kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,247
- 16,169
Humphrey PolePole ni kama vile alikuwa akiwahutubia vijana wa bodaboda ambao wengi wao hawakuwepo wakati wa Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete na namna walifanikiwa kuwa Marais wa Tanzania.
Pia alifanikiwa kutuambia kuwa nyuma yake wako pia akina Mzee Warioba na wazee wenzake wa kanda ile.
Na mwisho amefanikiwa kuonyesha kuwa kuna vita ya udini kwenye uongozi; hasa baada ya kuonyesha kuwa Mkapa alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya matangulizi wake Mzee Mwinyi (mwislam) na Magufuli alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya Jakaya (mwislamu). Kwenye hili Polepole alisema kuwa unapogombea kwa mara ya kwanza kura utakazopata sio za kwako, bali za Rais aliyekukabidhi kijiti. Hapa natofautiana nae kabisa, kwakuwa kwenye uchaguzi wa 1995 Mkapa alikuwa hajulikani ukilinganisha na mgombea wa upinzani; Lyatonga Mrema. Mwl Nyerere ndiye aliyemsaidia kupiga kampeni vinginevyo angedondoshwa; sio kwasababu ya udhaifu wa uongozi wa Mzee Mwinyi. Mwl Nyerere alidiriki kusema hawezi kulala nyumbani eti kwasababu ya ubaba wa taifa, wakati yuko jukwaani akasema "I can not let my country go to the dogs". Hivyo tatizo ni CCM kumsimamisha mgombea (Mkapa) ambae hajulikani kwa watu.
Magufuli alipata kura chache uchaguzi wa 2015 kwasababu Lowassa alikuwa na nguvu kuliko JPM, sio kwasababu ya uongozi wa JK ulikuwa mbaya. Hapa Humphrey anaongelea udini kwakuwa anafahamu kuwa uchaguzi wa 2020 JPM alishinda kwa kuwaengua wapinzani wote na kuiba kura.
Nijuavyo mimi Humphrey na wenzake wataashindana lakini hawatashinda hii vita ya udini.
Humphrey anawadanganya watoto wachanga kuwa mchakato wa katiba ulivunjika kwasababu ya rasimu ya katiba ilikuwa inawabana viongozi wabadhilifu ndiyo maana JK aliikataa. Huu ni upuuzi sawa na upuuzi mwingine kwakuwa katiba mpya pendekezwa ingeanza kufanyakazi baada ya uongozi wa JK kumalizika na kuondoka madarakani; hivyo, JK hakuwa na sababu ya kuiogopa katiba ambayo ina masharti magumu kwa viongozi. Sababu ya kweli ya kuvunjika uwandishi wa katiba mpya ni Mzee Warioba na Polepole ambao walikuwa wanataka muungano wa serikali 3 badala ya serikali 01 ya sasa; hoja ambayo ilikuwa inahofiwa kuwa itakwenda kuvunja muungano hasa baada ya kuungwa mkono na UKAWA.
The main agenda sasa imefahamika kuwa ni UDINI, UDINI, UDINI kwakuwa kuna watu hawakutaka Samia (mwislamu) kuwa Rais baada ya JPM kufariki. Hii ni ajenda ya kidini kabisa, hakuna lingine hapo. Walimkataa hata kabla ya kujua ataongozaje atakapoapishwa. Sasa tuko tayari watanzania kwa hili.
View: https://youtu.be/0j3WOvqNL_A?si=LrrfTy6_Ek55Bzso