Polepole fuata sheria za kazi, saa 3 usiku siyo muda wa kazi

Hakuna kitu muhimu hapa duniani kama familia yako! Kila kitu tunachokifanya ni kwaajili ya familia. Hata kama hiyo familia ina mtu mmoja tu _ Wewe!
Nadhani na yeye ana familia. Ni vyema kuwa na moyo wa kujitolea kwa manufaa ya taifa. Tuwaombee wasichoke.
 
Hakuna muda wa kustarehe na familia hapa kwani hata yeye pole pole anafamilia pia lakini anapiga kazi muda wwte...nakuunga mkono mh.pole pole piga simu hata sa 8 usiku

Kama wananchi hawajaanza kupata raha viongozi wanapata wapi hiyo raha?
Tena walio viongozi wake na waume zenu waskie na waelewe kwamba hakuna atakaepata raha mwaka huu
 
Katibu mwenezi wa CCM na Mbunge wa kuteuliwa anaendesha kipindi mubashara cha "Papo Kwa Papo" saa 3 usiku lkn anawapigia simu watendaji wa serikali akitaka watolee ufafanuzi baadhi ya kero za wananchi...
Hiv bado ana nafasi ya katibu mwenezi au tayari ni mbunge.Mbunge kumpigia mtendaji usiku ni ukiukwaji wa haki za kiajira. shughuli zote za serikali mwisho saa 12 jioni,isipokuwa zile za ulinzi na usalama wa maisha na mali za raia
 
Hiv bado ana nafasi ya katibu mwenezi au tayari ni mbunge.Mbunge kumpigia mtendaji usiku ni ukiukwaji wa haki za kiajira. shughuli zote za serikali mwisho saa 12 jioni,isipokuwa zile za ulinzi na usalama wa maisha na mali za raia
Hata ingekuwa saa 4 asubuhi, Polepole hana mandate na watumishi wa serikali.

Kuna namna ya chama kuisimamia serikali lakini siyo hivyo anavyofanya Chakubanga.
 
Mwenyezi Mungu, Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika Jibril pamoja na Mikaela, Wasomi wote duniani, wenye Akili nyingi na Mimi Mwenyewe.
Unajitafutia laana bure wewe banyamulenge.
Unamhusishaje Mwenyezi Mungu na Yesu Kristo na baba la uovu!
CCM = Uovu.
 
Hizo kazi zenyewe kila wakati wanajisifu kuzichapa mbona hatuoni positive outcome kwa raia wa kawaida?!

Wanadhani kuongea sana na kuteka vyombo vyote vya habari ndio maendeleo ya nchi, wacha waendelee kujidanganya, wanajua fika hao watazamaji wameshawachoka.
Kwa uchache japo umesema huzioni hizo kazi:
1.Ada shule za msingi na sekondari
2.Nafuu ya foleni Ubungo baada kukamilika fly Over
3.Ubunifu wa Vitambulisho vya machinga,Kwa sasa wapo huru kibiashara huku wakichangia kodi serikali yao
4.Ujenzi wa Barabara nchini
5. Na kadhalika.
Ila mkuu kwa jinsi ulivyojipanga kupinga hapo najua utasema hayo ni maendeleo ya VITU, Kama vile ADA yanalipiwa mawe....!!
 
Wala huzimi simu
Unasema ulipo network shida inakatikatika
Huku unaikata mwenyewe hadi anashika adabu

Wenzio wanaweza kwenda hadi kampuni ya simu kuwauliza mtu fulani naumber .....Alikuwa Eneo gani ambalo mtaandao unasumbua?
Na Kuna Simu yeyote amepokea au kupiga siku hiyo na Muda huo au karibu na huo?
Makampuni ya simu yanatoa tuu taarifa chaaap!?
Hahahah
 
Wenzio wanaweza kwenda hadi kampuni ya simu kuwauliza mtu fulani naumber .....Alikuwa Eneo gani ambalo mtaandao unasumbua?
Na Kuna Simu yeyote amepokea au kupiga siku hiyo na Muda huo au karibu na huo?
Makampuni ya simu yanatoa tuu taarifa chaaap!?
Hahahah
Waende tu...
 
Kwanza Polepole hana mandate na watumishi wa serikali.

Na hata watumishi wa ccm pia hana mandate nao, ni katibu mkuu na mwenyekiti.
Inavyoonyesha watu wengi humu hawalitambui hilo. Uwajibikaji wa serikali dunia nzima unafuata protocol zake, sio kila MTU ni msemaji au kila mtu waweza mhoji na au kila MTU ni mhojaji.

Hata Kinana aliwafundisha CCM kuwa kama waziri au mtendaji yeyote wa serikali anakwenda hovyo wao vikao ndio vina mhoji bosi wao (Rais kwa ngazi ya taifa, RC kwa ngazi ya mkoa au DC kwa ngazi ya wilaya) kwa nini Fulani hatekelezi ilani ya chama na sio Polepole au Bashiru kumpigia simu Waziri au mkurugenzi au DMO kumuuliza.

Je, kama alipokea maagizo toka kwa Rais huko hakuta kuwa kumchongea Rais na wananchi kama maagizo hayo yalileta sintofahamu?
Polepole na Bashiru waache kiherehere cha kijinga, kazi za kiserikali sio kama za chama za uongo uongo. Kwamba Leo unasema hivi na kesho vile, huko ni kanuni na sheria tuu
 
Back
Top Bottom