sioni tunanufaika vipi na muungano wa namna hii ambao kila pande wanalalamika.
 
Hao ndo wanyakyusa bwana, hawapepesi macho wanahit to the pont,. Mtauliwa sana awamu hi kwa kuongea ukweli
 
Ngoja mtikila aanze kushughulika na hii issue, manake currently nadhani hana kesi nyingine.
 
Ndio malipo ya kula na vipofu halafu unawapush-push mikono yao kwenye sahani kutaka ule vyote wewe peke yako. Anayekulalamikia unamwua. Wakigundua hila zako mbaya inakula kwako.
 
Tumefika hapa kutokana na unafiki wa ASP+TANU na sasa CCM kwa kuficha ukweli kuwa 1963 zanzibzr kulifanyika uchaguzi huru,wa haki na vyama vingi.

Japo Asp walipata viti 11 vyama viwili kutoka pemba viliungana na kuwa na viti 13 hivyo kuunda serikali ambayo ndiyo iliyopinduliwa 12january1964 kabla ya kuapishwa.
Hii ndio siri bendera ya zanzibar haina rangi nyekundu kuashiria kupata uhuru kwa kumwaga damu,maana mapinduzi yale yalipindua matokeo ya uchaguzi huo huru na wahaki kwakuwa hakuna yaliyepinga matokeo yale.

Baada ya hila hizo za mapinduzi wakijua hali itakuwa tete kiusalama wakaamua kuungana fasta miezi 3 baadae 26April1964 ili wapate ulinzi kijeshi toka Tanganyika jambo linaloendelea hadi Leo hii.

Kama haitoshi 1977 wakaungana vyama na kuzaiwa CCM. na kuingizwa msamiati TANZANIA BARA na muungano kupoteza uhalisia wa muungano wa awali uliosema wazii ZANZIBAR + TANGANYIKA = TANZANIA wao wanafiki sikuhizi wanaita Zanzibar na tanzania bara .
Huu muungano sio wa CCM wa kuamuliwa kwa maslahi yao hivyo kwanza WAZANZIBARI na WATANGANYIKA wakae nchini mwao waamue kama tuna uuhitaji tena, ndipo tujadili uwe vipi kisha ziwepo katiba ya zanzibar na Tanganyika kisha IUUNDWE KATIBA YA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO TANZANIA nasio ujadiliwe na CCM DODOMA AU WATANZANIA BARA!!! (wadanganyika tumefumbuka).
Nadhani ndiyo utaratibu unaofaa kuutumia kwa sasa!! Hakuna haja ya kuendelea na mazingaombwe ya muungano!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom