Polepole aachwe aongee asinyamazishwe, asizuiwe

Polepole aachwe aongee asinyamazishwe, asizuiwe

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
365,910
Reaction score
845,837
Muogope sana mtu mkimya, muogope sana asiyeongea maneno mengi, ni ngumu kumjua hisia zake ni ngumu kumjua maumivu yake .. Ni ngumu zaidi kumjua anawaza nini

Mfurahie muongeaji sana, sometimes tunaita kubwabwaja,huyo katikati ya kujiachia kwake kuna mahali atajisahau na kuongea asivyotegemea au ambavyo hakupaswa kuvitamka hadharani!

Ni katika kuongea kwake sana ataihabarisha hadhira bila kujua vitu na mambo mengi yaliyokuwa yamekosa majibu.. Muongeaji sana ni mropokaji na mropokaji ana faida nyingi nzuri na mbaya kutegemeana na upande

Vipindi vya Polepole kwenye vituo vya luninga bila kujali vinafadhiliwa na nani vinatupa somo muhimu sana ya kwamba binadamu ni nani katika uhalisia wake.. Hasa pale unapompoka hadhi na sahani yake!

Vipindi vyake vinamuumbua yeye mwenyewe na kumuacha uchi wa mbuzi kwa kiwango kikubwa cha unafiki anachoonesha kwakuwa anatambua wazi anachokifanya sasa, angetokea mwingine akakifanya wakati ule wa mwendazake pengine hata kaburi lake lisingeonekana, kama sio kupotezwa huko kwenye jela za mbali nknk

Maneno ya polepole yanafunua mengi mabovu na mabaya ya utawala uliopita na kwa sehemu yanaweza kutengeneza ushahidi siku itakapotokea huko mbeleni zikafunguliwa kesi za kikatiba na jinai..

Kwa kutokemewa wala kukaripiwa anapata mzuka na kufunguka zaidi na hapo ndio wengi wanapataka

Ameanza kuzungumzia kuhusu wahuni ambao walipaswa kumalizwa ndani ya chama lakini kwa bahati mbaya kudra za Mwenyezi Mungu zikapindua matokeo

Sasa Polepole atawajibika ikibidi awataje wahuni waliomalizwa na orodha ya wahuni ambao walikuwa 'hawajamalizwa'.. Na walitumia mbinu na njia gani 'kuwamaliza' wahuni ndani ya chama.. !

Anaupiga mwingi kwa raha zake, akimaliza mtori atazikuta nyama chini..Taharuki ni pale atakapokuta ni nyama ya fisi wakati keshakunywa mtori wote
 
Madaraka yakikutoka ghafla bila kutaraji,upo ugonjwa unaokuingia mwenye I.Q,kubwa pekee huweza kuhimili hili,unless otherwise unaweza kuwa kama mwehu,I must congratulate Mr.Bashiru,ameweza kukontrol hii situations.
 
Taharuki ni pale atakapokuta ni nyama ya fisi wakati keshakunywa mtori wote
Pcha hazionekani, Jaribu kuweka Tena
jf.jpg
 
Madaraka yakikutoka ghafla bila kutaraji,upo ugonjwa unaokuingia mwenye I.Q,kubwa pekee huweza kuhimili hili,unless otherwise unaweza kuwa kama mwehu,I must congratulate Mr.Bashiru,ameweza kukontrol hii situations.
Nadhani suala la Bashiru kua mtumishi wa umma kwa muda mrefu limemfanya kujua Nini maana ya kuheshimu mamlaka hata Kama hupendi.Sasa huyu mwingine mzee wa Vieite amekulia huko kwny ma NGO's hawezi kujua "maadili" ya huko serikalini.
 
Lazima aonje jiwe la moto, kipindi chake aliumiza watu wengi sana. Ngoja aone umuhimu wa uhuru wa kujieleza maana alivyotufanyia kwa kweli sina hamu nae hata robo. Angelazwa hata jela ama atekwe na wasiojulikana ili aone Watanzania tulipitia kipindi gani enzi ya uongozi wake.
 
Na Ni mmoja Kati ya wahuni ambao wamesahauliwa kushughulikiwa na serikali.
 
Lazima aonje jiwe la moto, kipindi chake aliumiza watu wengi sana. Ngoja aone umuhimu wa uhuru wa kujieleza maana alivyotufanyia kwa kweli sina hamu nae hata robo. Angelazwa hata jela ama atekwe na wasiojulikana ili aone Watanzania tulipitia kipindi gani enzi ya uongozi wake.
Aliingizwa bungeni kufacilitate process za atake asitake, tutamlazimisha.
 
bwana pole pole, mmiliki wa mbwa wawili, fighter na tiger🤣 na ka vieitte kamoja, na unafiki mwingii
 
Mbona polepole alishafafanua kuhusu wahuni ni wapiga dili, wala rushwa, wakwepa kodi n.k

Mmeshapeleka mawazo yenu kuhusu wahuni ambao hawajamalizwa kwamba kuna watu walitakiwa kuuliwa
 
Back
Top Bottom