Polepole amefanya nimwelewe Magufuli


Magufuli aliukataa mfumo mzima wa upinzani wakati alipaswa apambane na hao "wasaliti" na sio kutaka kufuta kabisa mfumo wa vyama mbadala...

Tazama sasa madhara ya alichokifanya sasa, hakuna mbadala na wenye CCM 'wamemuondoa' na wala hakuna wanaoweza pambana na jinamizi CCM...
 
Ukanda siyo kweli.... Hizi ni propaganda tu. Ila la kukataa kukosolewa ndiyo linaloleta ukakasi. Jee ilikuwa ni tabia yake ya asili au ni matokeo ya taarifa alizokuwa anapewa?
Mkuu, heshima sana. Uko sahihi. Kwangu mimi nasema Magufuli alikuwa anajua chanzo cha matatizo yetu, lakini hakuwa na uelewa wa namna ya kuyaondoa. Alikuwa anatumia nguvu kuliko akili. Na pia alikuwa anapenda kuabudiwa na mtu ukimsifia kidogo tu japo kwa unafiki, anakuamini na kukusogeza karibu. Na tatizo lake kubwa ni kudhani CCM ikibaki peke yake basi ataweza kui-control Tanzania kwa urahisi. Kwa kifupi hakuwa anataka challenge ya aina yoyote. Huwezi kuwa rais mwenye maono halafu ukalazimisha watu kama kina Kibajaji ndiyo wawe wabunge. Hata kumwacha Samia awe makamu kwenye uchaguzi wa 2020 lilikuwa ni kosa kubwa.
 
Kwani Kuna upinzani Tanzania? Mbona we mgumu kuelewa? Kwahiyo Kwa akili yako hata Sasa Kuna mtu anayepingwa na yeyote kweli au ni drama tu kuridhisha personal desires?
 
Nilichojifunza watu hawawi wema kwa kuwa aliyeko madarakani ni mwema, bali ni kutokana na mfumo unaowalazimisha wawe wema.

Makonda alifikishwa kwenye Tume ya maadili ya umma, nini kilitokea... Sabaya alifikishwa mahakamani, mahakama iliamua nini?
Ulichoandika hata chizi atakucheka, hizo tume na mahakama zimeundwq au zinasimamiwa na nani?. Magufuli hakuwq na wema wowote wala hakuna mwanaccm atakuwa mwema kwa Taifa!. Wote wanapambania maisha yao... Huyu polepole angekuwa ndani ya mfumo angeyasema haya?.
 
Sema tena na tena. Alikuwa anatumia approach ya ajabu kabisa kwenye kuongoza. Nikupe mfano mwingine: Polepole anasema yule mbunge mjinga aliyependekeza eti Magufuli aongozewe muda wa urais, alitumwa na wana mtandao ili kumfanya Magufuli aonekane kuwa ni mroho wa madaraka. Well, inaweza kuwa ni kweli. Lakini hatua alizochokuwa ku deal na huyo mbunge zilikuwaje? Alimwita Polepole na kumlalamikia kuwa anahujumiwa na mtangulizi wake na kumwambia aseme kuwa Magufuli hataki kuongezewa muda. Je, alifanya nini kwa huyo mbunge mjinga ambaye alikuwa anamhujumu? Mbona hatukusikia anapewa onyo au adhabu nyingine yoyote?
 
Kwani Kuna upinzani Tanzania? Mbona we mgumu kuelewa? Kwahiyo Kwa akili yako hata Sasa Kuna mtu anayepingwa na yeyote kweli au ni drama tu kuridhisha personal desires?

Naona tuna mitazamo na uelewa tofauti wa siasa za Tanzania zilivyo na zinavyopaswa kuwa, hatuwezi fika muafaka...

Naona bado umekazana kutazama "ilivyo" na sio "inavyopaswa kuwa"...

Na kwa mtazamo wako huo maana yake hata hakuna haja ya kuwa na vyama including CCM kwa sababu watu wote kwenye siasa ni corrupt...
 
Uhakika, watu wetu hawawezi ku reason
 
Pamoja na hayo mazuri, mabaya yalikuwepo pia.
 
Kwani Kuna upinzani Tanzania? Mbona we mgumu kuelewa? Kwahiyo Kwa akili yako hata Sasa Kuna mtu anayepingwa na yeyote kweli au ni drama tu kuridhisha personal desires?
Mawazo ya kijinga kama haya ndiyo yalimwangusha Magufuli na yakatufikisha hapa. Haya nikubaliane na huu ujinga kuwa hakuna upinzani wa kweli... kwa nini wasiweke mazingira mazuri kwa upinzani kuwepo kwa sababu ni jambo muhimu sana kwa nchi?
 
Magufuli alisema mtamkumbuka kwa mazuri yake.
 
Vipi kuhusu;-
1. Tsh 1.5 Trillion zilizoibuliwa na CAG 2016/17 na kisha kumfukuza CAG kazi

2. Fedha za Plea bargain feki alizokuwa anakusanya na DPP Biswalo Mganga na kuzificha China

3. Ununuzi wa ndege kupitia Boeing bila kufuata sheria ya manunuzi ya umma??

4. Mikataba ya akina Mayanga construction kujenga Chato International Airport

Nimesema machche lakini nataka nikuhakiishie hata Magufuli hakuwa na uchungu na mali za umma, bali alikuwa ni fisadi sawa na mafisadi wengine wa CCM.

Sina huruma naye kwa kuwa hata yeye Magufuli alikuwa anapanga kuwauwa wenzie, ni kwamba tu walimtaimu akaondoka yeye.

Polepole hana jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…